Ujumbe wa Mungu kupitia Biblia ni simple.
- Mungu alimwumba mwanadamu kwa ukamilifu
- Mwanadamu alitumia uhuru na utashi wake kumuasi Mungu
- Mungu aliandaa taifa ili amlete mwokozi wa mwanadamu
- Yesu alikuja, akafanya kazi ya wokovu
- Imebaki kwa mwanadamu kumwamini na kumpokea Yesu ili apokee wokovu
Sasa Biblia nzima imeelezea namna gani Mungu ametekeleza mpango wake wa wokovu, kupitia vitabu vya manabii, vitabu vya wafalme, vitabu vya hekima kama Mithali na nyimbo kama Zaburi n.k.
Ukisoma Biblia kama mtu mwenye elimu ndogo kabisa unaweza kumjua Mungu, na ukitaka kusoma Biblia kwa undani na kufahamu mambo mengi zaidi pia utamjua Mungu.
Inawezekana yako mambo machache yanayohitaji ufafanuzi hilo sio shida ndo maana kuna watu wanasoma Biblia na Theology mpaka level za PhD kwa lengo la kuwasadia wengine na kuimarisha Imani zao. Lakini hauhitaji Degree ya Biblia au Theology kumjua Mungu kuwa na uhusiano binafsi na yeye.
Unachohitaji ni kuwa na moyo wa kujifunza na unyenyekevu ndivyo utakavyo saidika. Lakini ukiamua kuwa mkaidi hata kama kila kitu kingekuwa as plain as possible bado utamkataa Mungu.