Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Naunga mkono hoja, haiwezekani jukwaa litumike Kwa maslahi ya vikundi au watu badala ya Umma.

Pole sana ila sheria zifuatwe.

Nawashauri TCRA wangefungia jukwaa la siasa na mengine ambayo yanaandika siasa ,then Yale mengine yasalie na wamiliki wadhibiti maudhui y Kisiasa kwenye majukwaa yasiyo ya siasa.
Acha upimbi nyie watu waoga sana, kwanini hamtaki kukosolewa?
 
Huku kulikuwa na Uhuru mkubwa sana wa kutoa maoni

Wale watumiaji wa mitandao mingine ya kijamii, chukueni tahadhali huko X, Instagram ama Facebook

Huu utawala wa sasa, sioni ukivumilia maoni mbadala
Ni hatari aisee,
 
Picha upige mwenyewe kwa utashi wako, halafu unakuja kuifungia sehemu inayotupunguzia msongo wa mawazo! Huu ujinga haukubaliki hata kidogo.

Nawahakikishia watawala; kamwe hamuwezi kuwalazimisha watu wenye akili timamu kuwapenda kupitia nguvu na vitisho. Njia pekee kwenu ni kukubali tu kubadilika.
 
Sheria za nchi lazima zifatwe.

Uhuru wa kujieleza na maoni kupitia vyombo vya habari vina mipaka yake, tuiheshimu.
Tueleze JF wamefanya kosa gani?
Mahakama gani imetafsiri sheria ipi imevunjwa?
Kuwapa TCRA mamlaka haya ni udhaifu wa sheria. Ilitakiwa wakosaji waburuzwe mahakamani wakajitetee na mawakili.
 
Uhuru wa vyombo vya habari lazima uheshimiwe mistake watu washindwe kufanya kazi zao kwa weledi kisa kulinda maslahi yenu.Mama na mwanao mnaofanya hivi mtaishia pabaya sana
 
Faida ya jf hawawez track account Yako ,pia huku wengi hatujuani.

Kajichanganye insta au fb wata deal na followers wako watano tu mbona unapatikana ndani ya nusu saa tu.
wanacho fanya kukutrack hata jf wanaweza ila nakupa hii mbinu.
1.Usikubari mtu kaingia DM katuma link ukafua ,ukifungua wamenasa IP yako ya kifaa na hata unapokwenda wanajua.
2.hakikisha unatumia kifaa ambacho mfano simu au laptop ina generate MAC address fake kuepuka kugunduliwa.
 
Back
Top Bottom