Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa 'drones' kuzisajili ndani ya siku 4

Hizi drone tunazotumia kwenye shooting zinahusika ama? Yani hii nchi kwa kweli
 
Nafikiri hii ndio sababu kubwa iliyowazindua kukazia hii sheria. Hata hivyo, ni sheria ambayo imekuwapo kitambo ila haikutiliwa mkazo, na kwa kweli haina ubaya hata nchi zilizoendelea kama Marekani wanasisitiza hili suala la registration (Kibali?) na requirements zao ni pana zaidi.
Register Your Drone
 
Hapo juu naona nyumbu wa upinzani wanaitukana serikali kwa kitu ambacho hawakijui vizuri. Hivi munakumbuka kuwa drone ilibeba vilipuzi na kutaka kumuua Madulo rais wa Venezuela?.
Ndio ujue wengi nyumbu kweli wengine hata wanachokibishia hawakijui ndio maana wanalinganisha drone na tiara, hivyo vitu viwili wapi na wapi? Binafsi nilikuwa sijui kama hazijasajiliwa nimestuka
 
Binafsi nimekuelewa hii comment yako mkuu,nadhani mamlaka husika wangetoa sababu kadhaa kwanini wanataka zisajiliwe kama ulivyoainisha hapa,huu mkanganyiko usingekuwepo
 
Nadhani drone ilitumika kubeba vilipuzi hata kwenye sherehe ya kijeshi kule Venezuela na Zimbabwe wakati wa kampeni za Munangagwa.

Huku kwetu, kuna mbwa wa jirani yetu waliuawa kwa sumu, tunadhani mtekelezaji alitumia kitu kama drone kubebea minofu ya kuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…