Mambo ambayo ni uongo lakini yanajulikana ni kweli kwa wengi

Mambo ambayo ni uongo lakini yanajulikana ni kweli kwa wengi

Umeanza kukitumia kichwa chako vizuri sasa
 
Ni jukumu la mzazi kujiandalia maisha yake ya uzeeni.
Robert Heriel yupo sahihi.
Nasi Vijana twatakiwa tuanze maandalizi ya uzee wetu bila kutegemea kizazi kijacho.

Usichokielewa kipi?
Kujiandalia maisha yake ni pamoja na ku support watoto wake, mzazi anauza shamba akupeleke chuo baadae unasema hakujipanga! Kuweni na shukurani
 
Anaandika Robert Heriel.

Leo tutajadili ishu ya UONGO dhidi ya UKWELI.
Katika Mantiki/Logic Ipo Hivi;
Ukweli + Ukweli = Ukweli
Ukweli + Uongo = Uongo
Uongo + Uongo = Uongo
Uongo + Uongo = Uongo

Mara nyingi ukweli hujulikana zaidi kwenye matokeo/mwisho wa Jambo au muda.
Ukweli huwaga hauna Pande mbili. Yaani ukweli hautegemei mtazamo au Maoni ya MTU. Ukweli NI ukweli.

Ngoja nikupe mifano ya UKWELI
i. Moto unaunguza - KWELI
Hii hahitaji mjadala, Watu wote na viumbe wote hujua Moto unaunguza. Yaani hata kichaa anajua ukweli huo.

ii. Mapenzi yanaumiza - KWELI
Watu wote Duniani na viumbe vyote Duniani vinajua mapenzi yanaumiza.

Yafuatayo ni mambo ya UONGO AMBAYO watu wengi hujua NI ukweli.

1. Laana na Baraka - UONGO
Unaambiwa ukifanya hivi utalaaniwa au ukifanya hivi utabarikiwa. Huo ni Uongo.
Nitakupa mfano, Kwenye dini unafundishwa Fanya kazi Kwa nguvu na bidii ili ubarikiwe. Lakini unakuja kugundua wapo wanaofanya kazi hawafanikiwi, na wapo wasiofanya kazi wanafanikiwa. Mantiki ya Jambo hili ni Uongo.

Au unaambiwa kuna Laana ya Wazazi, lakini unakuja kuona wapo wanasiowaheshimu wazazi wao lakini wanaishi Kwa furaha na Maisha ya mafanikio, muda huohuo kuna wanaowaheshimu wazazi wao lakini wanateseka. Mwisho unahitimisha ni UONGO hakuna kitu kama hicho.

Ukweli NI huu; kila MTU au kiumbe kimeshaupangiwa nini kitafanya katika Maisha yake. Chochote ukifanyacho kipo katika Akili ya mtunzi aliyekubuni.

2. Kumwabudu Mungu ndio kufanikiwa - UONGO
Wapo wasiomuabudu Mungu na wamefanikiwa.

3. Yesu alikufa ili kutukomboa - UONGO
Dhana ya kusema bila ya Yesu Watu hawawezi kumuona Mungu ni UONGO kwasababu wapo ambao tayari walikuona huyo MUNGU hata Kabla ya Yesu kufa. Kimantiki hiyo stori ni ya uongo Kwa sababu tayari inapande mbili.

4. Kifo kililetwa na dhambi ya kula tunda pale Edeni - UONGO
Kwa sababu wapo viumbe ambao hawakula lile tunda na wanakufa. Wanyama, ndege na samaki, na mimea inakufa licha ya kuwa haikula lile tunda.
Kifo NI mfumo wa Maisha Kwa mwanadamu. Hakina mahusiano na masuala ya maadili.

5. Kutoa zaka unapata thawabu kutoka Kwa Mungu - UONGO
Ni uongo Kwa sababu wapo ambao hawatoi zaka lakini wamefanikiwa. Viongozi wa dini wasiseme Uongo katika hili, muulize kiongozi wako mbona kuna Watu hawatoi zaka na wanamaisha mazuri kuliko wanaotoa?

Kwa kifupi zaka ni malipo unayompa mchungaji au Sheikhe au kiongozi yeyote wa Kiroho mara baada ya kupokea Huduma Fulani. Kama huna Huduma yoyote uipatayo kwenye mambo ya Kiroho hautakiwi kutoa zaka.
Ukienda kanisani au msikitini lazima utoe zaka kwani unaenda kupata Huduma hizo.

Ngoja ninywe maji kisha narudi kupendele.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Upuuzi mwingine wa kufungia mwaka
 
Unaumwa wewe!

Mimi naongea uhalisia wewe unaleta mihemko yako.
Uafrika sio kuishi ndotoni.

Uafrika sio kufanya Watoto watumwa
Uafrika sio kuzaa hovyo Watoto kwa kutegemea Watoto watakuja kunisaidia.
Hizo ni dhana potofu.

Nitaendelea kusisitiza falsafa na dhana hizi kukomboa fikra za waafrika ambazo zimekuwa utumwani Kwa kipindi kirefu.

Kumtunza mzazi sio lazima, mahalo popote pale iwe duniani, mbinguni, mbugani au akhera.

Mimi sio wale wazazi ninaodanganya Watoto na kuwafanya wawe watumwa wa kifikra ATI nitumie hela nikubariki au nitumie Pesa Mimi Baba yako nikubariki.
Siwezi waambia Watoto wangu uongo kama huo.
Nitawaambia wafanye kazi Kwa bidii, Kwa Akili, wawe na uthubutu wa kufanya chochote ili mradi wasimdhuru yeyote. Watapata.

Mimi kama mzazi kazi yangu ni kuwapa Watoto moyo, kuwapa mbinu za kushinda katika Maisha Yao. Na sio kuhangaika kuwatishia na vitu vya uongouongo ili wanipe Pesa.

Hizo Akili hata wanyama wenyewe Hawana.

Mtoto akupe fedha Kwa upendo kama fadhila na sio akupe Pesa Kwa vitisho vya uongo kuwa atalaaniwa Jambo ambalo halipo au akupe fedha kama wajibu.

Nenda serikalini, njoo kwenye Dini, hakuna sheria kama hizo.

Ndio maana kuna mifuko ya kijamii kwaajili ya kuweka Akiba za uzeeni.
Ili ukiwa Mzee usisumbue Watu hasa kwenye ishu za kiuchumi.
Kuwa waafrika haimaanishi muwe wajinga.

Tangu umezaliwa uliwahi kusikia mtu kapelekwa Mahakamani kisa hajamsaidia Baba au Mama yake?
Hakuna huo uhalisia hapa Afrika. Kawadanganye Neandathral wenzako.

Ahsante kwa jibu(haukulazimishwa) kwani kwangu umethibitisha nilichosema, ukumbuke sikujibu hoja yako yeyote(kama zipo) bali dhumuni lako la bandiko.

Aluta Continua.
 
Wewe ni materialism na sio idealism

Jaribu kutomheshimu huyo mzazi kama utafanikiwa endapo amekulaani
 
Dhumuni langu unalijuaje na kulipimaje kama halipo kwenye hoja nilizoweka hapo juu?

Unasema Jambo uhalisia ni Kwa sababu wewe ni Abunuasi, unaishi kwenye ndoto
 
Wewe ni materialism na sio idealism

Jaribu kutomheshimu huyo mzazi kama utafanikiwa endapo amekulaani

Hakuna kitu kama hicho.
Wapo wanaowaheshimu wazazi wao na Maisha Yao ni zaidi ya Laana.
Wapo wasiowaheshimu na wanaishi Maisha mazuri.

Ninachoeleza hapa ni kuwa Jambo lolote likiwa lenye Pande mbili basi jua Hilo ni uongouongo!
Nikakupa mfano, Moto unaunguza, jibu ni ndio. Hakuna MTU duniani atakayesema Moto hauunguzi. Hivyo jibu ni kweli.

Tukija kwenye Laana, wapo wazazi waliwalaani Watoto wao kuwa hawatafanikiwa iwe kielimu au kitaaluma lakini Watoto haohao wamefanikiwa.
Hapo ndipo tunasema Jambo Hilo ni uongo.

Kama baraka zingekuwa za kweli, basi kila mzazi anavyobariki Watoto wake wangebarikiwa na kufanikiwa katika Maisha.

Nenda Kwa wazazi wako waambie wakubarariki au wewe Wabariki Watoto wako vile utakavyo uone kama watabarikiwa.

MTU kujibariki anashindwa sembuse kubariki MTU mwingine (mtoto) huo ni uongo
 
Au unaambiwa kuna Laana ya Wazazi, lakini unakuja kuona wapo wanasiowaheshimu wazazi wao lakini wanaishi Kwa furaha na Maisha ya mafanikio, muda huohuo kuna wanaowaheshimu wazazi wao lakini wanateseka. Mwisho unahitimisha ni UONGO hakuna kitu kama hicho.
Hahahahaha!!! Hapa umeua kabisa mwamba😀😀😀😀
 
ROBERT HERIEL laana ipo babu. Acha kabisa ilo eneo. Usiombe yakukute.

Unaelezeaje waliolaaniwa na Wazazi wao lakini Laana haikamati?
Kwenye Logic tunaitaje hiyo Scenario?
Ndio hoja Ipo hivyo.

Uzi huu upo kisayansi, Logically.
Watu wanajadili Mapokeo walioyakuta kwenye jamii.

Ni sawasawa na Albadiri. Wapo walioombewa Albadiri haijawadhuru, na hakuna ushahidi wa walioombewa Albadiri wakadhurika. Hivyo hapo kimantiki jibu ni uongo.
 
Dhumuni langu unalijuaje na kulipimaje kama halipo kwenye hoja nilizoweka hapo juu?

Unasema Jambo uhalisia ni Kwa sababu wewe ni Abunuasi, unaishi kwenye ndoto
Sawa ulichosema, hakika hakuna hoja zaidi ya Sumu.
...isitoshe, ni wewe uliyeleta "Uhalisia" na sumu zako.... na kama kawaida zenu Neanderthal, na reverse psychology na matusi.
Utaeleweka tuu
 
Kujiandalia maisha yake ni pamoja na ku support watoto wake, mzazi anauza shamba akupeleke chuo baadae unasema hakujipanga! Kuweni na shukurani
Soma hii
FB_IMG_1671913951994.jpg
 
Sawa ulichosema, hakika hakuna hoja zaidi ya Sumu.
...isitoshe, ni wewe uliyeleta "Uhalisia" na sumu zako.... na kama kawaida zenu Neanderthal, na reverse psychology na matusi.
Utaeleweka tuu

Ndio maana nikakuambia jamii bado inaathari Mbaya ya Mapokeo. Wewe ni mmoja wa walioathirika.

Nakupa mfano mwingine,
Maombi yanaponya? Jibu linapande mbili, ndio au hapana. Hivyo kimantiki ni Uongo.
Kwa sababu wapo wanaoombewa hawaponi, na wapo wanaoombewa wanapona.

Hapa tunajadili Logic wewe unaleta mambo ya Mapokeo ya Mababu
 
Ha ha naona sumu uliyonayo hujaishika vizuri. Inakuathiri wewe muathirika Inakuingia sasa. Kanywe uji.
 
Back
Top Bottom