Niliuona huu uzi tangu siku ya kwanza nikaupotezea, mambo ya mashoga yananichefua sana halafu niliamini ungefutwa na JF haraka sana.
Kilichonishtua hadi jana asubuhi uzi bado upo na una comments zaidi ya 400 in less than 24hrs. Nikafungua na kuanza kusoma pamoja na comments ZOTE hadi ukurasa wa 47.
Niliyoyagundua;
1.Mleta mada ni mtu SMART sana, ukiangalia uandishi wake, jinsi anavyojibu comments za watu hata zile za kudhihaki bila kupaniki wala ku attack back, professional yake, utakubaliana na Mimi. Actually by default mashoga wengi ni watu smart. Technologies nyingi tunazotumia ikiwemo computer ziligunduliwa na mashoga.
2. Watanzania/ waafrika wengi ni wanafiki hasa linapokuja suala la ushoga. Mwanzoni mwa uzi watu walikuwa wanachangia kupitia side ID's. Unakuta ID ya 2012 lakini ina comments 200au300. Uzi ulipochanganya ndipo zikaanza kuonekana zile ID's kongwe& popular.
3. Ushoga upo kila mahali. Angalia mleta mada anasema ni muumini wa dini anahudhuria ibada lakini anayoyafanya chini ya kapeti ni siri yake. Je ni watu wangapi wanaofanya hivyo? Si ajabu hata viongozi wa dini wanasimama madhabahuni kuulani ushoga lakini wenyewe ndio wanajua wanayoyafanya vyumbani mwao.
4. Wanawake wanaongoza kwa double standard. Ushoga baina ya wanawake literally unakubalika(na ndio upo kwa kiasi kikubwa) lakini kwa wanaume ni haramu. Mara nyingi club nimekuta wanawake wanacheza pamoja, ole wao wanaume wafanye hivyo. So hata ushoga kwa wanaume unapigwa vita kuliko sababu una disarm wanawake wanaotumia sex ku manipulate wanaume, unawapa competition wasiyoiweza.
5. Siyo kweli kwamba uwazi kwenye ushoga utahamasisha vitendo vya kishoga. Sigara na pombe vipo wazi mitaani na vinapewa promo na vyombo vya habari lakini kuna watu wengi hawavitumii na hawana mpango wa kuvitumia. Ukihisi utakuwa shoga kisa mwingine kajitangaza ni shoga ujue wewe ni shoga wa mafichoni.
Mkuu
Bharka kamwe usijihisi mdhambi au mpungufu kwa hali uliyonayo. Kama ndicho kinachokufurahisha wewe pamoja na wenzio kifanye with full Watts. Kama ni dhambi Mungu ndiye wa kukuhukumu na siyo binadamu. Bila shaka una la kujitetea mbele zake kama siku ya hukumu itakuwepo.
Mwisho nawapongeza
JamiiForums kwa kuruhusu maoni na mitazamo tofauti ijadiliwe, bila kuzuia watu kama mleta mada kujieleza.
JF WHERE WE DARE TO TALK OPENLY.