Mambo makubwa manne niliyojifunza baada kifo cha Hayati Magufuli

Bina damu wote........./na Africa ni moja!! hukusoma nini?? hii mipaka ni ya wazungu, urundi/rwanda ni mikoa ya Tanganyika tu ile!!.....hivi wajaluo/wakurya /Masai/wachgga wako na jamaa zao nchi mbili tofauti!

akienda huku ni sawa na huku!! Makonde/wahaya wako nchi mbili tofauti mipaka imepita kati yao! leo utasemaje ivo?? Mpaka wetu ungenyooka tokea Tanga, Nyerere angekuwa m- kenya.
 
Hueleweki una maanisha nini.. Jiwe alikuwa mjinga kama walivyo wajinga wengine waliopo Africa
 
Hauko sahihi.. kwa hiyo wewe ulifurahi dhuluma katika chaguzi na dhukuma dhidi ya uhai wa watu? Au kwa hiyo wazungu walimsingizia? Rot in hell jiwe
 
Hii Nchi ipo ipo tu ili Mradi siku zinaenda
 
Hahahah mnafiki sana huyo ndo maana mama Samia kaamua kumrudisha maana la manyani sasa!
Umesahau msomaji wa vifo mwandosya yule bwana kipindi magufuli yupo hai kila siku alikua anatangaza vifo. Ila jpm alipokufa ndugu zake nao wakaacha kufa
 
JPM alichukiwa na mnafiki Tundu Lisu na Watanzania.

Lisu na Lema ni walelewa Ubelgiji siyo watanzania.
Wewe ni mpuuzi mkubwa. Kama leo Palamagamba anakiri , kuwa waliwadanganya waTanganyika. Bado hujielewi kuhusu kina Lissu ?!
 
Kwahiyo wanaoweza kudindia maslahi ya nchi ni nani ?!
Hawa ccm hawa kweli !!
 
Hauko sahihi.. kwa hiyo wewe ulifurahi dhuluma katika chaguzi na dhukuma dhidi ya uhai wa watu? Au kwa hiyo wazungu walimsingizia? Rot in hell jiwe
Hujanielewa kamanda labda sababu ya mihemko na jazba. Point yangu ni pana kidogo na inaangazia jinsi mfumo wa kibeberu unavyofanya kazi hasa kuelekea nchi zenye raslimali wanazozitaka.

MO (Modus Operandi) yao ni kwamba ukiwapa raslimali wanazozitaka hata ukanyage haki za binadamu na demokrasia namna gani wala hawakusumbui. Angalia kwa mfano Saudi Arabia. Kuna demokrasia gani kule? Haki za binadamu zinaheshimiwa huko? Mbona Saudia ndiye mshirika mkubwa wa Marekani na analindwa sana? Israeli je?

Ukiwauliza akina Saddam Hussein na hata Muamar Gaddafi watakwambia kuwa kilichofanya wauwawe wala siyo udikteta wao bali ni kujifanya vidume kulinda raslimali zao. Demokrasia na haki za binadamu ni kivuli tu ambacho hutumiwa na hawa jamaa wakiona kuwa huwapi wanachokitaka. Na sasa wamejumuisha na haki za mashoga humo. Ukijifanya tu huungi mkono ajenda yao hiyo unasingiziwa kuwa unavunja haki za binadamu na kama unawabania raslimali wanazozitaka hii ni sababu tosha ya kukuletea "demokrasia" yao.

Na hata ukiwapa wanachokitaka inabidi uwe macho uendane na matakwa yao. Wakiona umeachwa nyuma na wakati au wakiona wanaweza kuzipata raslimali zako bila wewe basi wanakuweka pembeni wanaweka mtu wao ambaye ni boya zaidi yako. Kama unabisha nenda kamuulize Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga aliyeishia kuzikwa na watu sita huko Morocco tena katika kaburi la kawaida tu.

Mimi naamini kuwa kama Rais Magufuli asingekomaa sana na kutumia maguvu tu dhidi ya vita vyake vya uchumi na akina ACACIA sijui na akina nani leo hii angekuwepo. Alikuwa anaweka precedent mbaya sana kwao. Imagine viongozi wote wa Afrika wangevuvumka na kutumia maguvu kuhusu haki za raslimali zao mabeberu wangeishije? JPM had to go whether alikuwa dikteta ama la!

Na hakuna binadamu a(li/na/ataka)yefurahia dhuluma dhidi ya uhai wa mtu au wizi wa kura na hili nimeligusia hapo juu kuhusu legacy yake.

Labda sasa utakuwa umenielewa muktadha na wigo mpana wa hoja yangu.
 
Nimekuelewa. Lakini lawama zaidi nizitupe kwa uongozi wa awamu ya 3 & 4. Baada ya kuingia mikataba ya kishenzi na so called wawekezaji (wazungu), dhidi ya nchi. Ni kama rasilimali hizi zilikuwa mzigo kwa nchi.

Kwa hiyo kiongozi yeyote anayefuata lazima mikataba ile imtese. Ubaya wa Jiwe naye kwa kutaka , sifa za ki mungumutu akakosea kuwakandamiza wakosoji wake. Na wengine kuwahonga nyadhifa na vyeo .
Ajabu sote tunazeeka na kufa. Where are they now ?!.

Yeyote anaeomba kuwaongoza watu , awe mwerevu kama ndege au hata nyoka. Ukileta sifa na mabavu utavuna nothing.
 
Hauko sahihi.. kwa hiyo wewe ulifurahi dhuluma katika chaguzi na dhukuma dhidi ya uhai wa watu? Au kwa hiyo wazungu walimsingizia? Rot in hell jiwe
demokrasia africa ndio chanzo kikubwa cha Vurugu
 
Imagine gesi ya Mtwara tuliambiwa kuwa sasa tutaweza kujitegemea katika nishati hiyo leo hii ukiuliza hiyo gesi iko wapi na inamnufaisha nani hakuna anayejua. Si ajabu wajanja wachache wameshajichotea mabilioni yao wamejenga mahekalu yao huko Masaki na Mbezi wanasukuma maRR mapya mabarabarani na watoto wao wamo kwenye system wakati Mmakonde mwenye gesi huko Ntwara anaendelea kupikia kuni.

Kuwa mwerevu kama ndege au hata nyoka tu haitoshi. Inabidi pia uwe mzalendo. JK alikuwa mwerevu na mjanja sana lakini alitufikisha wapi na mamikataba haya mabovu ya madini na gesi? Ukitaka kula nawe kubali uliwe anakupa uhuru wa kujieleza hata kumuita dhaifu na Vasco da Gama lakini huku anafanya yake.

Kasafari ketu bado karefu sana...kama tumo safarini!
 
Kwenye hili la Gas & mafuta 2015 July, niliwadharau sana wabunge na bunge lililokuwa linamaliza muda wake, kuelekea uchaguzi mkuu 2015 Oct. Serikali iliyokuwa imebakiza miezi miwili tu kuondoka. Iliwalazimisha wabunge, kupitisha muswaada wa Gas & mafuta kwa hati ya dharura, chini ya madam spika usiku wa manane. Hata wapinzani walipokataa na kuonya, juu ya dharura ile na kususa hawakujali.

Na alipoingia Rais mpya November 2015 akawambia waTanganyika Gas & mafuta si yao tena. Bali wawekezaji. Tanganyika kama tumerogwa na ujinga vile !!

Tatizo la nchi hii iko Kwenye cheo namba moja. Cheo hicho kimepewa utukufu wa kimungu mungu hivi. Inabidi kila mtu kujikomba ili kutafuta uteuzi . Nawakumbuka sana wa Kenya. Huwa hawaabudu sana matakwa ya Rais anatakaJe
 

Spot on!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…