Mambo 16 niliyojifunza kwenye hotuba ya Rais Samia - Januari 4, 2022

Mambo 16 niliyojifunza kwenye hotuba ya Rais Samia - Januari 4, 2022

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Yafuatayo ndio nimejifunza kutokana na hotuba ya Jana.

1. Rais amekasirishwa na maoni yaliyotolewa na speaker Ndugai kuhusu mikopo.

2. Rais amemshambulia speaker Ndugai at individual capacity na sio Kama speaker kwenye maoni kuhusu mikopo.

3. Rais amehaidi kukopa zaidi na mpaka Sasa wamepata commitment ya trillion 7 Kama mkopo nafuu.

4. Mikopo anayochukua Rais Samiah ni ya masharti nafuu, kwa maana hayana riba.

5. Serikali kwa Sasa inakopa ili ikalipe madeni ambayo yameanza kumature.

6. Rais anaamini ya kwamba maendeleo yanapatikana kwa kukopa.

7. Rais anaamini yeye siyo Rais wa Kwanza kukopa na kwamba huko nyuma tuliwahi kukopa sana mpaka tukaitwa high indebtet country.

8. Rais anaamini kwamba mkopo wake ndio Bora kuliko mikopo mingine yote ambayo awamu zingine zilizopita zilikopa.

9. Rais amekiri tozo ni kidogo haziwezi kuleta maendeleo, hivyo tutakopa na kutoza kwa wakati mmoja.

10. Rais anaamini kwamba wananchi wameridhika na tozo hivyo tozo zitaendelea sana.

11. Rais amekiri ya kwamba Tanzania sio ya kwanza kutoza hata nchi kubwa huko zina tozo nyingi.

12. Rais anaamini adui yake mkubwa yupo ndani ya CCM na sio upinzani.

13. Rais hafanyi maendeleo kwa ajili ya mwaka 2025, Bali kwa ajili ya Watanzania.

14. Rais anaamini kuna baadhi ya mawaziri wanafanya kazi kwa ajili ya 2025, na anania ya kuwaondoa.

15. Rais anaamini wanaompinga kwa Sasa Ni wale waliokuwa wanamdharau kwamba hataweza majukumu ya kuleta maendeleo Sasa wanashangaa anafanya maendeleo.

16. Mwisho, nilichojifunza ni kwamba kiongozi yeyote ndani ya CCM atakaye toa maoni tofauti kwenye suala la mikopo atachukuliwa ana malengo ya kumpinga Rais na yupo kwenye kundi la maadui linalotaka urais.

Wewe Kama mwanajamii forum ulijifunza Jambo gani kutoka kwenye hotuba ya Rais Jana?.
 
1. Rais amekiri ya kwamba Tanzania sio ya kwanza kutoza hata nchi kubwa huko Zina tozo nyingi.

Nchi nyingine kuwa na tozo nyingi sio sababu ya nchi yetu pia kuwa na mlolongo wa tozo kwani impact ya hizo tozo katika kila nchi ni tofauti kwa wananchi wake depending on the economic configuration ya nchi husika.

Kama Samia ataendelea kukopa at ZERO interest rate hiyo itampa afueni ya kuwapunguzia mzigo wa tozo wananchi. Samia asijidanganye one of the most pressing issues that has impacted negatively on the ordinary people ni hizi tozo kwenye miamala ya simu; na hizi zilikuja kwasababu mabenki yalikuwa yameshindwa kushindana na huduma za fedha zilizokuwa zinatolewa na makampuni ya simu!

Banks lobbied for the introduction of those charges because they could not compete, and the govt. relented to their unjustified complaints which affected the economic growth of our economy because a significant portion of the population was financially excluded.

I hope kwenye budget ijayo suala la tozo lipatiwe tafakuli ya kina na njia nyingine mbadala zitafutwe kuziba pengo la tozo kwani zipo nyingi. Unfortunately, under the current Finace minister no headway can be made on the tozo issue because he does not have what it takes to solve it. You need a financially sound person as a finance minister to achieve good results.
 
Imagine having "square pegs in round holes".

Nguzo Zina pembe nne harafu mashimo ni ya duara!

Hivo ndivyo walivyo Wana ccm,harafu Wana ccm ni wepesi sana Wana "ngozi raini na nyembamba mno".

Yaani maoni tu,Raisi wa nchi anapaniki balaa,sasa hebu fikiria tungekuwa na demokrasia kama ya Kenya,Makamu wa Raisi anakupinga wazi wazi,anakupa makavu,wqbunge wa chama chako wanakutusi hadharani!!huyu mama angekufa kwa kihoro
 
Yafuatayo ndio nimejifunza kutokana na hotuba ya Jana.

1. Rais amekasirishwa na maoni yaliyotolewa na speaker Ndugai kuhusu mikopo...
La msingi akope lakini asituletee mambo ya mgao wa zanzibar 1/3: wakati zenji ina watu wachache
 
Back
Top Bottom