Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Tulisema taifa limeshakuwa la kipuuzi. Na whoever anaejaribu kuwa real wanamrafutia HILA. JF ILIweza kudumu kipindi cha NGOSHA seuze haya maigizo
Sasa kama Watanzania wenyewe ndio ma keybord worrior kama sis unategemea nini?
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
Kwa hiyo tunatudi tena Kenya!!
Kama ilivyokuwa 2020?
 
Watufunge na sisi wananchi wote sasa wabaki wao na familia zao waendelee kufaidi.
 
Jukwaa lilipotea kwa siku 21 watu wakahamia Kenya talk.

VPN zimeanza kutumika 2020 baada ya influence ya kigogo kule Twitter kuanzia siku ya uchaguzi mitandao yote ilikuwa geo blocked hadi November 3 watu mlishasahau aliyeanzisha haya mambo?
Tofauti na kufungia lakini alikofanya huyu wasasa

Miezi 3, alafu anataka kula zetu eeh hiyo Oktoba 🙌
 
Back
Top Bottom