Mambo ambayo ukifanya watu hawatasita kukuua. Bila kujali Sheria zipo au hazipo, Mungu yupo au hayupo

Mambo ambayo ukifanya watu hawatasita kukuua. Bila kujali Sheria zipo au hazipo, Mungu yupo au hayupo

Mbona Mbowe hakukuuwawa? Odinga pia alishiriki kumpindua Moi ila hakuuwawa?
Mbona Trump anamhusu Putin na hamna kitu amefanywa? Nadhani ungesema nchi za kiafrika ila huko nje sio kweli. Mbona Prince wa saudia alifanya peace na Israel ila hajauwawa?

Sio kweli, Nyerere alisupport Biafra ili wajitenge na Nigeria ila hakuuwawa. Same to Ali Hassan Joho alitangaza 2018 kuwa Mombasa inajitenga na Kenya na akawa anadai referendum ila hakuuwawa.

Sasa Fanya wewe Uone ili uelewe Somo lake.
Maswali unayouliza ni kama Mtu anayesema, mbona Fulani anatoka na Wake za watu lakini hapakwi Mafuta au hauawi.

Nilichoandika ni hivi, makosa hayo ukifanya Jua upo kwenye Mchezo wa Kifo.
 
NASISITIZA, MAMBO AMBAYO UKIFANYA WATU HAWATASITA KUKUUA. BILA KUJALI SHERIA ZIPO AU HAZIPO, MUNGU YUPO AU HAYUPO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Oooh! Kuua ni ukatili, kuua sio HAKI. Oooh! Kuua ni Kwa nchi zisizoendelea! Ndugu zangu usije ukajidanganya Wala kudanganywa. Wala usije ukajichanganya. Watakuua, utamalizwa.

Kuna mambo ukifanya nakuhakikisha umejiingiza kwenye Hatari kubwa ya kuangamizwa, kuuawa, kupotezwa. Mambo hayo yapo Katika Nyanja zote, kisiasa, kijamii na kiuchumi
Kama Ifuatavyo;

1. KISIASA,
a) Uhaini, kufanya mipango ya kumuua Mfalme au Rais, kuratibu au kushiriki mipango hiyo. Kwa namna yoyote Ile.
Watakuua nakuhakikishia, kama wewe ulivyopanga kumuua au kumpindua mfalme Basi tegemea matokeo makubwa ya Hatari yatakayokurudia.

b) Kuipasua nchi.
Mfano nchi ya Tanzania, ufanye Njama igawnyike Mapande Mapande kama vile Sudan Kusini na Sudan Kaskazini. Watakuua nakuhakikishia. Labda uwe na bahati Sana uchoropoke. Au uwe umewazidi mipango, mikakati na mbinu.

c) Kuungana na Adui wa Nchi.
Mfano, Korea Kaskazini na Kusini. Wewe ni Mkorea Kusini lakini unaunga Mkono Korea Kaskazini au kinyume chake. Watakuua mchana kweupe.

d) kusogeza Mpaka wa Nchi.
Mfano, Malawi wanaleta chokochoko wanataka labda ziwa na baadhi ya maeneo. Au vile Idi Amin anataka kuchukua baadhi ya maeneo ya Kagera alafu wewe unajifanya unaungana na Amini au Malawi ili Tanzania ichukuliwe maeneo yake. Watakuua nakuhakikishia.

e) Ugaidi
Matendo yoyote ya Kigaidi hasa ukiwa frontline na kiongozi. Utauawa Bila huruma.

f) Uasi Jeshini.
Wewe ni Mwanajeshi, labda ukaona Jambo Fulani linaenda ndivyo sivyo. Ukaamua kushawishi wenzako wenye mtazamo kama wako. Kaa ukijua Mchezo unaoenda kuufanya ni vita ya Kifo na uhai. Kuuawa ni njenje.

2. KIJAMII
a) Kulala na Mke au Mume wa Mtu.
Kuna wanasema, oooh! Huo ni ushamba, hooo! Kujichukulia Sheria mkononi, oooh! Sio uungwana.
My friend, huo uungwana ungeanza nao wewe hapo. Sio uchukue Wake/Waume za watu alafu uwatake wawe waungwana, watakuua nakuhakikishia. Utauawa, au kufirwa, au kufanyiwa matendo yanayolingana na Jambo ulilofanya.

MKE au Mume wa Mtu thamani yake ni kubwa kwenye maisha ya Mtu. Huwezi ukaenda kuchukua Mke au Mume wa Mtu alafu ukaleta Maneno yako ya kanisani au misikitini huko. Watakuua nakuambia.

Oooh! Haki za binadamu. Hizo Haki za binadamu zitumie kuheshimi Mali na vitu vya watu wengine. Kama Haki hizo hukuzitumia Jua hakuna atakayezikumbuka kuzitumia. Utauawa.

Labda ukutane na watu wasio na nguvu ya kufanya hayo. Lakini kama Mtu ananguvu yoyote Ile. Tegemea Kuuawa kikatili.

b) Urithi na wizi wa Mali.
Urithi ni Haki ya asili ya Mtu.
Unapochukua Haki hiyo tegemea Kuuawa.
Historia inajieleza, mauaji Mengi yamechangiwa na ishu ya Urithi na wizi wa Mali.

Wewe unajijua huna Haki ya kuchukua Mali Fulani, why utake kuichukua Mali hiyo kama sio dharau, kiburi na kujifanya mwamba. Hakika utauawa.

Mfano,
Umeolewa, huna Kazi ya maana, Mumeo ni tajiri wa kutosha, uwiano wenu wa mchango wa Mali kwako ni 20 Mume 80 yaani 2:8 au 1:4.
Imetokea mmegombana, alafu ukadai Talaka, alafu kwenye Mali unataka upewe nusu kwa nusu. Hakika yake utauawa. Hiyo sio Haki yako.
Inakuwa Haki yako ukiwa kwenye Ndoa lakini mara utakapoondoka haiwi yako tena Bali kila mtu anachukua kilichochake.
Ni kama kampuni. Kila mtu achukue Hisa zake.
Sasa kitendo cha wewe kutaka kuchukua Hisa ambazo sio zake ni kujitafutia matatizo makubwa ikiwezekana kuuawa.

Ndio maana Kila siku Mimi Mtibeli nawaambia wanawake na ninyi mfanye Kazi, muwe na Hisa zenu.
Sio mzae tuu au mjifiche kwenye kichaka cha kufanya Kazi za nyumbani sijui kulea.
Ilhali siku hizi matajiri na watu wengi Wana watafutia wadada WA Kazi na Kazi karibia zote hapo nyumbani zinafanywa na Dada wa Kazi.

Utauawa. Na Sisi Watibeli hatutashangaa kwa sababu Dawa ya watu kama ninyi ni Kifo hasa mkiwa mmedhamiria.

Mfano, 2
Mtoto wa nje hupaswi kudai HAKI ya Urithi kama hukulelewa kwenye familia ya Baba yako. Lilikuwa jukumu la Mama yako kupeleka kwa Baba yako ukaishi huko.
Kwa Sisi Watibeli tunajua Mtoto ambaye hujamlea huyo sio mtoto wako.
Mtoto wako ni Yule uliyemlea.

Mtoto atarithi kwa mama au upande wa Mamaake ikiwa alikulia huko. Hiyo ndio HAKI.
Achana na Maneno ya kilaghai na uongouongo na unafikinafiki yanayotokewa na HAKI zijui za binadamu. Haipo hivyo.

Sehemu ambayo hujakulia au kulelewa wewe utabaki kuwa mgeni tuu. Hata wewe mwenyewe ukifika nafsi yako itajiona hivyo.

Ndio maana Mimi Mtibeli kila wakati nawaambia, hasa wanawake ikiwa umeamua kukaa na mtoto Moja kwa Moja basi Hakikisha unatambua vitu muhimu kama hivyo.
Ukikaa na mtoto Hakikisha unamtafutia na Urithi kwa sababu huyo ni mtoto wako.
Sio ukae naye wewe alafu Biological father amtafutie Urithi ilhali hakai naye. Huyo sio mtoto wake kimazingira ila ni mtoto wake kibaolojia.

Lazima umuandalie na HAKI za Baraka zake kama mtoto.

Baba hawezi kumbariki mtoto ambaye hajaishi naye hizo Baraka zikashika. Tumia Akili ndogo kujua Hilo.
Baraka za Baba lazima ziwe na connection ya kimwili, kiroho na kimazingira.
Lazima Baba ajue Tabia na makuzi ya Mtoto.

Na umri sasa watoto kujuana na Baba ni Kati ya Miaka 0-15.

Baraka pia ni sehemu ya Urithi ambao unapiganiwa kufa kupona hasa na watoto wenye AKILI wenye mipango ya Muda mrefu na wanaotaka vizazi vyao viwe na Nguvu.

c) Kuiba mashamba au viwanja vya watu.
Utauawa wewe. Ugomvi wa ardhi umeua wengi Sana.

Acha niende Kanisani Kwanza, alafu tutaendelea.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kiongozi nimekuelewa.
 
Sasa Fanya wewe Uone ili uelewe Somo lake.
Maswali unayouliza ni kama Mtu anayesema, mbona Fulani anatoka na Wake za watu lakini hapakwi Mafuta au hauawi.

Nilichoandika ni hivi, makosa hayo ukifanya Jua upo kwenye Mchezo wa Kifo.
Hamna!! mtu akitaka kukuuwa atakuuwa tu hata ukimzidi cheo, pesa au umaarufu atakuuwa hata kwa wivu tu. Mbona kina chenge ni mafisadi yameuza nchi hayauwawi ila kuna vijana wasio hata na madhara kama Saanane waliuwawa? Nani hapo ni hatari?

Nachosema hakuna justification yoyote ya kuuwa mtu, msihalalishe haya mambo.
 
Hivi hiyo vita inayoendelea hapo Congo na Huko Ukraine maelfu ya watu wanavyokufa unafikiri ni Jambo gani linapelekea vifo vyao kama sio Masuala ya mipaka ya ardhi?
Wewe ulisema ukiungana na wavamizi utamalizwa, ndio nasema hao Donbass walipiga kura kuunga mkono ijitenge iende Russia mbona huyo zelensky hakwenda kuwauwa au kunyonga kiongozi wao? Wanaokufa ni pande zote sababu ya vita haina macho ila sio kama vile wanaokufa ni waliojitenga tu. In fact viongozi hawajafa wanaokufa ni raia wa kawaida tu
 
Nafikiri Biblia huijui vizuri.

Yale mambo 10 ni muhtasari tuu ambao umefafanuliwa kwenye Biblia nzima, Quran na Sheria za kila Nchi
Hakuna cha muhutasari, Mungu alisema dhambi au yakuachwa ni 10 tu, huo muhutasari nani alikwambia? Nisije kuwa naongea na Mchungaji Zumaradi anayeenda Mbinguni kila siku.

Mnatuwekea limiti ya kuishi sanaa, kila kitu kiwe dhambi tutaishi vipi?
 
Hapo kwa mtoto nadhani hauko sahihi.....kama uliweka mimba unapaswa kuwajibika kwa tendo lako....haiwezekani umtongoze binti....mpange miadi mkutane kimwili na umuweke mimba alafu linapokuja suala la malezi unakimbia ukitegemea utawajbika.......kama ulivyotoa jasho wakati unapiga bao lenye kutunga mimba na ndivyo mtoto huyo anastahili jasho lako......

Kama ingekuwa Una heshimu muunganiko wako na mkeo usingetongoza nje na kufanya uzinzi......

Huyo mtoto ikithibitishwa kuwa ni mbegu yako basi anastahili jasho lako na kama huna hiyari basi mahakama itakulazimisha kufanya hivyo......
Hapa anachoongea mwandishi ni pale unamhitaji mtoto km baba ili umchukue ukae na umlee na watoto wako ulionao kwenye familia yako lakini mama yake akakunyima mtoto mapema aidha kwa sababu ambazo ni za kipumbavu:Kukunyima mtoto kwa hasira ili kukukomoa,kejeli za mama yake kuwa atamlea mwenyewe, mama kutoka familia bora na kuwa kiburi,mama kukunyima mtoto ili amtumie mtoto kukuchuma angali wakati mwingine ameolewa,mama kuwa na mawazo potofu kuwa mwanae atateswa na mama wa kambo,nk.Mimi kwa vigezo hivi ukininyima mtoto husitegemee lolote maishani mwangu,bahati mbaya kuna watoto bado wanaweza kujitambua lkn bado akashindwa kukutambua na kuungana na mama halafu siku umekufa yanajileta na ***** kudai urithi,nahisi nitafufuka siku hiyo.But kuna watoto hujitambua mapema na kujileta mapema kwa baba zao na kuzikataa itikadi za mama zao hao ndo upata ushindi katika hili
 
Hapa anachoongea mwandishi ni pale unamhitaji mtoto km baba ili umchukue ukae na umlee na watoto wako ulionao kwenye familia yako lakini mama yake akakunyima mtoto mapema aidha kwa sababu ambazo ni za kipumbavu:Kukunyima mtoto kwa hasira ili kukukomoa,kejeli za mama yake kuwa atamlea mwenyewe, mama kutoka familia bora na kuwa kiburi,mama kukunyima mtoto ili amtumie mtoto kukuchuma angali wakati mwingine ameolewa,mama kuwa na mawazo potofu kuwa mwanae atateswa na mama wa kambo,nk.Mimi kwa vigezo hivi ukininyima mtoto husitegemee lolote maishani mwangu,bahati mbaya kuna watoto bado wanaweza kujitambua lkn bado akashindwa kukutambua na kuungana na mama halafu siku umekufa yanajileta na ***** kudai urithi,nahisi nitafufuka siku hiyo.But kuna watoto hujitambua mapema na kujileta mapema kwa baba zao na kuzikataa itikadi za mama zao hao ndo upata ushindi katika hili
Andiko lako ni zuri lakini limejaa jazba sana......

Hatukatai kuwa watoto wa aina hiyo huwa mara nyingi wana migogoro sana na hii inatokana na wewe ulivyomalizana na mama yake......

Kwa akili za kike ni kweli huwa wanakuwa rude hasa pale wewe Baba mtoto ukiwa ulimzalisha huku tayari una familia.......

Kufupisha mambo ni kuwa kwa namna yoyote ile ikiwa wewe ulichukua muda wako na kumtongoza mama yake na kumpa mimba na ikithibitishwa kuwa wewe ndio Baba wa mtoto wa mtoto basi mwanao ana haki kama watoto wako wengine......kuepusha yote haya dhibiti nyege zako na utulie na mkeo.....

Huwezi kuyakimbia matokeo ya matendo yako machafu kwa sababu nyepesi kama hizo......uwe umemlea au umegombana na mama yake haki yake kwako haifutiki.....hata ukiandika wosia wa kumdhurumu utapingwa mahakamani na yeye atapatiwa haki yake......

Kwa usalama wako wagawie mapema mali zako watoto unaowapenda angali ukiwa hai lakini kama ni urithi mahakama haingalii ndoa bali ni uhalali wa watoto....
 
Back
Top Bottom