Ukiwaingilia wazungu ulaji wao hutoboi. Nasema hutoboi! Wamezoea kujichotea madhahabu, gesi na madini mengine karibu na bure halafu wewe utoke huko ulikotoka uje uwanyang'anye? Who are you?
We jiulize. Baada tu ya kufariki, habari za ikulu na siri za serikali zikaacha kuvuja. Wanaharakati wote (Kimambi, Maria, Ngurumo, Chahali, Kigogo, Fatuma, Zitto, TL...) ghafla wakawa kimya. Hata wapinzani nao kimyaa eti maafikiano wakati mpaka leo hawawezi kufanya mikutano na kunadi sera zao. Hata Amsterdam aliyekuwa anafungua kesi kila leo ili mteja wake aruhusiwe kurudi nchini kimyaa japo mteja wake bado hajarudi...
Waafrika (isomeke watu weusi duniani kote) hatujui tunachokitaka acha tu wazungu waendelee kutuibia na kututawala mpaka Yesu atakaporudi. Kila mtu anawaza kuiba na kujinufaisha yeye, familia yake na marafiki. There is no hope for Africans labda ifike mahali tubadili kabisa falsafa na mitazamo yetu. Na hii itachukua vizazi kadhaa.
JPM alikuwa kiongozi sahihi kuhusu ubabe wa kiuchumi na angekuwa savy na kuacha tu kutumia maguvu kwa waliomkosoa angeifikisha nchi hii pazuri sana. Hakukuwa na haja ya kuvunja haki za binadamu na kuchafua demokrasia namna ile. Angekuwa savy kama mama pengine angekuwa hai na tungekuwa tunasonga mbele.
He sabotaged himself na kutia doa legacy yake mwenyewe...na matokeo yake wenye dunia yao wakatumia kisingizio cha uvunjaji wa haki za binadamu na ukosefu wa demokrasia (via Korona) kumwondoa.