Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Screenshot_20250906-145924_Chrome.jpg
kenya talk hii hapa
 
Mbona mimi situmii VPN na hapa naipata?
Nilikuwa natafuta comment kama hii maana hata mie sina VPN (nikasema kulikoni au simu yangu ina VPN bila kujua)

Actually niliona post kwenye page yao ya Facebook nikasema niingie kujaribu na nikafanikiwa)
 
Wameteka wakoasiji wakawaumiza na wengine kuwaua wakaona haitoshi wakamuweka ndani mpinzani mkuu wa CCM katika uchaguzi huu Tundu Lissu wakaona haitoshi na sasa wanafungia mitandao ya kijamii Ili taifa liwe kimya kama liko msibani
Sasa ni wakati wako shujaa ujitokeze mitaani
 
Mkuu wewe ni mkongwe mwenzabgu humu umesahau migration ya watu kwenda Kenya Talk kwa waliokuwa Tanzania au hicho kipindi ulipumzika kuingia humu?

Issue sio barua , Melo alikuwa treated vibaya utawqla ule vingapi vilifanyika bila barua??

Ukiniuliza barua nami nitakuuliza 2020 wakati mitandao kama Twitter[X] , WhatsApp , Facebook, YouTube zimefungiwa kuanzia tarehe 28 October hadi November 3 ,2020 kuna barua mlipewa?

Hivi mtu si alivamia Clouds TV na footages zikatoka picha zake ni yeye je tulikuja kuambiwa vipi zaidi ya kusema alikuwa matembezi .

Tusiwe wasahaulifu mapema.
Mkuu,
Nakumbuka sana, tulienda huko Kenya talk kabisa. Ila jf haikufungiwa, hakukuwa na official statement ya kufungia mtandao.

Leo tumeambiwa mtandao utafungwa na leseni kusitishwa kwa 90days, wewe tofauti huioni kweli?
 
Ndiyo wakati ule tunatumia VPN?

Wanataka Kufunga maoni mbadala Nchi nzima 🙌
Jukwaa lilipotea kwa siku 21 watu wakahamia Kenya talk.

VPN zimeanza kutumika 2020 baada ya influence ya kigogo kule Twitter kuanzia siku ya uchaguzi mitandao yote ilikuwa geo blocked hadi November 3 watu mlishasahau aliyeanzisha haya mambo?
 
Back
Top Bottom