Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Dah leo Babu Loliondo kutokana na foleni kuwa kubwa ikabidi awaambie watu wapange foleni tofauti ya UKIMWI kushoto na kisukari kulia. Unaambiwa mstari ule wa kushoto (Wa ukimwi) haukuwa na mtu hata mmoja, babu akafurahi kuwa waathirika wamepungua sasa akawa anataka kumwaga ile dawa ya ukimwi! Duh watu wakaanza kupiga kelele "hhaaaa babu usimwage bwana, huwezi jua babu acha bwana tuko hapa leo siku ya tano babu" ikabidi babu ashangae vipi tena!
 
Mh! Hii kali coz kila mtu anaeenda kule anasingizia kisukari
 
Sifungamani na upande wowote! Anayeweza kumuepushia kiumbe taabu,mateso,maradhi n.k ni Mungu pekee. Dawa tutumiazo pamoja na njia nyingine kadha wa kadha ni sababu tu! Na ndio maana wapo wanaokunywa dawa na wakapona na wapo wanaokunywa dawa na wasipone!

Tujiulize uwezo Babu alionao umetoka wapi? Bila shaka ni Mungu ndio chanzo cha uwezo huo. Basi tuishi kwa imani, Mungu ni mkubwa!
 
mchokozi wewe.....umenifurahisha sana....:washing:
 

good food for thought mpendwa. keep it up

Glory to God
 
Sijaelewa. Babu anatibu UMAK (Ukosefu wa Makombe Klabuni)?
 
nice joke but amwage dawa ipi? Kuna aina ngapi za dozi pale?
 
Wana JF kuhusu tiba ya Loliondo na kauli tata kutoka makanisa ya kiroho msimamo wangu ndiyo huu,

  1. Kama babu ni roho itokayo kuzimu, nchi hii tuna mitume na manabii wengi kwa nini wasiombe Mungu wao akawajulisha kuhusu ukweli wa mchungaji mstaafu huyo badala ya kutoa hoja zisizo na mashiko. Mbona Kakobe alishawahi kusema kuwa Mrema ni chaguo la Mungu anashindwa nini kuomba Mungu ampe maono juu ya tiba hiyo kisha akawatangazia umma ili kutoa nusra kwa watu wanaokwenda kupata tiba. Kushindwa kuweka maono hii ni ishara ya kushindwa na kuanza kuona wivu wa kihuduma!
  2. Kama babu angejuwa tapeli asingekubali ku - charge Tshs 500.00 kwani roho ya kitapeli hujali mali, sifa na umimi kuliko hofu ya Mungu. Pia watu wasingekwenda kule ambako barabara na miundo mbinu ni mibovu kuliko maelezo, kisha uniambie watu wengi wawe wajinga kukubali shida na taabu bila mafanikio.
  3. Kutokana na hilo, upo uwezekano mkubwa wa kuchakachua huduma ile kwa kupanda mamluki kibao ambao watajifanya wanatoa huduma inayofanana na hiyo lakini mwisho wa yote kweli itajitenga.
  4. Mwisho, basi hao wachungaji wanaomuombea mabaya mchungaji Mungu wao hasikii, iwaje jambo nyeti kama hili ashindwe kuwajibu hali ya kuwa watu wanaendelea kupotea kwa mujibu wa mitazamo yao.
Ukisikiliza ushuhuda toka kwa watu waliotoka Loliondo ni lazima uwepo wa Mungu utakuwepo kule.
 
Inaonekana hakuna mtu aliye na ukweli juu ya tiba ya loliondo ila ni Mungu peke yake. Naomba tusitishe mjadala huu tujadili mambo mengine. Hii ni kwa sababu imefika hatua ya wengine kuwarushia wengine matusi badala ya kujibu hoja! Tumwachie Mungu atoweka wazi ukweli! Days will tell the truth. Mbarikiwe.
 
Adha ya maradhi ajuwaye ni mgonjwa. Tusikurupuke kulaumu na kukandia kwa kusukumwa na kiburi kinacholetwa na kuwa na afya njema. Taratibu jamani..taratibu.
 
Uchambuzi wako umekaa kimaslahi zaidi just like those statements from Pengo et al.

Mbona Yesu alitumia tope kumponya kipofu?Kwanini asingesema tu mimi ni Yesu,nakuamuru upate kuona?
Tatizo ni kwamba unataka ukishawahudumia watu basi na kanisa uanzishe kimaslahi,hao maaskofu wanhofu tu kuhusu congregations zao na si eti kwamba miujiza yenye Yesu haitumii vitu!

Biblia inasema kila mtu atakula kwa jasho lake,jasho la babu ni lipi?

Hata mara nyingine watu wakipitia mambo magumu ie magonjwa yanayohitaji upasuaji,halafu upasuaji huo ukawa wa mafanikio,basi huchukuliwa kama ni muujiza kwa muumini aliyefanyiwa upasuaji huo....Kuna wanaomeza dawa wakipona wanamshukuru Mungu na Yesu kwa muujiza wa uponyaji.

Tuachane na maslahi kwenye issue za kiimani.
 

nawahurumia watu wengi sana wanapotea kwa kukosa maarifa!

ooh, God have mercy on your people!
 

jibu liko kwenye maneno ya Mungu mpendwa. acha uvivu, kasome utaelewa. achana na watu wanaoongea kw ahisia bila ufahamu. ni neno la Mungu pekee litakalokuondolea wasiwasi. imani bila neno la Mungu si imani ya kumpendeza Mungu kwani waabudu halisi watamwabudu katika roho na kweli. zingatia kuwa kweli ni neno la Mungu, basi hakuna zaidi. si miujiza wala ndoto, ni NENO LA MUNGU.

ubarikiwe sana

Glory to God
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…