Mambo ya Ndoa: Mkiwa na Amani inakuwa raha sana kwa kweli, Ishu ni kui-maintain hiyo Amani

uran

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
19,101
Reaction score
31,995
Asikuambie mtu kwenye ndoa kipindi cha Amani, huwa kimejawa na furaha na mshawasha wakutosha.

Hasa ukute umeoa/kuolewa na rafiki yako, mnapatana.

Unajikuta unatamani kuwa karibu na mke/mume wako wakati wote, unapata hamu yakumnunulia zawadi hata kutoka outing za hapa na pale.

Ndugu zangu nimejichunguza sana, kipindi nina amani na mke wangu! Hata kuchelewa nyumbani haipo kama yupo. Najikuta natamani kumaliza mambo yangu haraka as atafanya whatever I need.

Tukiwa na amani atanifanyia chochote anachojua kitanifurahisha, na ninaamini iko hivyo kwa wanandoa wengi.

Changamoto inakuja kwenye kuhold on hiyo Amani, sisi ikitembea sana ni wiki tatu yaani hapo imedumu kweli kweli. Nimalize wiki tatu mfululizo! Haipo hiyo, sijui kwanini. Kitatokea tu kitu.

Yaani kuna wakati tunapatana kinoma, ile sana hadi nasema hatuwezi gombana sisi, halafu gafla tu kinatokea kitu. Napigwa mnuno!

Na itategemea situation unaweza kudumu hata siku mbili, mnasemeshana lakini ile kawaida tu, mambo mengine anafanya kwasababu ni wajibu wake tu.

Niliwahi kujitahidi na kuwa makini ili ugomvi wowote usitokee walau ndani ya mwezi mmoja nikajifunza kusoma hisia zake kwa umakini, lakini waapi.

Hii Amani ya kwenye ndoa kwako inadumu kwa muda gani?
 
Mnaweza kuwa kwenye peak ya furaha ila ukajikuta umeulizwa swali la kijinga tu na majibu yako yakaharibu kila kitu...

Sijui wanawake wengine hawajiamini au vipi.
 
Sio ndoa hata huku kwenye uchumba mambo hayo hayo mpk unatamani kuwaambia upande wa mwanaume waje kufata mahari yao…!!
Mara nyingi nyie ndio huwa mnavuruga mambo aisee.

Unaweza kuuliza swali ambalo mimi nitaliona la kijinga kumbe wewe uko serious 🤣.
Mfano; mbona Mbappe hafungi?
Hapo natakiwa nikujibu vipi ili usikasirike?
 
Asikuambie mtu kwenye ndoa kipindi cha Amani, huwa kimejawa na furaha na mshawasha wakutosha.

Hasa ukute umeoa/kuolewa na rafiki yako, mnapatana.

Unajikuta unatamani kuwa karibu na mke/mume wako wakati wote, unapata hamu yakumnunulia zawadi hata kutoka outing za hapa na pale.

Ndugu zangu nimejichunguza sana, kipindi nina amani na mke wangu! Hata kuchelewa nyumbani haipo kama yupo. Najikuta natamani kumaliza mambo yangu haraka as atafanya whatever I need.

Tukiwa na amani atanifanyia chochote anachojua kitanifurahisha, na ninaamini iko hivyo kwa wanandoa wengi.

Changamoto inakuja kwenye kuhold on hiyo Amani, sisi ikitembea sana ni wiki tatu yaani hapo imedumu kweli kweli. Nimalize wiki tatu mfululizo! Haipo hiyo, sijui kwanini. Kitatokea tu kitu.

Yaani kuna wakati tunapatana kinoma, ile sana hadi nasema hatuwezi gombana sisi, halafu gafla tu kinatokea kitu. Napigwa mnuno!

Na itategemea situation unaweza kudumu hata siku mbili, mnasemeshana lakini ile kawaida tu, mambo mengine anafanya kwasababu ni wajibu wake tu.

Niliwahi kujitahidi na kuwa makini ili ugomvi wowote usitokee walau ndani ya mwezi mmoja nikajifunza kusoma hisia zake kwa umakini, lakini waapi.

Hii Amani ya kwenye ndoa kwako inadumu kwa muda gani?
Unajikuta unaongea mwenyewe tu
 
Back
Top Bottom