Mambo kumi yaliyobebwa ndani ya kikao Kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Tundu Antipas Lissu, Brussels Ubeligiji

Mambo kumi yaliyobebwa ndani ya kikao Kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Tundu Antipas Lissu, Brussels Ubeligiji

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
1. Mhe. Rais ameonyesha wanadamu wenye damu ya siasa Kwamba hakuna Nchi itapiga hatua ikiwa vipande vipande. Tanzania ilimkosea Tundu Lisu Kwa Yale yaliyomkuta, Tanzania ilimkosea Tundu Lisu kumfuta Ubunge na Mwisho Tanzania ilimkosea Tundu Kwa kuacha kuchukua hatua ikiwemo kuchunguza shambulio dhidi yake.

2. Serikali haiwezi kuomba mwananchi wake MSAMAHA ila viongozi waliopewa dhamana wanaoweza wakaingiwa na utu wakaomba Msamaha bila hata kutamka wanaomba Msamaha

3. Tundu Lisu ana roho ya binadamu, anaweza kufanya analysis akabaini pamoja na kuponea kifo Lakini Tanzania Kwanza.

4. Siyo wanasiasa wote walikubaliana na ukatili aliofanyiwa TL ila walikosa nafasi ya kutoka na kukemea. Baadhi wangelazimika kujiuzulu.

5. Chadema ina viongozi na itaendelea kuwa na viongozi

6. Mazungumzo haya yanakwenda kumtoa Mwenyekiti ndani kama siyo ijumaa basi baada ya taratibu za urasimu wa mahakama kutimia.

7. Jaji alikataa Kibatala kuwasilisha oral submission, alishaelekezwa bila kuonekana Kwa mwanga wa Kesi kufungwa Lisu asingeonana na mama

8. Yapo mazingira ya nope nikupe, usipokubali kumwachia Mwenyekiti tutabaki huku ukimbizini. Mama hapendi utawala wake ufananishwe Kwa ndani na mwenda zake. Anawaza kutengeneza Urais wake, yeye ni Rais na afundishwi Urais

9. Wale binadamu wote walioshiriki kumdhuru Lisu adhabu inawaka Kwao, kama siyo Duniani basi Mbinguni. Akiwemo aliyemfuta Ubunge

10. Mama kaupiga mwingi ila Tundulisu kaungana kuongeza sauti.

Mwisho, Tanzania ni kubwa KULIKO CCM na Chadema. Leo Taifa linaamani baada ya wazazi kuelewana. Pamoja na umaskini ila tunapaswa kuungana sisi kwanza kabla ya kuomba misaada nje
 
Sasa siasa itakuwa ni kama ile ya majirani- Odinga na kenyata...
 
Mbona Lisu anatetea ndoa za jinsia moja na bado ana wafuasi kama wewe??
Lissu hajawahi tete ndoa za jinsia moja,na kama dini yako inaruhusu muoane wanaume kwa wanaume basi olewa tu


Ila hilo jambazi acha avune alichopanda,mungu wake mtetezi alishatangulia mbele za haki sasa acha apambane na hali yake
 
Nice move.

Hatua nzuri ya kuanza kuliunganisha taifa, vyema viongozi wakawaachia watanzania haki yao ya kuchagua wawakilishi wao wawatakao na viongozi wajifunze kuheshimu maamuzi ya watanzania.

Yeyote anayehusika kudhulumu haki hii muhimu ya watanzania aonekane adui namba moja kwa mustakabali wa kukuza umoja na ushirikiano wetu, wala asionekane jasiri atakaepongezwa kwa kupewa uwaziri kama asante.
 
Lissu hajawahi tete ndoa za jinsia moja,na kama dini yako inaruhusu muoane wanaume kwa wanaume basi olewa tu


Ila hilo jambazi acha avune alichopanda,mungu wake mtetezi alishatangulia mbele za haki sasa acha apambane na hali yake
Itakua umemsahau Robert Amsterdam wewe ama la wewe sio memba wa Chadema.

Wenzako wote wanafahamu kwamba ndoa za jinsia moja ndio agenda kuu ya uchaguzi kwa chadema in 2020.
 
Sabaya aachiwe.
sabaya ameenda kumuibia mtu kwa bunduki mbona unakuwa mgumu kuelewa! kesi yake huwa ni miaka 30 kwenda mbele!

angefanyia ndani ya HAI ingekuwa rahisi kuficha ila kaenda kuiba Arusha na CAMERA zimemuonyesha

yeye mwenyewe alikuwa analia msibani kama kapoteza baba alijua hili linakuja! hata angekimbilia ubalozi wangemuacha nje wenyewe wampitie tu kwa ukatili wake yeye kama yeye!
 
Back
Top Bottom