Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Hii nchi ina sinema nyingi sana...
Ndio maana tunashika nafasi ya pili Afrika kwa kuzalisha filamu kwa wingi. Nigeria wanaongoza. Lakini kwa hali hii tunaweza kuwapiku muda si mrefu. Tatizo la filamu zetu ni ubora.
 
Haifiki ijumaa atapangiwa kazj nyingine believe me.
 
undefinedasije tu kwenda kuwa constable kule Nanyumbu...undefinedIla kafanya vizuri kunawa mikono
Pamoja na jibu alilotoa halitampendeza malaika, ila kafanya jambo jema kujitoa
 
Hata kama Anasingiziwa Achutame tuuu....!?, huyo anaekosea-kosea kwa kuto shaurika atajuaje kama anakosea?.ama ye ni Malaika Mweusi aishie juu ya ubinadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jiwe ndio tatizo kwa kutaka kick public. Huu ni udhibitisho vyombo vya kimamlaka huwa haviwajibiki kwa umma bali kwa rais kwenye maagizo toka juu. Hayo rais aliyomuambia Mambosasa huwa tunahoji humu jukwaani kila siku lakini hamna majibu zaidi ya ubabaishaji. Leo rais kahoji ndio mambo sasa anaona ni wakati wa kujibu.
 
Mambosasa angekaa kimya tu,wenye akili zetu,tunajua hapa anatafutwa MTU wa kutolewa kafara,
Haiwezekani,ishu ya Mo,IGP asijue,DCI asijue,TISS wasijue,na wote wana ripoti kwa Mkulu,
Hii ni kama Ishu ya kikokotozi cha mafao,upuuzi ulifanywa na Waziri,Mkurugenzi wa SSRA akatolewa kafara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa muda nilivaa viatu vya rais halafu nikawa nasoma alichonijibu, nikajikuta napandwa na hasira kali, nikachukua simu nimpigie igp ili ampeleke akawe analinda magodown, ndipo nikagundua mimi si rais na hata namba ya igp sina, dah!

Rais si Mungu.
 
Lile picha walilocheza wakimuhusisha dreva teksi la kishamba sana. Yaani limewaacha uchi kabisa na kituko mbele ya jamii.
Kwa sasa ni afadhali wanyamaze tu maana watu washamwachia Mungu.
Wakijaribu kuleta muvi nyingine maana naona mkuu wa kaya keshaichomekea wataumbuka zaidi na kutonesha kidonda ambacho kishageuka kovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikujua kama jpm ni muigizaji mzuri kiasi hiki!
 
Kumbe rais ndiye anatuona watanzania ni wajinga. IGP anayempa maagizo ya kuwashughulikia maRPC wazembe kama Mambosasa ndiye aliyekalia taarifa. Shubamiti!
 
Mambosasa hawezi kutumbuliwa kwani anaijua picha yote na wakizidi kumprovoke ataharibu kila kitu kuhusu scandal name huenda akawataja wahusika ili kama mbwai na iwe!
Nami namtia moyo kuwa usikubali kulibeba peke yako na ikibidi itisha press ujisafishe!
Nyakati nyingine, ninyi watu wazima mliobakisha miaka miwili au mitano kustaafu mbona kama akili zenu mnaziachaga home wakati wa kwenda kazini? Mnakubalije kufanya dili na watoto wadogo?
 
Sasa akikaa kimya si ndio lawama zitamwangukia??
Jiwe anajua kila kitu ila anapangua kishamba.
 
Serikali za kinafiki ndio watendaji wake wanabeba lawama za wakubwa.
Sasa wewe ulitaka Polisi ichukue lawama wakati tatizo sio lao??
Huu unafiki hautatui matatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…