Mambo Usiyoyafahamu Kuhusu ushoga na Jinsi Unaweza kuwaepusha Watoto Wako

Mambo Usiyoyafahamu Kuhusu ushoga na Jinsi Unaweza kuwaepusha Watoto Wako

Mi naumiza kichwa kumjua huyo mwanasiasa na msanii
Nimesoma comments huko juu inavyosemekana mwanasiasa ni bwana waziri mdogo mwenye upara
Na msanii ni yule mtoto wa fela aliehit Sana kipindi fulani
 
Mimi sipromote ila nataka jamii ipate awarness ya nini kinaendelea…Kuficha ficha ndo shida zinakuwa nyingi….kutoka kwenye comments inaonesha kabisa watu hawajui kuhusu huu ushoga so ni ngumu hata kwa wao kutambua au kubaini viashiria vya mwanzo ili wawezs kuwasaidia…Wengi wanakuja kugundua imeshakuwa too late…Acheni jamii ipate mwanga ili tuokoke

Imagine una kijana wako wa kiume anajihusisha na vitendo hivi ila kwa siri,wewe hujui na unakua huna shaka kisa ana videmu viwili vitatu kumbe vile videmu ni kwa ajili ya kufunika kombe mwanaharamu apite…Sasa kupitia huu uzi mtoa mada amebainisha shoga anaweza kuwa na demu au hata mke so kuna kitu watu wanajifunza kuliko kukaa kimya na ujinga wetu
 
Hapa ni kumtafuta dem wa huyu mtoa mada ili tumle kimasihara, maana naona anakosa ukuni waziwazi.
 
Nimesoma comments huko juu inavyosemekana mwanasiasa ni bwana waziri mdogo mwenye upara
Na msanii ni yule mtoto wa fela aliehit Sana kipindi fulani
👏👏👏Ngoja nipekue pekue
 
Jamaa kafunguka ukweli mwingi tu
Mambo aliyoyagusia yote ni dhahiri yapo ,na mwanaume akishaanza kula ile kitu ni ngumu kuacha ,shoga akilewa anaushawishi mkubwa mno yani seduce yake ni zaid ya mwanamke

Yupo rafiki yangu nimekuwa nae nimecheza nae hizi tabia ni tangu utoto nafikiri kuna hormone zilimzidia

Alilewa siku moja alinishawishi ilikuwa kidogo tu nimle bahati sikuwa pombe nilikuwa timamu nikamescape

Mwingine aliniita kwake kijanja ila huyu alikuwa na HIV,sikumla alinipa offer y kitu nikitakacho,

Fb sasa ndo zaidi ya kumi ila hakuna hata mmoja niliemfokea wote niliwasikiliza nikawaescape kijanja mno

Hadi wazee kabisa wapo ni gay
Mwanume utumie uanaume wako ipasavyo ukikaa tu mwili utakupeleka unavyotaka na inakuwa ngumu kuucontrol when it too late
 
This thread seems planned to me. It’s clearly a set up by some pro-gay NGO to win hearts and minds. I could see a sudden surge of aggresive pro gay posts from multiple individuals seemingly from no where; their main goal being to shut down peeps having opposite but valid arguments and concerns against the proliferation of homosexual behavior in society.
 
Uhalisia upo ivo ila mtoa mada unabidi ufanye jitihada za kuacha sasa kama ni porno video za gays zinakuhamasisha uache kuangalia na vile unasema una vijisent vya kununulia na mabando ya kutosha basi ukiwasha vpn unatataka ufukue fukue huko mpaka upate hisia za kufanya tendo hilo..tafta muda wa kuenjoi zaidi na demu wako unavoleta mikausho ndo hiyo hali inakuzidia ya kujiona unajiweza kumbe unapojiona unajiona ndo unaharibu zaidi,, kuna wakat inabidi upate tiba ya hisia kwa hisia sas hapo ni wewe kufosi ila ukikomaa kusema ni hisia zinakujia hapo utakua unafel kwanini zisikujie hisia za kujiua kwamba unywe sumu ufe au ujikate kichwa cha uume wako ila zinakuja hisia za kuingiliwa kimwili kinyume na maumbile jambi la kwanza hapo unatakiwa ujue unapambana na pepo wale waliofanya sodoma na gomora zikawashwa moto hivo unapopambana na hio hali muombe Mungu sana sana akusaidie kushinda hilo pepo tumia njia mbali mbali kuacha tumia chumvi ya mawe inuizie nia yako ogea kwa siku 21 mfulilizo bila kukosa pia katika hili nenda kwa mwanasaikolojia mwambie ukweli atakusaidia then zingatia ibada kama ni juma mosi ama jumapili naamini utakaa sawa..
 
Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu kuna watu walikuwa na dhambi ikiwemo kuua watu wengi kupitia ujambazi na uchawi kuna watu waliukana ubinafsi kwa kuuza nafsi zao,wakafanyiwa ukombozi wa kumpokonya shetani tena kwa lazima aaichilie nafsi ya mtu na sio ombi, baada ya nafsi zao kukomboka leo wapo poa wamesimama na maisha yanaenda.
Pambana fanya mazoezi ya kuirejesha nafsi yako itoke kwa shetani ikitoka tu ile kiu ya kutamani kiu ya kuwashwa itaisha.Ni mafunzo ya kuvishinda vita vya kiroho tu.
Ushoga sio biology ni spirit.
Ulishawaj kuwa shoga?? Yeye ametoa ushuhuda wake nadhani ungemuonea huruma kuliko kumpinga, kama alivyosema angetamani kuwa binadamu wa kawaida lkn imeshindikana, tumwombee
 
Ulishawaj kuwa shoga?? Yeye ametoa ushuhuda wake nadhani ungemuonea huruma kuliko kumpinga, kama alivyosema angetamani kuwa binadamu wa kawaida lkn imeshindikana, tumwombee
Soma uelewe vizuri ndugu.
Yasiyo wezekana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana.Kama mateja wameacha uteja,kwann ushoga ushindikane.Hakuna tabia inayoshindikana
 
Ni ndefu kiasi ila jitahidi umalize.

Natumaini Wote Mu wazima wa afya, kwa walio wadhaifu basi Mungu awaponye na awatie nguvu tena.

Modes nimeamua kutumia ID tofauti na ambayo huwa natumia kwa sababu za privacy tu sababu ID nayotumia nafahamika personally na baadhi ya watu, kwa hivyo naomba msije ku reveal hata mkijua (the matter of privacy), nataka tu kutoa elimu kiasi kuhusu hili jambo kwa faida ya wote.

Kwanza niwape pole wazazi au familia ambazo wamekua na mmoja wa familia ama mtoto mbae labda ni gay/shoga na wameumizwa na jambo hilo,najua sio rahisi kuli handle, ni fedhea hasa katika jamii zetu, ila napenda kuwaambia msijione labda ni wazazi wabaya, au labda hamjui kulea, is not your fault.

Dhumuni kuu la kuanzisha hii thread si kwa ajili ya kuongelea uzuri au ubaya wake ila ni ili kutoa a simple knowledge ya jambo husika (gay) na ili pia niweze kuwapa mwanga wazazi na watu ambao jambo hili limekua likiwachanganya na kuwahudhunisha na labda jinsi ya kuokoa watoto pia. Kwa maana nimesoma maoni na mada nyingi ambazo huandikwa humu na maybe 80% ni very wrong na si kwa ubaya bali ni kwamba wengi hata hawajui jinsi inavokua na kwa kutokujua inafanya hata wasiweze kujua chanzo, na jinsi ya kuepukana na hilo. Nimeonelea mayb ni vyema kama mtapata kitu kutoka kwa real person who have real experience.

Karibu👇
Wengi wangependa kujua kuhusu mimi, watu wengi wamekua wakijiuliza mtu anakuaje gay, ukiniuliza nimekuaje gay sina jibu kamili kuhusu hilo swali, hata ukiniuliza nilianza lini kuwa gay sitakua na jibu sahihi.

KUHUSU MIMI
Ni kijana, kwa sasa nina 26 years, nimesoma hadi degree, ninafanya kazi nimeajiliwa mahali, sitarajii kuoa soon wala sijawahi kuwaza kuhusu hilo japo mama anaexpect soon nimletee daughter inlaw, hajui kama kijana wake ni gay na wala hajawahi kuhisi, sababu ukiniangalia kwa macho mimi mwanaume kamili, sina girlish behaviour, nina marafiki almost wote ni straight, na wao pia hakuna mtu anajua kua im gay, nina girlfriend pia, napenda kuvaa casual na sitembei kiajabu ajabu niko very normal in my formal life, ila nina boyfriend pia, lakini nina girlfriend pia wakuzugia (yes na hii siifurahii sababu nafanya kuridhisha marafiki na wazazi ili wasihisi chochote na pia sitaki kuwaudhi wala kuwadhalilisha ndugu zangu kwa jambo ambalo najua kabisa jamii yetu haipendi japo ndivyo nilivyo).

Sijawahi kufurahia kua gay hili niweke wazi, na siwezi taka mtu awe, and im not proud of it na siwezi taka mtu wangu wa karibu ajue that im gay, na wala siwezi taka mtu awe gay, ila siwezi kujizuia, ni automatically nimezaliwa hivyo, hakuna mahali nilijifunza au story za vijiweni labda nilifanyiwa vitendo vya ukatili hapana , nachojua ni tangu nikiwa mdogo sijawahi kuwa na hisia na msichana hata kidogo nimejaribu kujifunza sana jinsi gani nihamishe hisia zangu, lakini nimeshindwa, sababu mpaka leo ukiniwekea msichana mrembo sana mbele yangu na mwanaume handsome mbele yangu kitakachotokea ni kuwa mwanaume atateka akili yangu yote, msichana taona tu ni mrembo its fine, hata awe amevua nguo maybe sitaweza hata kumuangalia sababu nitaona is disgusting. Ila yule mwanaume nitakua ni kama vile ambavyo mwanamke akiona mwanaume handsome anavofeel. Natumai umepata picha japo kidogo.
Niliwahi kudhamilia kua straight ila nikashindwa, hisia kwa girls ni sifuri kabisa, natamani ningekua kama wanaume wengine ila nimeshindwa, yani automatically tu, na mahitaji ya mwili yako pale pale.

KABLA NIANDIKE MAMBO MENGINE MENGI, TAFADHARI ZINGATIA HUU USHAURI.

SOMA KWA MAKINI JINSI YA KUEPUSHA WATOTO NA MASWALA HAYA (hapa zaidi kwa wale ambao sio natural born ila wanataka kujaribu)

1- hakuna mzazi au mtu anaweza kuzuia kabisa lisitokee zaidi ya Mungu, hivyo jambo la kwanza kabla ya yote ni kuombea familia yako Mungu awaepusha kizazi chako.

2- Wengi hawapendi kuongea na vijana wao kuhusu masuala ya gender na masuala ya mahusiano na masuala ya sex, hii ni mbaya sana, sababu unampa uwanja mkubwa kijana ajifunze hayo mambo mtaani, wazazi msione aibu kuongea na watoto wenu, siongelei wakiwa wamekua, hapana ila wakiwa wadogo kabisa ongea nao, waambie wewe ni mwanaume na wewe binti, mwambie wewe mwanaume usikubali mtu akufananishe na mwanamke, muelezee yote yanayompasa kutenda kama mwanaume, mwambie mambo ya kuingiliwa sio yako, pia muelekeze kuhusu afya yake, matumizi ya condon, nchi za qwnzetu haya wanafundishwa hata shuleni , ila huku bado ni taboo kuongelea , ongeeni na watoto wenu kuhusu sex na yanayohusu jinsia yao.

3- Usikubali mtu yoyote amfananishe mtoto wako wa kiume na msichana, au kumsifia wewe ni mrembo, mwambie na umfundishe mtoto ako kabisa kua wewe ni wa kiume, wewe sio mrembo, mtu akikuambia hivo manaake anakutukana na anakudhalilisha, mtengenezee mindset mtoto wako ajione yeye ni mwanaume ,jambo lolote linalomfananisha na mwanamke achukulie ni matusi na dharau, nataka kusema tu kua hii mindset game inasaidia sana mtoto kujizuia hata kujaribu mambo furani sababu ameshaweka kwa akili yake kua ni kitu kibaya, na hii itafanya hata kuwa vigumu kushawishika. (nitelezea chini zaidi)

4- Mtoto akiwa mdogo, tafadhari wewe mama, dada, kaka, baba, ukiona anapenda vitu wanavyopenda wasichana, anapenda kujaribu jaribu viatu vya kike, rangi za kucha, sjui midoli ya princes , ama kuiga waschana either wanavotembea au kuongea, usifurahie , hapo kengele ilie kichwani mwako, hapo fanya jitihada zote kumnusuru mtoto katika umri huo mdogo, akipita hapo, basi huezi fanya kitu tena. Kuna watu watasema mbona wangu alikua hivyo na sasa sio gay, nakwambia ni gay ila incloset like me, ila huezi kujua sababu anafanya iwe privacy. Kama huamini, fanya jambo moja, hakiisha una unlock simu yake bila yeye kujua na fatilia emails, texts, whatsapp, browsing history etc, utapata kitu hakika.

Jambo la mwisho ni kufatilia mienendo ya watoto wenu, hapa nimesema kabisa , kama mtoto ni gay atakua gay tu huwezi zuia ila kwa kumtegemea Mungu peke ake, ila angalau ukifanya hayo ya juu , utamuokoa mtoto wako na familia yako kutoka kwenye fedheha na aibu ndogo ndogo na kubwa, sababu ni afadhari awe gay na usijue pia watu wasijue iwe siri yake kuliko ukute mwanao amevaa kama mwanamke anakatiza mitaani na makeups, ama uone watu wakimdhalilisha nitandaoni sababu ni gay, hiyo inaumiza zaidi.

HAYA CHINI NI MAONI YANGU NA EXPERIENCE YANGU NA PIA UFAFANUZI WA BAADHI YA MASWALA PENGINE UNAWEZA KUJIFUNZA KITU NA KIKAKUSAIDIA KUJUA JINSI YA KUHANDLE.

Kuna watu nimeona humu wanacomment kua gay unaweza mtibia hospitalini, kwamba unampeleka gay anaenda kupigwa bomba sababu akiingiliwa anakua anawashwa huko kwenye haja kubwa hivyo akiwashwa anatafta mtu wa kumuingilia, HII STORY SIO UKWELI

Kua gay ni suala la hisia zaidi , wala sio swala la kuwashwa, ni hisia, badala ya mtu kupenda jinsia tofauti anapenda jinsia yake, hii story ya vijiweni itafanya kweli wazazi wahangaike kupeleka mtoto wao akapigwe bomba ili aache kua hivyo na kumbe wanapoteza tu pesa na muda bure, hii story ya kuwashwa sjui hata watu wameitolea wapi.

Nimekua gay tangu niko mdogo, naongelea kihisia yani kupenda same gender, ila mala yangu ya kwanza kusex ilikua wakati nipo na 14 years, miaka hiyo yote hadi nafikia miaka 14 sikuwahi kuwashwa huko, na hata baada ya hiyo first time sijawahi kuwashwa , sababu hisia zinatoka ndani sio huko, ni kama msichana akimpenda mvulana , sijui kama hua anawashwa huko chini, nachojua ni hisia tu, anampenda mtu na anatamni kua nae, pia huko iko hivyo. Hakuna gay anaewashwa huko chini ndio atake kuingiliwa, hivyo hata ukipata mwanao yupo hivyo hio sio solutuon hata kidogo. Watu wanaopigwa bomba ni wale waliokua assulted , na wanatoa zile sparm kwa njia ile ili kuepusha maambukizi yoyote uko kwenye haja kubwa kama fungus au magonjwa mengine kama aliemuingilia alikua na magonjwa, na mtu akiwashwa huko basi ni kwa sababu amepata maambukizi either ya fungus au bacteria , ndio anakua anawashwa thats why anafaa akapigwe bomba, hata wasichana wakibakwa na wakalawitiwa pia hupigwa bomba kuepusha hizo infections.

Suala lingine watu wengi wamecomment ni suala la kusena ati vijana wanajiingiza kwenye ushoga sababu wanapenda maisha mazuri hivyo wanakubali kuingiliwa ili waishi maisha ya starehe na wanajiuza sjui na nini. Huyo anaefanya hivyo ni prostitute tu kama ilivyo kwa straight wanaoamua kujiingiza kwenye ukahaba ili wapate pesa. Nachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anaejibadilisha kua gay, maybe yes hao wa hivyo wako ni kama straight people tu, sio kila msichana anajiuza ila wako wanaojiuza kwa sababu zao, the same kwa hawa gays pia wako wanaojiuza ila wengi pia hawajiuzi wala hawafanyi sababu wanataka pesa ama nini hapana.

Mfano kuhusu mimi, nimetokea familia yenye uchumi mzuri, nimesoma, ninakazi yangu nzuri yenye mshahara mkubwa, nina kila kitu cha muhimu ambacho vijana wengi au watu wengi wangependa kumiliki pia na vyote nimevipata kwa kupambana, na work very hard, namake sure sikati tamaa wala kutegemea favour ama kutarajia kitu kutoka kwa boyfriend, NO, unawezaje sema nimekua gay sababu nataka mteremko sjui maisha mazuri? Hivyo hiyo dhana muachane nayo, wazazi deal na hisia za mtoto, usijefikilia labda hujampatia maisha mazuri ndio kawa hivyo, hapana, tena wengi walitoka familia bora ndio wanakua hivyo, ni sababu wanazaliwa hivyo.

Pia kuna watu wanasema kwamba mtu anakua gay sababu labda aliingiliwa kwa nguvu akiwa mtoto labda aliingiliwa na mjomba ama sjui nani ndio akawa hivyo, hii pia ni uongo, kwa sababu kuna watu waliwahi kulawitiwa wakiwa wadogo au hata wakiwa wakubwa ila hawajawahi kubadilika na kuwa gays na wameendelea kua malijali mpaka sasa japo hilo swala la kulawitiwa lime waaffect psychologically (sio kua gays), hivyo hata mtu akibakwa hawezi kubadilika na kua shoga, akibadilika ujie alikua gay kitambo.


Lakini pia nataka mfahamu jambo moja, kua hili tatizo ni kubwa sana katika jamii yetu (nimetumia neno tatizo sababu linahesabika kama tatizo kwenye jamii), ni kubwa kuliko mnavodhani, watu wanawaangalia hao gays kama kina James delicious wanaojionesha na akiona watoto wake wako sawa anatukana hao wengine, hapana hujajua tatizo lilivyo bado. Sitaki kuongelea sana hao wanaojionesha sababu pia sijawahi kujiassociate nao wala sijawahi kua na rafiki anaejionyesha hivyo sijui sana. Ila fahanu haya kwa leo:-

Taelea hii mifano inayonihusu ili mjue kua hata ndoa haziko salama sana kama watu wanavoamini kwamba mtu akioa hawezi kua gay.

(1) Wanawake mlioko kwenye ndoa ombeeni ndoa zenu sana. Siwezi sema ni kwa % ngapi ila wanaume wengi ni bisexual, au bisexual curious, mimi binafsi nimewahi kua kwenye relationship na mume wa mtu sio mala moja. Ngoja niongelee hii sababu nimekua napatana sana na mtu ambae ni mume wa mtu mala nyingi, moja ambayo ilikua very serious relationship pia alikua mume wa mtu, from very happy family, alikua sometimes wanakuja wote na mke wake office ninapofanya kazi , hii ilikua inanikasirisha sana , hadi leo najiona mwenye makosa sana sababu mke wa jamaa alikua ananipenda sana na kuniheshimu bila kujua tunashare. Ila jamaa hakutaka kuniacha, alinipenda sana ila ilikua kwa siri sana sababu ni mheshimiwa pia, hivyo hata dating zetu ilikua tunasafiri kwenda mkoa mwingine ama hata kenya au nchi nyingine kwa ajili ya privacy. (alikua mtu wa kusafiri sana hivyo tulisafiri pamoja), hata sasa hivi bado yuko na mkewe na watoto family iko poa ila mkewe HAJAWAHI KUJUA HILI HADI LEO.


Nikawa kwenye uhusiano na mtu mwingine , huyu tulianza relationship kitambo pia, alikua hajaoa, funny thing ni hadi akanitambulisha kwa demu wake kama rafiki, girlfriend akaamini , hivyo hata akinikuta natumia gari la jamaa anajua ni shemeji, akikuta nimelala ndani ya nyumba anajua ni shemeji tu hadi harusi nilishiriki pale mlimani city sababu jamaa alitaka lazima niwepo, na kabla ya harusi yani siku moja kabla, alikuja kwangu tukasex kama kuniaga na kesho yake akafunga ndoa, hata alipooa japo tulikubaliana kuachana ila hatukuachana, hadi sasa ni happy family ila mke wake HAJAWAHI KUJUA.

Story ni nyingi ila wacha niishie hizo sababu zingine zitareveal kirahisi ID yangu maybe na za hao watu na nisingependa iwe hivyo, ila walioko kwenye ndoa wengi ni bisexual hasa hizi modern marriages. Watu sasa hivi wanaoa sababu tu jamii inataka waoe thats why hali ni mbaya, hata mimi mother akinipush sana nioe nitaoa , na cycle itaendelea like that, wapo vijana na watu wazima wengi ni gays ila huezi jua hata siku moja, kuna mtu tulikutana tu kwenye dating site moja ya huko nnje sababu hutumia zaidi dating site za kulipia kwa ajili ya privacy, siku tunakutana kwa mala ya kwanza sikuamini kama ni yeye, ni mtu maarufu sana na anaeheshimika sana ( ni kijana ) huko siasani. Pia mwingine huko kwenye music industry na nyimbo zake zinapendwa sana , ni za maadili.

Nataka kusema kua tatizo lipo more than you can imagine na sio rahisi kumjua mtu, hivyo kuliko kunyooshea vidole tu bila solution , ni vyema kuangalia ni kwa namna gani mtu anaweza kuzuia yasitokee kwake na kwa nwingine.

(2) Kuna watu hutongozwa na hawa gays kwenye mitandao, wala usijione unamkosi au labda umefanana na gays, hapana wewe ni straight. Kuna watu hulalamika kua ametongozwa na gay facebook au kwenye social medias, ukimuangalia huyo mtu utagundua kua ni very handsome na attractive , na gays wengi hudate na watu attractive zaidi , huwa hawafuati watu ambao wana sura personal, ndio sababu msione hao wanaotongozwa na gays huko labda wananyota mbaya au nao wanaonekana gays , hapana ila ni sababu wako attractive, tena gays wanapenda watu ambao sio gays, yani hata mimi watu niliodate nao naweza sema ni straight. Hivyo kama wewe ni handsome expect tu siku moja inaweza kukutokea na isikufanye uwaze sana na ujishushe thamani, mwambie tu im not gay then block that person. Hivyo wenye vijana ambao ni handsome wako attractive, msihisi kua labda vijana wenu ni gays hapana, ila tu nuombe Mungu awaepushe kufuatwa na gay, sababu ninachoweza kusema gays ni watu ambao wako na ushawishi mkubwa sana, unawesa hata kusex nae na mkimaliza ndio ukajiuliza imekuaje hadi ukafanya vile na unakua umechelewa tayari.

(3) Wanaume wengi ni curious, yani wameumbwa kutaka kujaribu vitu, hivyo imekua rahisi sana kushawishika, hata hawa ambao wako humu wanaongea kwa hasira na kufoka kuhusu gays tena hao ndio rahisi sana kuwashawishi, hasa wanaokunywa pombe, nina mshikaji wangu mmoja ambae ni gay, humuogopa sana sababu ana huo ujasiri wakutongoza atraight na wanaingia box, alishawahi kumtongoza straight guy akiwa na demu wake, jamaa alishindwa amfanye nini , girlfriend wake akacheka sanaaa wakaondoka. Ila hakukata tamaa na alimpata jamaa one day baada ya miezi mingi, hadi leo najiuliza sana.

La mwisho ni hili, watu mnapinga sana haya mambo ya NGO's za kusaidiwa hawa gays, ila hilo jambo lina faida sana hamjui tu, sio kwao tu kwa kila mmoja wenu, hata wewe straight ambae hauna mtoto gay, sababu hili jambo ni mzunguko. Gays ni watu ambao wako kwenye risk kubwa ya kupata maambukizi mbalimbali hasa HIV, Especially kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha , Hizo NGO's zinasaidia kuwapa elimu na kuwapa dawa mbalimbali za kuzuia wasipatwe na magonjwa au kuambukizwa magonjwa , inawapa huduma muhimu hata kama wanaumwa ili kuzuia wasiambukize wengine, na hii ni muhimu sana, sababu hili la magonjwa linakuja kukuathili hadi wewe straight huko ambae hata huhusiki,.mzunguko uko hivi👇

gay na gay wanasex, mmoja anamshawishi wasitumie condom, bila kujua anamuambikiza mwenzake let say HIV, huyo mmoja anaenda tena kusex na mwingine, anamuambukiza pia, huyo mwingine ni straight ila curious , anenda kusex na gay anaambukizwa, nae anaenda kumuambukiza girlfriend wake, ambae huyo girlfriend ana mchepuko pia ambae ni mume wa mtu, nae anaambukizwa , nae anaenda kumuambukiza mke wake nyumbani, hatimae unafikiwa.
Au huyo gay alieambukizwa, anamshawishi kijana wako (vijana wengi straight wanashawishika kirahisi sababu ya kutaka kujaribu kuona inakuaje), kijana wako anasex nae anaambukizwa, nae anamuambikiza girlfriend wake na cycle inaendelea, ni hatari kwa taifa.

Serikali ruhusuni hizo NGO's kuokoa taifa, nawaambia ukweli gays wako wengi sana , na wale ambao ni uneducated au wanaojiuza wengi wanamagonjwa na hawapati msaada hata huko hospitali za kawaida, huko Kenya wameruhusu NGO's na zinasaidia sana , wako mpaka na special hospitals , psychologists ambao wanawasaidia pia kuishi normal na wale ambao wameshawishiwa kujaribu kuwafanya waache. NGO's haziko kwa ajili ya kuwamotivate , hapana, ziko kwa ajili ya kuzuia usambaaji wa magonjwa.

Naomba niishie hapa , kama kuna swali lolote uliza kwenye comment nitakujibu, tupo kujifunza na kusaidia kupunguza hili jambo, hivyo tafadhari tusitumie kugha za kuuudhi sana na nimejaribu kuelezea kidogo ili mpate kujua naongelea nini. Karibuni.
Kuna waliwahi kuingilia wakiwa wadogo sana kiasi cha kutokukumbuka. Nakumbuka mtoto mdogo wa miaka mitatu alikuwa anamshikashika baba au mtu mwanaume sehemu ya kiume, hiyoo ni dalili ya mtoto kuingiliwa. Inawezekana huyo aliwahi kuingiliwa bila yeye kukumbuka. Imethibitisha kwamba gay anayegay kwa kudra za Mungu. Kama livyosema malezi na kuwalinda watoto vizuri kunachangia sasa.
 
Back
Top Bottom