Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Jamani tuandae Passport mapema maana muda wowote waanza saka 1 1 kama alivyosema Mange
 
Huu ulikuwa utabiri wa 2013
Binti wa zamani
 
Mkuu,
Nakumbuka sana, tulienda huko Kenya talk kabisa. Ila jf haikufungiwa, hakukuwa na official statement ya kufungia mtandao.
Basi ndio kama hivyo mkuu kipindi kile na hiki tofauti yao ni jinsia ila mambo ni yale yale.
Leo tumeambiwa mtandao utafungwa na leseni kusitishwa kwa 90days, wewe tofauti huioni kweli?
Na it was predicted kwani hujui ile story ya watu wanaotakiwa kuripoti habari za uchaguzi walitakiwa wajisajili hivi inaingia akilini ?
 
Waungwana mimi kidogo kwenye masuala ya teknolojia ni mweupe.....hivi wakifungia wanamaanisha kwamba hata uwe na VPN huipati au ni mwendo wa VPN kama kule X...??
 
Mkuu,
Nakumbuka sana, tulienda huko Kenya talk kabisa. Ila jf haikufungiwa, hakukuwa na official statement ya kufungia mtandao.

Leo tumeambiwa mtandao utafungwa na leseni kusitishwa kwa 90days, wewe tofauti huioni kweli?
Ni yale yale tu
 
Mambo ya ajabu kuwahi kutokea , tukilaumu ya the late president ila this is too much , uamuzi wa kufungiwa umechukuliwa haraka sana , sidhani hata kama mkurugenzi aliitwa kuoneshwa makosa yake , zaidi post zile wanajibizana na msemaji mkuu
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
The cartel
 
Tumuombe Allah (S.A.T) nusu ya miaka mitano awe akhera.
 
Tulisema taifa limeshakuwa la kipuuzi. Na whoever anaejaribu kuwa real wanamrafutia HILA. JF ILIweza kudumu kipindi cha NGOSHA seuze haya maigizo
 
Back
Top Bottom