Mambo 16 niliyojifunza kwenye hotuba ya Rais Samia - Januari 4, 2022

Mambo 16 niliyojifunza kwenye hotuba ya Rais Samia - Januari 4, 2022

Kwa vile JF wanaogopa maoni yangu na ya kuyadelete nitaongea kwa replies.

Nilichojifunza na ninachozidi kujifunza ni kuwa mwanamke sio kikwazo cha kuwa kiongozi bora. Hata hivyo kuwa mwanamke Rais Tanzania ni changamoto kubwa. Rais Samia ameshindwa kujizuia katika mambo matatu: 1Mipasho - kama mwanamke wa kibongo anashindwa kuweka mambo moyoni; lazima aseme. 2) Woga. Wanawake was Tz (si Ujerumani) kwandani hawajiamini, ni woga. Mama anaogopa kwa hiyo anajaribu kuwamaliza kisiasa wanaoweza kumfanya asiwe Rais 2025; 3) Kisasi; ànashindwa kusahau na kusonga mbele. Anawawinda wapinzani wake ndani na nje ya CCM.

Mama ana mengi mazuri. Ajifunze kwa critics wake wakati akiendelea na ajenda zake. Speech yake ya Jana (sehemu ya mipasho) ni Aibu kwa taifa.
 
Nilichojifunza,ukiwa na mawazo tofauti na mkubwa utashambuliwa kila kona.Kinachofuata kama ilivyo kawaida kwa marais wa Africa Ni kushughulikiana.Kwa Sasa Ndugai anafuatiliwa na usalama,watampoteza muda si mrefu.
 
Yafuatayo ndio nimejifunza kutokana na hotuba ya Jana.

1. Rais amekasirishwa na maoni yaliyotolewa na speaker Ndugai kuhusu mikopo.

2. Rais amemshambulia speaker Ndugai at individual capacity na sio Kama speaker kwenye maoni kuhusu mikopo.

3. Rais amehaidi kukopa zaidi na mpaka Sasa wamepata commitment ya trillion 7 Kama mkopo nafuu.

4. Mikopo anayochukua Rais Samiah ni ya masharti nafuu, kwa maana hayana riba.

5. Serikali kwa Sasa inakopa ili ikalipe madeni ambayo yameanza kumature.

6. Rais anaamini ya kwamba maendeleo yanapatikana kwa kukopa.

7. Rais anaamini yeye siyo Rais wa Kwanza kukopa na kwamba huko nyuma tuliwahi kukopa sana mpaka tukaitwa high indebtet country.

8. Rais anaamini kwamba mkopo wake ndio Bora kuliko mikopo mingine yote ambayo awamu zingine zilizopita zilikopa.

9. Rais amekiri tozo ni kidogo haziwezi kuleta maendeleo, hivyo tutakopa na kutoza kwa wakati mmoja.

10. Rais anaamini kwamba wananchi wameridhika na tozo hivyo tozo zitaendelea sana.

11. Rais amekiri ya kwamba Tanzania sio ya kwanza kutoza hata nchi kubwa huko zina tozo nyingi.

12. Rais anaamini adui yake mkubwa yupo ndani ya CCM na sio upinzani.

13. Rais hafanyi maendeleo kwa ajili ya mwaka 2025, Bali kwa ajili ya Watanzania.

14. Rais anaamini kuna baadhi ya mawaziri wanafanya kazi kwa ajili ya 2025, na anania ya kuwaondoa.

15. Rais anaamini wanaompinga kwa Sasa Ni wale waliokuwa wanamdharau kwamba hataweza majukumu ya kuleta maendeleo Sasa wanashangaa anafanya maendeleo.

16. Mwisho, nilichojifunza ni kwamba kiongozi yeyote ndani ya CCM atakaye toa maoni tofauti kwenye suala la mikopo atachukuliwa ana malengo ya kumpinga Rais na yupo kwenye kundi la maadui linalotaka urais.

Wewe Kama mwanajamii forum ulijifunza Jambo gani kutoka kwenye hotuba ya Rais Jana?.
Mie nimejifunza kwamba "ccm ni ile ile"
 
Zidumu fikra za mwenyekiti....
X: Hakuna umeme wa elfu 27, jiandaeni kulipa ile 320k iliyokuwepo, hakuna mserereko
 
Nimejifunza kwamba Kesi ya mbowe directly ina mkono wake mwenyewe na wala sio washauri au wasaidizi.

Mama ukimbeep anaweza akakupigia mpaka chaji ikaisha.

Wananchi na viongozi wasipokuwa mikono nyuma na wanyenyekevu mama anaweza akageuka Vladimir putin with iron fists.

There is no room to opinion and alternative views within CCM and that should be the case from opposition. Wakae kwa kutulia.
 
Jana kiuhalisia kulikuwa hakuna hotuba,ilikuwa ni mipasho mwanzo-mwisho.

Ilitumika jazba zaidi kuliko BUSARA.

Nchi hii ni ya watanzania wote na kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake kulingana na maono yake,ilimradi asivunje katiba.

Kuna tatizo kubwa Afrika la viongozi kupenda sifa zaidi, kuliko kuambiwa ukweli.

Ni Afrika pekee unakutana na marais wapenda sifa mfano wa yule aliyekuwa Gambia Yahya Jammeh!
 
Magu alikua anajisifia ndo kafanya vitu vingi kuliko wengine huyu nae anasema ndo mikopo nafuu Ever akaweka na kidhungu kabisa sasa dah. Anyway
 
Nilichojifunza mimi hii dunia ni ya Mungu,hamuwezi kumpiga marisasi mwenzenu kama mbwa mkabaki salama mwenyezi Mungu alimponya lissu MAKUSUDI ili ashuhudie watesi wake wakihadhilika!!

Mkuu hujajifunza. Umetoa maktaba yenu.
 
Hujaandika ulichojifunza ila umeelezea orodha ya uliyoyasikia
🤣🤣🤣🤣🤣
Kwani mtu akifundishwa kutoa na kujumulisha,si atasema nimejifunza kutoa na kujumulisha?
Na Hangaya alikuwa anatoa somo.
 
Nyakat za mwendambingun watu wawil au watatu wanajichimbia ikulu na kuamua kukopa mihela kimya kimya halafu mzee akitoka barabarani anawaaminisha watu nchi ina mihela mingi na hawakopi.

Ameondoka kaliacha linchi halina kitu na mamirad kibao+miden mikubwa mikubwa...tena nadhan hyo vp ndiye anapaswa tumning'inize coz ndiy alikuwa anashirikiana na mzee kutupiga mchanga machoni. Kibaya sana mama naye akakubal kirahis tu huyo m-kigoma awe vice wake.

Leo wale walioshirikiana na mwendazake ndiy wanataka kumsulubu mama,ashindwe kutekeleza mamirad yale and then watujie na porojo za "Mama amefeli'....hapana,na tuseme hapana wamwache mama afanye kaz..over!
Wakati hayo yanafanyika huyo mama yako muimba taarabu alikuwa wapi katika serikali hii?
Mfike mahali mjifunze kuipenda nchi yenu na sio watu wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom