EPISODE 12: Wacha kudharau watu kwa muonekano wao, heshimu kila mtu maana huwezi jua
Hapa naomba nitilie mkazo kwamba kama ulikuwa na hiyo tabia please stop despising people based on their appearance at once and for all. Respect everyone because you never know. I emphasize the importance of treating everyone with respect and avoiding judgment based solely on outward appearances.
Point ya msingi hapa ni kwamba, one should not underestimate or look down upon others based on how they look, as appearances can be deceiving, and you may not fully understand someone's worth or capabilities without getting to know them. The call for respect underscores the idea that showing kindness and consideration to everyone, regardless of their appearance, is a more just and equitable approach. Unaweza kutumia google translator kupata maana kwa kugha ya kwenu hata Kingoni.
Iko hivi, maisha ya hapo ofsini kwa walemavu yaliendelea kama kawaida as time ilivosonga na mimi nikaendelea kupata uzoefu. Aisee nilikuwa deep sana kwenye issues za disability pamoja na mikakati mbali mbali ambayo ipo kisheria, kisera na kiprogramu ambayo ipo katika utekekelezwaji ili kutetea haki za watu wenye ulemavu. Niliongeza uzoefu mkubwa sana kwenye CV hususani mwasala ya disability inclusion into developmental programs. Nimeenda sana bungeni kufanya lobbying and advocacy sessions na kamati mbalimbali za kudumu za bunge na kuwapa madini wabunge mambo gani ya kwenda kuongea bungeni yakuwezesha watu wenye ulemavu. Hapa niwamegee siri moja, michango mingi ya wabunge wakati wa vikao vya bunge mara nyingi inakuwa ni madini wanayopewa na wadau mbali mbali husussani hizi NGOs kwenye sekta husika. Kama wiki hiyo yatajadiliwa matahalani maswala ya ukatili wa kijinsia basi NGOs zinazodili na maswala ya kijinsia wataandaa vikao na wabunge na kuwapa madini ya nini sheria, sera na mikakati ya kimataifa inataka ili kumlinda mtoto au mwanamke dhidi ya ukatili wa kijinsia. Hivyo hivyo kwenye mijadala ya maswala ya uchumi, usafirishaji, nishati nk. So hata sisi tulitumia fursa hiyo vizuri fursa, na waheshimiwa wabunge hawana baya mkikaa nao na kuwaelimisha vizuri basi wanaibeba ajenda yenu vizuri tuu, ila angalizo isiwe tuu hoja ambazo zinamwelekeo wa kukiaibisha chama watakukataeni mcha kweupe, hahahaa.
Kwakweli namshukuru Mungu niliiva sana kwenye maswala ya disability inclusion na mpaka leo nina uzoefu mkubwa sana whent it comes to disability inclusion and empowerment. Nimesema hapo juu kwamba tuwache kudharau watu kisa nafasi zetu au mwonekano wa mtu maana huwezi kujua huyo mtu au watu tunaowadharau watatufaa vipi. Najua hii sio hoja ngeni kwenu na mmeshaisikia mara nyingi sana. Hapa nitakupeni uzoefu wangu kwa mfano hai kabisa.
Pale kwa walemavu nilimkuta sisat duu mmoja hivi ameajiriwa kwenye nafasi ya maswala ya M&E. Alikuwa ni professional kweli kweli kwenye M&E. Sasa kwenye kuhangaika hangaika na ajira akajikuta ameajiriwa pale. Kiukweli yule dada sijui niseme alikuwa na nyodo au ni dharau au ni kujiskia sana, maana sijui hata mimuweke kundi gani. Ni dizaini ya vile visista duu vya kuvaaga mawani za macho si mnajuaga vijitabia vyao (sio wote jamani ila ni most of them). Any way tumuite tu sista duu.
Basi bhana, sista duu wetu yule kiukweli hakuwa mtu wa kuchangamana sana na watu alikuwa very selective, na mara kwa mara alikuwa anasema pale ofisini yeye hapakuwa sehemu yake target zake ni kufanya kazi na internationa NGOs yaani yeye alijiona ni wakimataifa zaidi. Haikuwa kitu kibaya kutamanai kufanya kazi na international organizations lakini alikuwa anabeza sana ile ofisi as if yeye hakuwa anafanya kazi. Kiukweli yule dada alikuwa mzuri sana kwenye maswala ya M&E nampa respect kwa hilo hata mimi alibrash vitu sana ambavyo niliviapply katika kazi zangu. Sista duu I still salute you kwa hilo, ulinifaa sanaaa.
Basi sista duu ilikuwa asione kazi kwenye international NGO anaomba na alikuwa ananyenyekea sana wageni kutoka kwenye international NGOs wanaokuja pale ofisini. Kule hakukuwa kujichanganya bali ilikuwa ni kujishobosha, any way kila mtu ana mbinu zake hata mimi nilishawahi kulamba viatu vya Dr KJ kama mnakumbuka ili mradi tuu kupata ninachotaka. Na hata hapa still bado nawalamba watu miguu wakivutiwa na CV yangu wanipe connection ahahahaa. Unashangaa nini unaambiwa hata viongozi wengi wa Kiafrika wanalamba viatu vya wakubwa wa magharibi ili waendelee kupata misaada na wengine kusalia madarakani – sembuse mimi na sista duu? Habari ndio hiyo.
Kama nilivosema pale ofsini kulikuwa na wageni wa aina tofauti tofauti sana wanaokuja. Kwa kuwa tunadili na watu wenye ulemavu basi ilikuwa ni kawaida watu wenye ulemavu kuja pale wengine kuomba misaada, wengine kutafuta kazi lakini pia wafadhili wengi sana au mashirika ya kimataifa walikuwa wanakija pale kuangalia namna ya kufanya kazi na sisi. Na hao wafadhili na mashirika ya kimataifa ndio ilikuwa target ya sista duu. Na vile alikuwa na kingereza kilichonyooka basi aliwaentertain vizuri sana ilia pate connection.
Sasa nakumbuka wakati Fulani wakati nina miaka kama mitatu pale ofsini ilikuwa ni kipindi cha mvua. Siku hiyo ofsini tulikuwa mimi na sista du utu ofsini kwa sababu kuna safari tulkikuwa tunaandaa ili tusafiri. Gafla akaingia ofsini jamaa mmoja kwa mwonekano tuu alikuwa yupo kama rafu rafu kimtindo, alikuwa amevaa pensi yake halafu amelowana chepechepe. Sasa ile anaingia pale reception hakuna mtu akaanza kuita sista duu akatoka. Sijui kaongea naye nini mara karudi akaniambia nitoke nikamsaidie kuna mtu anamletea ubishi hataki kuondoka.
Mimi nikatoka nikiwa na tahadhari zote nikijua labda ni kibaka na kweli kwa muonekano tuu yule jamaa uanaweza ukamuitia ukibaka kwanza alikuwa na dreads hizi fupi ila nilipozichunguza nikagundua zina matunzo hizi ni vile tuu zimelowa na mvua. Basi nikamsalimia pale jamaa akasema anataka kuongea na uongozi ila yule sista duu hampi ushirikiano wa kutosha. Nikamsikiliza pale jamaa akasema hana muda sana ni muhimu aongee na uongozi kama vipi tumpe namba za simu ya mkuu wetu pale.
Kiukweli jamaa ilikuwa ngumu sana kumwelewa, sista duu akawa analazimisha jamaa aondoke. Ila mimi kiubinadamu tuu nikamwambia sistaduu hebu mwache jamaa asubiri basi hata mvua ikate maana ilikuwa inanyesha balaa. Sista duu akasema kama utakaa naye hapo reception sawa maana hamwamini mwani kumuacha mwenyewe. Anaenda kuendelea na kazi zake ofsini kwake. Basi mimi nikaenda kuchukua laptop yangu nikawa nimekaa na yule jamaa pale reception huku na endelea na shughuli zangu na huku numdodosa mdogo mdogo. Nikampa na kikombe cha gahawa pale ili walau mwili upate joto.
Sasa yule jamaa alikuja na dereva wake ila alikuwa amemwacha mbali kidogo maana walipotea potea sana kwenye kuitafuta ile ofisi ilipo. Yule jamaa alivokuja pale simu na kila kitu chake alikuwa ameacha kwenye gari hivyo akaniomba amfate dereva wake ili kama anishirikishe kilichomleta pale. Basi akaenda baada ya muda mfupi nikaona m-prado unapaki pale nje jamaa akashuka na begi lake la laptop. Then akanaimbia kama mimi mwenyeji pale na nipo kitengo gani. Nikamwambia, basi akaniambia kwakuwa menejiment haipo basi atanishirikisha mimi kilichomleta na majibu yanatakiwa ndani ya wiki moja so mimi nilitakiwa niijulishe menejiment proposal yake. Nikamwambia basi ngoja nimuite na yule sista duu jamaa akagoma kabisa akasema kama siwezi kufanya naye mimi kikao basi wacha aende.
Nikamwambia basi tuendelee. Jamaa akawasha kompyuta yake na akaanza kunipitisha kwenye program ambayo wanataka kufanya na sisi pale ofisini ambayo itawanufaisha watu wenye ulemavu. Asee yule jamaa alikuwa na anawakilisha shirika moja la ulaya ambao walikuwa wanajishughulisha na maswala ya afya sasa yeye alikuwa amehamishiwa Kenya ambako ndio makao makuu ya East Africa ya hilo shirika. Na ni yeye ndio alieandika hiyo proposal ya kufanya kazi na watu wenye ulemavu Tz na ilikuwa ni proposal kubwa tuu yenye pesa mingi. Kwa kweli nivutiwa na ile proposal sasa pale ikawa ishu ni menejiment ya ofisi yetu wakiiridhia tupige kazi. Ndio mana alikuwa anafosi sana kuonana na menejiment.
Nikamwambia mimi na yule sistaduu ni sehemu pia ya menejiment ila hilo swala ni bodi ya wakurugenzi sio CEO peke yake. Ila nikamhahakikishia atapewa jibu ndani ya hiyo wiki moja. Basi akanishukuru pale tukabadilishana biz cards. Pia akaniachia na ile proposal ili niipitie vizuri ili nitakapoiwasilisha kwa wakubwa iwe rahisi. Aliniachia full proposal yenye mpaka bajeti, ilikuwa ni kubwa mno. Ile project ilikuwa ina nafasi nyingi tuu za kazi kwa wale watakaobase pale ofsini na watakaohitajika kule kwenye shirika lao. Nikaisoma pale then nikamshirikisha sista duu. Unaambiwa alipagawa sana baada ya kuiona ile proposal. Nikamuonyesha na biz card ya yule rasta alipagawa zaidi mana jamaa alikuwa ni partnership advisor wa hilo shirika so ni cheo kikubwa sana. Basi kwenye kuzicheki zile positions mimi nikaona moja ambayo inafaa kubase kule kwenye shirika nikasema hapa lazima nifanye jambo. Na sista duu nay eye aliiona ya mkuu wa kitengo cha M&E ipo akasema nay eye lazima afanye jambo. Sikutaka kumakatisha tama pale na pia sikutaka kumwambia jinsi yule rasta alivomkataa wakati tunafanya nae kikao kile.
Basi mimi nikampigia simu CEO na kumpatia ile taarifa akasema ataitisha kikao cha menejiment na bodi kesho yake. Kweli siku ya pili mimi nikapresent ile proposal utafikiri mimi ndio niliyeiandaa. Basi huku na huku nikapewa jukumu la kumjibu yule jamaa kwamba menejiment na bodi ya wakurugenzi imeridhia kufanya ule mradi in partnership na shirika lao. Basi siku hiyo hiyo nikamu-email rasta na akarespond promptly kwamba wataorganize a skype meeting baina yao na sisi. Baada ya kama siku tatu tukafanya skype meeting pale na deal was closed kwamba tuanze maandalizi ikiwemo kutafuta wafanyakazi.
Basi tukatoa matangazo pale. Binafsi nikamcheki rasta kwa wasapu kumwambia kuwa nina interest na ile position niliyoiona kwenye proposal ambayo ipo kule upande wao. Pale pale akanicall na akanifanyia interview kwa njia ya simu ambayo sikujiandaa kabisa. Akaniambia japo sijaona CV yako lakini nitakuinterview technical questions basi tukafanya interview tukamaliza. Ila akaniambia atanitumia email ya mwajiri wa ofisi yao wa Nairobi ili nitume CV na cover letter. Alivonitumia email address na mimi nikaandaa CV yangu na cover letter faster nikamtumia yule mwajiri. Akanijibu nijianda kesho nitafanyiwa interview kwa video call. Kweli kesho yake tukanya interview, walikuwa panelist wawili nakumbuka rasta hakushiriki. Pale pale wakaniambia nimepata Kazi so nisubiri offer letter. It was simple like that.
Basi wiki iliyofata kweli nikapokea offer letter na contact ambao nilitakiwa nisign na kuwarudishia immediately. Siku ya pili nikapokea simu kutoka kwenye ofisi yao ya hapa Dar ambapo ndio ingekuwa ofisi yangu mpya ya kufanyia kazi. Nikatakiwa nipeleke testimonials zangu kwa uthibitisho, basi nikafanya hivyo na nikawaomba wanipe mwezi mmoja ili niweze kumalizana na huku kwa walemavu. Ujue sio vizuri kuondoka mahali ukiwa na vimeo vimeo, clear kwanza vimeo vyako ndio uondoke na huo ndio uprefessional.
Baada ya wiki wakati tangazo la kazi limetoka sista duu akaniuliza taidume tunafanyaje sasa maana chansi ndio hii mimi nikamjibu mwenzio hapa nilipo naandika resignation letter naenda kujoin na shirika la rasta. Akashtuka sana akaniuliza mbona muda bado mpa briefing pale akashangaa sana. Akaniambai nayeye atamcheki. Ikabidi nimwambie tuu ukweli pale kwa situation yake itakuwa ngumu maana rasta hataki hata kumuona na hata mpa ushirikiano wa kutosha na anawza akamuharibia kabisa.
Nikamshauri kwa kuwa rasta hamjui kwa jina ni bora tuu akafanya procedures za kawaida anaweza akapata maana una CV nzuri. Akanijubu wewe niconnect basi, msaada wako utakuwa umeishia hapo kuhusu hayo mengine niachie mimi hakuna mkate mkate mgumu mbele ya chai. Nikasema poa. Pale pale nikamcall rasta na kumweleza interest za sista duu. Sasa rasta akataka kujua huyo sista ni nani nikamwambia subiri nampa namba yako atakupigia. Kweli nikampa sista duu akasema atampigia jioni akiwa off.
Basi tukaendelea na majukum na mimi nikasubmitt ile resignation letter kwa mkono kwa CEO. Kiufupi alisikitika sana lakini kwa kuwa alikuwa mwelew akaniruhusu kwa moyo mmoja. Usiku kwenye saa mbili hivi wakati nipo home napiga msosi mara nikaona rasta ananipigia. Nikajiuliza kuna nini tena? Kupokea pale akaniambia tuu kifupi ofisi yao haiwezi kufanya kazi na sista duu. Akaniamba wewe umepata ile kazi sio kwa sababu una vigezo vikubwa kuliko watu wengine bali additional value was the respect you showed when we first met. Basi akaniongea sana pale akasema wao katika ofisi yao wanasisitiza sana kuheshimu na kujitoa kwa ajili ya watu wengi. Akanianbia hata sista duu amemweleza maneno hayohayo na kumwambia wazi kwamba hawawezi kufanya nae kazi. Basi tukagana pale na mimi nikamcall sista duu kumuuliza imekuwaje maana jamaa kanipigia. Alichoniambia tu niachane na mambo hayo ahikuwa rizki yake na rizki anatoa Mungu. Kwa yale majivuno yake sikutaka kumshauri chochote.
Ndio ikawa hivyo hivyo ndugu zanguni.
Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa