Mambo tata matatu, Uteuzi wa Jaji Kiongozi Siyani

Lakini haiwezi ikatafsiriwa kuwa ni rushwa ili atende anayotaka mteuzi, endapo kama cheo chake hicho kipya kitamwonyesha kubadilika na alivyokuwa mwanzo?
Mkuu hapa umenena. Uwezekano huo upo mkubwa. Maana ya rushes ni matumizi mabaya ya ofisi kwa maslahi binafsi. Hili nalliona kwa mbali.
 
Mama sijui ana mataizo gani! Kulikua kuna ulazima gani wa kufanya uteuzi wakati mchakato wa kesi ukiendelea?
Kwamba hakutakuwa kuteua kwakua kesi ya Mbowe haijaisha? Ni sheria gani inamzuia?

Mnapenda kuhubiri utawala wa sheria ila linapokuja swala linalowahusu nyinyi sheria huwa mnaisahau kabisa,mnaanza kufikiria kama kuku kishingo.
 
Kwamba hakutakuwa kuteua kwakua kesi ya Mbowe haijaisha? Ni sheria gani inamzuia?

Mnapenda kuhubiri utawala wa sheria ila linapokuja swala linalowahusu nyinyi sheria huwa mnaisahau kabisa,mnaanza kufikiria kama kuku kishingo.
Kubali tu huu uteuzi una kitu ndani yake. Na ndiyo maana tunaipigia kelele Katiba Mpya ili ipunguze sintofahamu kama hizi.
 
Implications ya uteuzi wa jaji Siyani ni kwamba anatakiwa kuhama kutoka Mahakama Kuu Masjala ya Rushwa na uhujumu uchumi kwenda Mahakama Kuu Masjala Kuu (Main Registry). Sasa kwakuwa Mahakama zote hizi ziko Dar sioni ulazima wa yeye kuacha kuendelea kusikiliza hilo shauri.
 
Huwezi kuelewa alichoondika Yeriko maana inaonekana huna ufahamu wa logic, haki au wewe si mtu mwenye mapenzi mema.
Yerico ni nani hata asiwe challenged kuwa vitu anavyoandika? Ukiona hauwezi kum-challenge ujue amekuzidi ubongo (una ubongo wa kuku), lakini hiyo isiwe sababu ya wengine kukaa kimya kama wanaona anachoandika Yerrico ni pumba.
 
Tatizo lenu CHADEMA tayari mnayo hukumu mliyokwishandaa kuhusu kesi ya Mbowe kutuhumiwa ugaidi. Tuwe watulivu tusubiri matokeo.
 
Yericko Nadhani Jaji Kiongozi anaendelea na Majukumu yake yale hii ni title tu
Asante mkuu kwa kuwaelewesha, Jaji Kiongozi haondolewi majukumu ya kusikiliza mashauri, japo atakuwa mtawala zaidi kuliko Jaji wa mahakamani
 
Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo ambaye ndiye Mungu wetu msaidie jaji huyu akafanye haki.... Na ikawe hivyo mbele yako Bwana Mungu.
Jaji simama na utende..AMINA
 
Nawewe Ni laana ya Aina yake. Huoni tatizo katika uteuzi huu
In your good opinion unadhani nani alitakiwa ateuliwe kuwa Jaji Kiongozi? Maana naona mmekaza misuli ya shingo kuhusu uteuzi wa Jaji Siyani kwa hoja ambazo hazielezeki iwe kisheria wala kwa misingi ya kanuni za natural justice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…