Mambo ambayo ukifanya watu hawatasita kukuua. Bila kujali Sheria zipo au hazipo, Mungu yupo au hayupo


Sasa Fanya wewe Uone ili uelewe Somo lake.
Maswali unayouliza ni kama Mtu anayesema, mbona Fulani anatoka na Wake za watu lakini hapakwi Mafuta au hauawi.

Nilichoandika ni hivi, makosa hayo ukifanya Jua upo kwenye Mchezo wa Kifo.
 
Kufanya dhuluma na na dharau za "kwani utanifanya nini".
 
Kiongozi nimekuelewa.
 
Sasa Fanya wewe Uone ili uelewe Somo lake.
Maswali unayouliza ni kama Mtu anayesema, mbona Fulani anatoka na Wake za watu lakini hapakwi Mafuta au hauawi.

Nilichoandika ni hivi, makosa hayo ukifanya Jua upo kwenye Mchezo wa Kifo.
Hamna!! mtu akitaka kukuuwa atakuuwa tu hata ukimzidi cheo, pesa au umaarufu atakuuwa hata kwa wivu tu. Mbona kina chenge ni mafisadi yameuza nchi hayauwawi ila kuna vijana wasio hata na madhara kama Saanane waliuwawa? Nani hapo ni hatari?

Nachosema hakuna justification yoyote ya kuuwa mtu, msihalalishe haya mambo.
 
Hivi hiyo vita inayoendelea hapo Congo na Huko Ukraine maelfu ya watu wanavyokufa unafikiri ni Jambo gani linapelekea vifo vyao kama sio Masuala ya mipaka ya ardhi?
Wewe ulisema ukiungana na wavamizi utamalizwa, ndio nasema hao Donbass walipiga kura kuunga mkono ijitenge iende Russia mbona huyo zelensky hakwenda kuwauwa au kunyonga kiongozi wao? Wanaokufa ni pande zote sababu ya vita haina macho ila sio kama vile wanaokufa ni waliojitenga tu. In fact viongozi hawajafa wanaokufa ni raia wa kawaida tu
 
Nafikiri Biblia huijui vizuri.

Yale mambo 10 ni muhtasari tuu ambao umefafanuliwa kwenye Biblia nzima, Quran na Sheria za kila Nchi
Hakuna cha muhutasari, Mungu alisema dhambi au yakuachwa ni 10 tu, huo muhutasari nani alikwambia? Nisije kuwa naongea na Mchungaji Zumaradi anayeenda Mbinguni kila siku.

Mnatuwekea limiti ya kuishi sanaa, kila kitu kiwe dhambi tutaishi vipi?
 
Hapa anachoongea mwandishi ni pale unamhitaji mtoto km baba ili umchukue ukae na umlee na watoto wako ulionao kwenye familia yako lakini mama yake akakunyima mtoto mapema aidha kwa sababu ambazo ni za kipumbavu:Kukunyima mtoto kwa hasira ili kukukomoa,kejeli za mama yake kuwa atamlea mwenyewe, mama kutoka familia bora na kuwa kiburi,mama kukunyima mtoto ili amtumie mtoto kukuchuma angali wakati mwingine ameolewa,mama kuwa na mawazo potofu kuwa mwanae atateswa na mama wa kambo,nk.Mimi kwa vigezo hivi ukininyima mtoto husitegemee lolote maishani mwangu,bahati mbaya kuna watoto bado wanaweza kujitambua lkn bado akashindwa kukutambua na kuungana na mama halafu siku umekufa yanajileta na ***** kudai urithi,nahisi nitafufuka siku hiyo.But kuna watoto hujitambua mapema na kujileta mapema kwa baba zao na kuzikataa itikadi za mama zao hao ndo upata ushindi katika hili
 
Andiko lako ni zuri lakini limejaa jazba sana......

Hatukatai kuwa watoto wa aina hiyo huwa mara nyingi wana migogoro sana na hii inatokana na wewe ulivyomalizana na mama yake......

Kwa akili za kike ni kweli huwa wanakuwa rude hasa pale wewe Baba mtoto ukiwa ulimzalisha huku tayari una familia.......

Kufupisha mambo ni kuwa kwa namna yoyote ile ikiwa wewe ulichukua muda wako na kumtongoza mama yake na kumpa mimba na ikithibitishwa kuwa wewe ndio Baba wa mtoto wa mtoto basi mwanao ana haki kama watoto wako wengine......kuepusha yote haya dhibiti nyege zako na utulie na mkeo.....

Huwezi kuyakimbia matokeo ya matendo yako machafu kwa sababu nyepesi kama hizo......uwe umemlea au umegombana na mama yake haki yake kwako haifutiki.....hata ukiandika wosia wa kumdhurumu utapingwa mahakamani na yeye atapatiwa haki yake......

Kwa usalama wako wagawie mapema mali zako watoto unaowapenda angali ukiwa hai lakini kama ni urithi mahakama haingalii ndoa bali ni uhalali wa watoto....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…