Mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa kwa mbali na nchi ya Tanzania

Basi ww iliekaa nao kwao hongera ila nimeishi nao miaka ya kutosha mfano swala la hali ya hewa na urahisi wa maisha ndiyo ilikuwa nyimbo yao kila siku
Wamarekani ni watu wabishi mpaka wamekimbia kwao ulaya wakaenda kuanzisha makazi Marekani, wamebishana kwenye nchi yao inavyoendeshwa mpaka wamepigana vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Wewe Mtanzania hujakimbia kwenu kwenda kuanzisha nchi nyingine wala kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe bado hujawafikia kwa ubishi.
 
Sawa tumekusikia chawa. lakini tz tuna watu duni waisionna akili Wala maono ya kutumia fursa kuendeleza watu wao

Tuna majambazi ya ccm ambayo yamehodhi rasilimali zetu na hayalipi kodi
 
Sawa mkuu
 
Sawa tumekusikia chawa. lakini tz tuna watu duni waisionna akili Wala maono ya kutumia fursa kuendeleza watu wao

Tuna majambazi ya ccm ambayo yamehodhi rasilimali zetu na hayalipi kodi
Nimeshakuwa chawa tena?kweli bongo si mchezo
 
Marekani umeenda lini mkuu?
 
...Sawa, Yote hayo yanatusaidia Nini ?... [emoji848]
 
Tanzania tuna rais mwanamke baada ya miaka 60 tu ya uhuru. Marekani hawana baada ya zaidi ya miaka 200 ya uhuru. Wanawake wawili, Hilary na Kamala, walijaribu kukaribia wakaangushwa na Donald Trump mara 2!
 
Safi kabisa,mfumo dume umetawala pamoja na kuhubiri usawa wa jinsia
 
Ni sawa tu ni kama Vijana wa Daslam hajui Wilaya ya Liwale ipo Mkoa gani?
Nimeeleza Watanzania wanaizungumzia Marekani kuliko Wamarekani wanavyoizungumzia Tanzania.

Sasa kijana wa Dar asipoijua Liwale iko mkoa gani hapo haijui Marekani?

Kijana wa Dar ni rahisi sana kuto8jua Liwale kuliko kutoijua Marekani.

Unajua kusoma kwa ufahamu na kufuatilia hoja kimantiki?
 
Kuna taifa ambalo hawalizungumzii taifa la Marekani?Marekani ni taifa kubwa!!ila tumewazidi kwenye baadhi ya mambo
 
Kuna taifa ambalo hawalizungumzii taifa la Marekani?Marekani ni taifa kubwa!!ila tumewazidi kwenye baadhi ya mambo
Fuatilia nukuu zako kwangu utaelewa kwamba sikubishana kusema hakuna baadhi ya mambo mmewazidi wamarekani.

Haiwezekani wawapite kila kitu. Wakiwapita ujanja maana yake mmewapita ujinga.

Unabishia hoja ambayo mimi sijaisema.

Mimi nimesema tu Watanzania wanawaongelea Wamarekani kuliko Wamarekani wanavyowaongelea Watanzania.
 
Umesahau, Tanzania imezidi Marekani umaskini na ujinga 👏🏾👏🏾👏🏾
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…