Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Dah! Weshafanya yao, sawa yanamwisho haya.
2995.jpg
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
Mtaifungia JF lakini hamtaifungia mioyo ya wana JF.....
 
Yaani waendeleze ufisadi na kuonesha mahusiano ya ajabu na fisadi halafu wanahamaki nini sasa. Hakuna kinafanyika gizani kiovu kwa maslahi ya Tanzania hakitajulikana.
 
Kama wanapendwa na wananchi asilimia kubwa,

Kama wana wanachama milioni 13,

Kama wameleteta maendeleo makubwa na serikali ya Idd Amini Dada haidawi kitu mbona wanatumia nguvu kubwa kupapambana na hoja za wananchi?
 
Kwani picha za huyo mfanyabiashara zilipigwa na JF.
Jamii forum haikuwepo siku hizo mbalimbali walipokuwa wanakutana ikulu.

Picha zimepigwa na mpiga picha wa Ikulu, zimewekwa mtandaoni na ikulu mawasiliano pia na Chivayo kwanini mzigo wanaangushiwa Jamiiforum?
 
Mzee wa kububujikwa na machozi atabubujikiwa chooni 😩
 
Back
Top Bottom