Mambo tata matatu, Uteuzi wa Jaji Kiongozi Siyani

Mambo tata matatu, Uteuzi wa Jaji Kiongozi Siyani

Yaan unamtetea zombe????ama kweli kila mmoja anatetea nafsi yako
Kitabu usichokielewa hakikuandikwa kwa ajilli yako.

Waandishi wa mihemko ndio walioupotosha UMMA na kuwaaminisha watanzania kwamba Abdallah Zombe aliwapiga risasi wafanya biashara wa Madini.

Inatubidi tujifinze kuweka maneno ya akiba ndiyo busara.
 
Uteuzi wa Jaji Siyani kuwa Jaji Kiongozi una sura tatu tata sana.

1) Ikiwa Jaji Kiongozi Mh Siyani atalazimika kuachia Jaji mwingine hii kesi ya Mh Mbowe, Athari za kuteuliwa jaji mwingine kwenye kesi hii ni kwamba ajaye anaweza kutoa maamuzi kwaniaba ya mamlaka za uteuzi ili nae apendelewe kupata ulaji wa ujiaji kiongozi... Hi ni dhana yangu tu tata.

(2) Ikiwa Jaji Kiongozi Siyani licha ya kuteuliwa kuwa Jaji Kiongozi ataendelea kusikiliza kesi ya Mh Mbowe, Upande wa Pili wa dhana yangu tata nikwamba, athari za Jaji Siyani anayesikiliza kesi hii ikiwa maamuzi yatakuwa kinyume na "UMMA", itatafsiriwa kwamba kapata asante kuwa jaji Kiongozi kabla hata kazi haramu ambayo mteuaji alishahukumu mbele ya dunia kupitia BBC Swahili hajaimaliza.

(3) Na kwa asilimia ndogo sana ikiwa Jaji Kiongozi Mh Siani ataendelea kusikiliza kesi kama kawaida, inaweza kuwa sasa ni ahueni kwa "umma" kwakuwa Jaji kiongozi atakuwa huru zaidi kuamua kwa haki bila hofu ya kuingiliwa tofauti na awali alipokuwa jaji wa mahakama kuu tu.

Kwa mizani hii mitatu na kwa asili ya siasa za kiutawala za Dar es Salaam, tuendelee kupiga magoti kila mtu kwa imani yake haki itendeke na ionekane kutendeka.

Na Yericko Nyerere
View attachment 1968603
Tunasubiri na kufuatilia kwa kqribu sana tusisahau kuchangia wake za makomandoo wanaoteseka......
 
Halafu kitu kama hiki kilishatokea awamu ya Mkapa mwishoni mwa miaka ya tisini.
Aliyekuwa Jaji Kiongozi, B Samatta alikuwa anasikiliza kesi baina ya makundi yaliyokuwa yakikinzana katika NCCR Mageuzi nadhani kuhusu kutambuliwa kwa wajumbe wao wa Baraza la Wadhamini kuhusu ulipwaji wa ruzuku.
Serikali ilionekana kuwa upande wa akina Marando, dhidi ya Lyatonga.
Wakati kesi inaendelea ghafla Mkapa akamteua Samatta kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Hamisi Msumi akateuliwa kushika nafasi yake.
Naomba tukumbushane kilichojiri baadaye kuhusu kesi ile.
 
Kawaulize Wapemba wanachofanyiwa huko kisha ulete mrejesho.
li ni miongoni mwa matatizo ya msingi ya Chadema. Hawana jema na wana pupa. Tangu lini mzanzibari akawa na siasa za kukomoa?
 
kwanini usibaki na namba tatu halafu hayo mengine ukayaacha?...

Jaji naye ni mtanzania, anahaki zake naye kama mtanzania, kesi ya Mbowe ni kesi kama kesi nyingine isitulazimishe kuacha mengine eti kwa sababu Mbowe anakesi iko mahakamani...
 
Naona Kama Yesu anachelewa kuja....ili sote tupange foleni kule kwenye tanuru
 
Sasa watu wasioona umuhimu wa Katiba mpya, ambayo inatakiwa iyapembue vizuri mambo kama haya, hapo ndipo pa kuanzia kunyoosha uelewa wao juu ya Katiba Mpya.

Ni jambo muhimu sana huyu mtu anayeitwa rais, asiwe ndiye mtu wa kuamua kila kitu bila kuwa na mipaka. Bunge haliwezi kumhoji, wala halina nafasi au sauti yoyote juu ya kila jambo analofanya. Hii siyo sawa hata kidogo.

Pili, hukumu itakayotolewa na mahakama yoyote juu ya hii kesi ya Mbowe, kutokana na mambo mengi ambayo yamekwishafunuliwa hadi sasa; kuna mahakama nyingine ambayo itaona na kuhoji uamzi wa kesi hii kama utakuwa umefanywa kwa kupindisha sheria.
Hapa atakayekuwa anajiaibisha ni huyo mteuzi, kama amefanya uteuzi kutokana na dhana ya kuyumbisha kesi hiyo. Aibu yake haitaishia Tanzania, bali dunia nzima itakuwa imefahamu maksudi ya huyo mwenye nia mbaya.
Yaani watu waone tatizo la katiba kwasababu ya matatizo binafsi ya Mbowe.

Are you guys serious ??
 
Chadema hamna jema!
Maoni ya mtu binafsi iweje yawe branded kama maoni ya chama kizima...?

Haya ni maoni ya Yericko Nyerere, hayahusiani na CHADEMA kama taasisi...!

By the way, haya mengine yapo tu na ni uamuzi wa mteuzi....

Kwa shauri lililoko mahakamani dhidi ya Freeman Mbowe ambalo Jaji Kiongozi Mteule Mustapha Siyani analisikiliza, kinacho matter ni haki kutendeka na ionekane imetendeka....!

That's all. Nothing more, nothing less...
 
In your good opinion unadhani nani alitakiwa ateuliwe kuwa Jaji Kiongozi? Maana naona mmekaza misuli ya shingo kuhusu uteuzi wa Jaji Siyani kwa hoja ambazo hazielezeki iwe kisheria wala kwa misingi ya kanuni za natural justice
enjoy your saturday!
 
Uteuzi wa Jaji Siyani kuwa Jaji Kiongozi una sura tatu tata sana.

1) Ikiwa Jaji Kiongozi Mh Siyani atalazimika kuachia Jaji mwingine hii kesi ya Mh Mbowe, Athari za kuteuliwa jaji mwingine kwenye kesi hii ni kwamba ajaye anaweza kutoa maamuzi kwaniaba ya mamlaka za uteuzi ili nae apendelewe kupata ulaji wa ujiaji kiongozi... Hi ni dhana yangu tu tata.

(2) Ikiwa Jaji Kiongozi Siyani licha ya kuteuliwa kuwa Jaji Kiongozi ataendelea kusikiliza kesi ya Mh Mbowe, Upande wa Pili wa dhana yangu tata nikwamba, athari za Jaji Siyani anayesikiliza kesi hii ikiwa maamuzi yatakuwa kinyume na "UMMA", itatafsiriwa kwamba kapata asante kuwa jaji Kiongozi kabla hata kazi haramu ambayo mteuaji alishahukumu mbele ya dunia kupitia BBC Swahili hajaimaliza.

(3) Na kwa asilimia ndogo sana ikiwa Jaji Kiongozi Mh Siani ataendelea kusikiliza kesi kama kawaida, inaweza kuwa sasa ni ahueni kwa "umma" kwakuwa Jaji kiongozi atakuwa huru zaidi kuamua kwa haki bila hofu ya kuingiliwa tofauti na awali alipokuwa jaji wa mahakama kuu tu.

Kwa mizani hii mitatu na kwa asili ya siasa za kiutawala za Dar es Salaam, tuendelee kupiga magoti kila mtu kwa imani yake haki itendeke na ionekane kutendeka.

Na Yericko Nyerere
View attachment 1968603
Uchambuzi huu tutaendelea kuufuatilia siku hadi siku, mpaka mwisho wa kesi husika
 
Ushahidi wa Adamoo utakataliwa kupokewa na mahakama au Mbowe na wenzake wataachiliwa huru.
"Ushahidi wa Adamoo utakataliwa na mahakama"; ikitokea kuwa hivyo, hapatakuwa na kesi tena!

Sasa baada ya hapo? Watu watafurahi na kusifu haki ilivyotendeka? Hakuna atakayesikitishwa na mfumo huu unaovuruga maisha ya watu?

Mimi ningetumaini kesi hii ndio ungekuwa mwanzo wa kukataa manyanyaso ya aina hii yasiendelee ndani ya taifa letu.
 
Umesema vyema sana tuendelee kupiga goti haki itendeke. Haki inaweza Kuwa mbowe kufungwa akipatikana na hatia au kuachiwa Huru kama Hana hatia.
Don't forget
 
Yaani watu waone tatizo la katiba kwasababu ya matatizo binafsi ya Mbowe.

Are you guys serious ??
Incredulously, at one time I considered you to be a reasonable and level headed contributor to these forums. What happened to you?
I mean, you have proved yourself to be not any different from the likes of Jingas, Magonjwas, Etweges, etc!
 
Back
Top Bottom