Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

Pesa ya ada,ya michango,ya kanisa,ya dhamana ogopa sana do try this Zina laana Huwa hazirudi ukisema chomoa kidogo
 
Labda zamani siku hizi unampaje mwanafunzi akalipe Ada, nenda nae bank au kwa wakala mpe risiti apeleke shule
 
Labda zamani siku hizi unampaje mwanafunzi akalipe Ada, nenda nae bank au kwa wakala mpe risiti apeleke shule
Mimi wakati nasoma nimepewa sana ada hadi milioni na sikuwahi kula hata 100
 
Very interesting
 
Katika kitu ambacho najisifu mpka leo ni kupita salama kipindi cha utotoni na kipindi cha mihemuko cha form 2,3,4,5&6 bila kudinywa...hapa watu watakataaa hahaha [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
Hongera kama ni kweli
 
CHAPTER 12

mguu kwa mguu mpaka kwa mganga tukamkuta mganga yupo macho anafanya tiba tiba zake kuna moto unawaka pale nje kwake lakini pia tulimkuta mwanamke nadhani yule ni mkewe nilimjua kama mkewe baada ya story story hapo mbele lakini pia tulimkuta mwanamke jimama la nguvu jeupe limekaa pale pembeni ya moto hivi.

kichwani nywele zipo wazi ana kitambaa cheusi kajifunga kama taulo kiunoni hivi lakini kifuani yupo wazi kabisa. yani kifua kinaonekana kabisa mitindi unaiona ile pale.

siku hiyo baada ya kuliona lile tukio ndo nikaamini kama uchawi upo na wanawake wanapenda ushirikina kuliko hata wanaume....


INAENDELEAAAA....

Lile tukio liliniogopesha kiasi fulani hivi ila ilinibidi nijikaze tu maana ndo tumleta mgonjwa tena.

wakati mganga akiendelea endelea na tiba zake nilikuwa nasikiliza maongezi yake akiwa kapandisha na lile jimama jeupe lililo nusu uchi.

Katika maongezi yake na mganga nilitambua kuwa lile jimama shida zake ni mbili na ndo maana yupo pale kwa mganga shida ya kwanza alikuwa naitaji mtoto ndoa yake ina kama miaka 17 hivi lakini hakubahatika kupata mtoto na manyanyaso na maneno yamekuwa mengi sana upande wa mumewe.

Lakini pia mganga alimwambia kuwa amelogwa lakini mganga akasita kidogo akamuuliza vipi unataka kumjua aliyekuroga akasema

"Ndio namtaka kumjua"

Jibu lilotoka kuwa aliyemroga ni mama yake mzazi. Lile jimama alikushtuka sana kivile maana sijui kama lile janamke sio dangaji la mjini.

Mambo yao yakaendelea weeeh mda uo me na uncle tunatazama mchezo tu lile jimama likamaliza tiba na yule mganga likavaa nguo zake hilo likaondoka zake. Kabla hakujapambazuka vizuri.

Inshu sasa ikabaki upande wetu na ostadh. Kuna mda nilijaribu kumshauri mjomba kuwa tusiseme tulienda wapi mpaka mwenzetu akakutwa na tatizo tuseme tu kuwa tulikuwa tunawahi gari ya asubuhi tukakutana na tatizo ila dakika ya mwisho uncle akuwa upande wangu alipoulizwa imekuwaje kuwaje.

Ikabidi aseme tu kuwa tulikuwa tunatoka kule shimoni kunakosadikika kuna madini.

Mganga akasema " imekuwa vizuri kusema ukweli lakini tiba ya huyu mwenzenu inahitaji vifaa na vifaa vinahitaji pesa na laiti kama mungesema mumkimbize hospital basi hata uko hospital musingefika nae angekufa njiani , huyu mda huu kuna mdudu kamvaa mwilini ... Akuishua hapo tu akatupa na kisa kinachofanana na chetu kuwa kuna mtu hapo hapo kijijini alishawahi kukutwa na madhira kama ayo.

Jamaa alikuwa na balaa watu wakajua kashafika akaswaliwa fresh maana alikuwa muislam ila dakika ya mwisho pale kaburini wanataka kumfukia sasa jamaa akapiga chafya... Lakini maamuzi yaliyotoka kuwa watu wapeleke mchanga chini tu haina jinsi"

Daaaah hapo akili sasa nadhani ndo ilizidi kupagawa maana tulipanga tunaenda mkoa X kijiji X kwa kwenda na kugeuza lakini sasa tunaambiwa tutulie siku kadhaa mpaka mwenzetu apone.

Uncle akatoa pesa baada kidogo akatoka na mganga sikujua wameenda wapi ila walivyorudi warirudi na vitu vya kiganga ganga hivi.

Mimi wakati wanatoka nilikuwepo na mke wa mganga tukawa tunapiga story story za hapa na pale kuhusu mazingira ya pale kijijini kiujumla. Katika maongezi yetu kuna mda akapigiwa simu kuna mtu akaongea nae huyo mtu nilisikia anamuita "MAMA SOMOE"

Kwa maongezi yao nilisikia kama mama somoe anataka kuja siku ya pili yake kuja kuwatembelea lakini pia kwa ajiri ya matatizo ya mtoto wake ambae ni Somoe.

Ujue sikujiuliza sana huyo MAMA SOMOE ni nani nilidhani ni mtu wa kawaida tu lakini jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.

Uncle akarudi na mganga mda uo ostadh yupo ndani ya banda la udongo tu. kalala tu mda wote.

baada ya kurudi na vifaa mganga alisema kuwa tiba ya ostadh itafanyika usiku lakini pia mkewe amuandalie chai mapema sana kwa ajiri ya usiku wakati wa tiba.

usiku ukafika bhana mganga akaimba imba nyimbo zake weeeh akishiriana na mkewe akawa anaitiki tu. akapandisha akaongea ongea mambo mengi sana lakini dakika ya mwisho akatoa maelezo kuwa kama tutataka kwenda tena shimoni basi twende kwake kwanza kupata dawa akataja na dawa kadhaa kwa ajiri ya ostadh inshu ya ostadh kiupande mmoja ikawa teyal imeshaisha tunasubiri apate nafuu tu tusepe mjini.

Sasa mida kama ya saa 4 asubuhi hivi inakimbilia saa 5 nipo na uncle hapo mda uo tukasikia mlio wa bodaboda mda uo sisi tulikuwa tumekaa tunapiga story nyuma ya nyumba ya mganga kwahiyo ilikuwa ngumu kumjua ni nani aliyekuja na bodaboda.

daaah kuna mambo yasikie tu kuna ile kauli inasema binadamu wanakutana ila milima ndo akiukutani ni ya kweli 100%.

ile nimenyanyuka naenda kunywa maji uso kwa uso na NAA tena round hii akiwa kabeba mtoto moyo ulipiga paaaaah kushituka na akili ikanijia fast kuwa inawezekana Naa ndio MAMA SOMOE mwenyewe ambae alikuwa anaongea na mke wa mganga siku ya jana.

Ndani ya mda mfupi nilipatwa na maswali kama yote hivi

nilijiuliza

1. NAA ATAREACT VIPI BAADA YA KUONANA NA MIMI ?

2. LAKINI IMEKUWAJE ANA MTOTO ?

3. MTOTO KAZAA NA NANI ?

4. VIPI KUHUSU SHULE ?

Gusa hapa kupata muendelezo πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Post in thread 'Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike' Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…