Yaani wivu tu!
kweli kabisa, hata Magu hakufanya hayaHii haijawahi kutokea !
JF ni media pekee iliyobaki na uhuru kwa kiasi. Nyingine zote zimetishiwa na kutishika. Nafikiri wanataka kufunga kazi wainyamazishe kama nyingine zote.Kabisa mkuu. Hawa wanalao jambo walikuwa wanatafuta sababu tu za kuifungia jf
Wamewaangushia tu, zile si picha zakupiga ndani ya ofisi za umma 🚮Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni
TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.
Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.
Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.
TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
Uzi umetembea speed ya 5G.Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni
TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.
Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.
Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.
TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
Labda upo nje ya nchiSina VPN. Labda katazo halijaanza.
Weee muhuni kumbe upo😁😁Sheria za nchi lazima zifatwe.
Uhuru wa kujieleza na maoni kupitia mvyombo vya habari vina mipaka yake, tuiheshimu.
Haya ndio ni maneno. Ni bora M7 kakubali yaishe.Mseveni anasema uganda kuna uhuru wa kuongea ila baada ya kuongea atashindwa kukuthibitishia uhuru wako
Sasa hapa umeingiaje?
Nipo sana .Akina Mwashambwa wapumnzike na uchawa wao....watuache wenyewe huku
JF ndio nyumbani kwangu.Aiseee! Yohana mbatizaji yumo humu au wamemkomoa?. Akina mwashambwa. Tiini mamlaka yenu, msing'ae humu within 90 day.