Nimefuatilia kwa muda mrefu juu ya "tiba-miujiza" inayotolewa na Babu wa loliondo.Kwa wengi wanaomuunga mkono ni sabab "wanajihisi?" wameponywa na dawa hiyo kimuujiza,na wanaompinga n kutokana na asili/chanzo cha dawa hiyo.
Dawa ya babu ikipimwa kwa vigezo vya kibiblia inapwaya ndio maana wa kina kakobe,pengo,mwingra wanapinga dawa hiyo.Kwa wakristo kigezo cha muujiza wowote kutokea(kuonekana) uwe wa kupona au la si kigezo pekee/cha muhimu kujua nguv za miujiza asili yake ni Yesu,kwa kuwa hata shetan,nabii wa uongo ana ishara tena kubwa ambazo zinaweza kuwadanganya hata wateule(wakristo wa kweli)-soma Matayo 24:24, ufunuo 13:13
Biblia imeturuhus kupima nguv (roho) zinazofanya kaz kwa watu kama Babu-1 yoh 4:1,3.
Babu alijinadi kuwa ametumwa na Mungu(Yesu) na kibiblia muujiza,uponyaji,vinafanyika kwa mamlaka ya Jina la Yesu- Matendo ya mitume 3:6,filip 2:9.
Kutumia vitu ktk uponyaj kibiblia sio lazima, bali n sharti vifanywe ktk jina la Yesu maana ndilo lenye mamlaka.
HIVYO MUUJIZA WOWOTE WAWEZA KUTOKEA KWA JINA LA YESU BILA YA KUTUMIA MAJI-matendo 3:6.
Je Babu kama kweli ametumwa na Yesu anaweza kutumia jina la Yesu pekee(pasipo maji) na watu wakpata uzima?
Muujiza wa Yesu ni kwaajili ya kuwaonya watu,kuwafungua,na kuwafundisha wasitende dhambi tena-wamgeukie Yesu sio warudi makwao kama wametoka 'theatre' bila kutubu-Yohana 5:14
Tena,muujiza wa Mungu ni lazma umtukuze Yesu na sio Babu wa loliondo-matendo 3:9 ,luka 5:26,13:13
Muujiza wa Muungu hauuzwi hata kwa shiling 1-kwani mmepewa bure toen bure-kwanin babu auze?
Babu anatakiw kujib hoja kibiblia kama kweli yeye katumwa na Yesu kweli-2petro 3:15 Tuwen macho hiz n cku za mwisho.