Mambo ya Ndoa: Mkiwa na Amani inakuwa raha sana kwa kweli, Ishu ni kui-maintain hiyo Amani

Mambo ya Ndoa: Mkiwa na Amani inakuwa raha sana kwa kweli, Ishu ni kui-maintain hiyo Amani

Nimemiss minuno ya mke wangu sometimes kununa kunanogesha mahusiano unaishi na mtu hata umfanyeje hakufuatilii wala hanuni
 
Kwasasa niko na Amani na wife bana, ishu haitakaa sana aisee.
Tukikaa hivi naenjoy kinoma!!

Hakuna mchepuko wakunitoa hapa 😃😃
Na hatimaye Amani imefikia ukingoni leo.
Ni mnuno sasa, I wish it won't last longer.
 
Nimemiss minuno ya mke wangu sometimes kununa kunanogesha mahusiano unaishi na mtu hata umfanyeje hakufuatilii wala hanuni
Kama hanuni kwako, kuna mahali ananuna
 
Asikuambie mtu kwenye ndoa kipindi cha Amani, huwa kimejawa na furaha na mshawasha wakutosha.

Hasa ukute umeoa/kuolewa na rafiki yako, mnapatana.

Unajikuta unatamani kuwa karibu na mke/mume wako wakati wote, unapata hamu yakumnunulia zawadi hata kutoka outing za hapa na pale.

Ndugu zangu nimejichunguza sana, kipindi nina amani na mke wangu! Hata kuchelewa nyumbani haipo kama yupo. Najikuta natamani kumaliza mambo yangu haraka as atafanya whatever I need.

Tukiwa na amani atanifanyia chochote anachojua kitanifurahisha, na ninaamini iko hivyo kwa wanandoa wengi.

Changamoto inakuja kwenye kuhold on hiyo Amani, sisi ikitembea sana ni wiki tatu yaani hapo imedumu kweli kweli. Nimalize wiki tatu mfululizo! Haipo hiyo, sijui kwanini. Kitatokea tu kitu.

Yaani kuna wakati tunapatana kinoma, ile sana hadi nasema hatuwezi gombana sisi, halafu gafla tu kinatokea kitu. Napigwa mnuno!

Na itategemea situation unaweza kudumu hata siku mbili, mnasemeshana lakini ile kawaida tu, mambo mengine anafanya kwasababu ni wajibu wake tu.

Niliwahi kujitahidi na kuwa makini ili ugomvi wowote usitokee walau ndani ya mwezi mmoja nikajifunza kusoma hisia zake kwa umakini, lakini waapi.

Hii Amani ya kwenye ndoa kwako inadumu kwa muda gani?
Pole Sana mkuu
 
Aliyeleta mapenzi Sina ham nae Bora naangalia mpira kwa Sasa🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom