Mambo 16 niliyojifunza kwenye hotuba ya Rais Samia - Januari 4, 2022

Mambo 16 niliyojifunza kwenye hotuba ya Rais Samia - Januari 4, 2022

serikali ya jpm ilikuwa ngumu mtu kuweza kukosoa kwa hofu.

serikali ya ssh unajihisi upo huru kutoa maoni au kukosoa, ila ujiandae kuchambwa
Hayo yote yanajibiwa na mtu anaitwa Tundu Lissu, aliweza kukosoa bila hofu wakati wa JPM na wala kuchambwa hakumbabaishi, tena amesema mpango wa kurudi nchini upo. Patamu hapo.
 
Ndio mkuu huu huu...we uon ulivojaa mambo!!
Duh hata sijui kesho yetu inakuwaje,: Hii ndiyo kuniambia unataka kununua kitu cha Tsh 1000/- unasema umepungukiwa unaomba uongezwe Tsh 900/-
 
W
Umejaa husda tuu Mkuu, fitna fitna hivi na mambo yafananiayo na hayo. Hivi kweli ni busara kumnanga Rais kwenye public wakati nafasi ya kwenda kumuona private kama jambo haujalifurahia unao? Sasa acha awaadabishe.
Wewe ni tongotongo
 
Yafuatayo ndio nimejifunza kutokana na hotuba ya Jana.

1. Rais amekasirishwa na maoni yaliyotolewa na speaker Ndugai kuhusu mikopo.

2. Rais amemshambulia speaker Ndugai at individual capacity na sio Kama speaker kwenye maoni kuhusu mikopo.

3. Rais amehaidi kukopa zaidi na mpaka Sasa wamepata commitment ya trillion 7 Kama mkopo nafuu.

4. Mikopo anayochukua Rais Samiah ni ya masharti nafuu, kwa maana hayana riba.

5. Serikali kwa Sasa inakopa ili ikalipe madeni ambayo yameanza kumature.

6. Rais anaamini ya kwamba maendeleo yanapatikana kwa kukopa.

7. Rais anaamini yeye siyo Rais wa Kwanza kukopa na kwamba huko nyuma tuliwahi kukopa sana mpaka tukaitwa high indebtet country.

8. Rais anaamini kwamba mkopo wake ndio Bora kuliko mikopo mingine yote ambayo awamu zingine zilizopita zilikopa.

9. Rais amekiri tozo ni kidogo haziwezi kuleta maendeleo, hivyo tutakopa na kutoza kwa wakati mmoja.

10. Rais anaamini kwamba wananchi wameridhika na tozo hivyo tozo zitaendelea sana.

11. Rais amekiri ya kwamba Tanzania sio ya kwanza kutoza hata nchi kubwa huko zina tozo nyingi.

12. Rais anaamini adui yake mkubwa yupo ndani ya CCM na sio upinzani.

13. Rais hafanyi maendeleo kwa ajili ya mwaka 2025, Bali kwa ajili ya Watanzania.

14. Rais anaamini kuna baadhi ya mawaziri wanafanya kazi kwa ajili ya 2025, na anania ya kuwaondoa.

15. Rais anaamini wanaompinga kwa Sasa Ni wale waliokuwa wanamdharau kwamba hataweza majukumu ya kuleta maendeleo Sasa wanashangaa anafanya maendeleo.

16. Mwisho, nilichojifunza ni kwamba kiongozi yeyote ndani ya CCM atakaye toa maoni tofauti kwenye suala la mikopo atachukuliwa ana malengo ya kumpinga Rais na yupo kwenye kundi la maadui linalotaka urais.

Wewe Kama mwanajamii forum ulijifunza Jambo gani kutoka kwenye hotuba ya Rais Jana?.
Ccm sii wamoja tena, na katiba mpya ndio dawa ya tuyaonayo, uhuru wa maoni chino ya ccm umwharamishwa mbali na kuwa unatambuliwa na katiba,katiba na sheria zinaweza subirishwa na wanaccm kwa katiba ya Sasa na hakuna kuwajibishwa kunakowezekana kwani wanayokinga yakutoshitakiwa.
 
NILICHOJIFUNZA;
Mbali ya kumshambulia Ndugai amewaambia wananchi kwamba tozo sitapunguza hata mkilalamika na hamna cha kunifanya.
Eti afanye nini baada ya kurithi miradi ya marehemu? Aache pengo kati ya Tabora na Dodoma kwenye njia ya reli? Aendelee kukopa kwa siri kwenye benki za kibiashara kama marehemu na kuwaambia wananchi "ni pesa yetu"?
 
Back
Top Bottom