Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Uteuzi wa Jaji Siyani kuwa Jaji Kiongozi una sura tatu tata sana.
1) Ikiwa Jaji Kiongozi Mh Siyani atalazimika kuachia Jaji mwingine hii kesi ya Mh Mbowe, Athari za kuteuliwa jaji mwingine kwenye kesi hii ni kwamba ajaye anaweza kutoa maamuzi kwaniaba ya mamlaka za uteuzi ili nae apendelewe kupata ulaji wa ujiaji kiongozi... Hi ni dhana yangu tu tata.
(2) Ikiwa Jaji Kiongozi Siyani licha ya kuteuliwa kuwa Jaji Kiongozi ataendelea kusikiliza kesi ya Mh Mbowe, Upande wa Pili wa dhana yangu tata nikwamba, athari za Jaji Siyani anayesikiliza kesi hii ikiwa maamuzi yatakuwa kinyume na "UMMA", itatafsiriwa kwamba kapata asante kuwa jaji Kiongozi kabla hata kazi haramu ambayo mteuaji alishahukumu mbele ya dunia kupitia BBC Swahili hajaimaliza.
(3) Na kwa asilimia ndogo sana ikiwa Jaji Kiongozi Mh Siani ataendelea kusikiliza kesi kama kawaida, inaweza kuwa sasa ni ahueni kwa "umma" kwakuwa Jaji kiongozi atakuwa huru zaidi kuamua kwa haki bila hofu ya kuingiliwa tofauti na awali alipokuwa jaji wa mahakama kuu tu.
Kwa mizani hii mitatu na kwa asili ya siasa za kiutawala za Dar es Salaam, tuendelee kupiga magoti kila mtu kwa imani yake haki itendeke na ionekane kutendeka.
Na Yericko Nyerere