Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,795
- 48,057
leo toka saa nne Fb na whatsapp zinagoma.sijui ni Tcra
Mimi nina ka kishada kangu hapa ila kenyewe huwaga kanaogeleaga baharini,vipi nikikipeperusha angani kitakubarika?Drones zinatumia anga,
kisheria vyombo vyote vinavyotumia anga ku operate, vinakua chini yao.
hapa jf watu hubishana kwa mkumbo na mihemko ya kisiasa kwani ni nchi gani kwa sasa iliyoondelea watu wanatumia drone ovyo pasipo Regulations ?Mkuu una amini sana hadithi za vijiweni za wanasiasa uchwara.
Hii sheria ya udhibiti Remotely Piloted Aircrafts au Unmanned Aircraft Systems (UAS) kwa hapa Tanzania imetungwa kabla hata huyo haijulikani atarudi lini Tanzania na kugombea uraisi, kimataifa ipo tangu 1944 chini ya shirika la kusimamia usafiri wa anga (ICAO).
Hapa JF ulishapandishwa uzi wa kuelezea sheria hii tangu mwaka 2018 kurudi nyuma.
Nafahamu vizuri sana, nimefanya kazi kampuni ya kutengeneza drones kama engineer najua fika kuhusu drones na airline industry nzima kwa ujumla.Yawezekana hujui kazi hatari zinazoweza kufanyika na hizi drones
hapana mkuu. Serikali inafanya kazi yake. Vinatakiwa viwe monitored otherwise vinaweza vikaleta madhara vikirushwa ovyo ovyo. Anga ni mali ya serikali na lazima waangalie usalama pia. Drones zinafanya kazi nyingi sana siku hizi hata kubeba mabomu.
Mkuu punguza lugha kali.
Drone ni chombo hatari sana kama kikitumiwa bila utaratibu maalum au uangalizi.
Kumbuka yule Kamanda wa Iran aliuwawa na drone.
Kumbuka drone zilitumika kushambulia visima vya mafuta huko Saudi Arabia na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.
Drone zimetumika kushambulia na kufanya ujasusi katika matukio mbalimbali duniani, na kuna uwezekano mkubwa sana zikatumika kufanyia ughaidi.
Fikiria mtu akifunga kinyunyizi cha nerve gas au sumu yeyote akawadondoshea watu matone au punje chache kama kwenye kampeni au uwanja wa taifa, atauwa watu wangapi?
Fikiria mtu akifunga bomu (plastic bomb kama la C4) kwenye drone akaenda kugongesha jengo au kulitupa kwenye umati au sehemu nyeti atauwa watu wangapi?
Fikiria wakati huu wa kampeni za uchaguzi mtu akigongesha drone kwenye helicopter ya mgombea yeyote hakutatokea machafuko nchi hii kwamba ameuwawa na taasisi au watu flani?
Tuache matusi na kuona wataalam wetu ni wajinga au washenzi, washamba, siyo wasomi huku wewe ukijiona ndiyo unajua kuliko hao wataalam wengi waliosomea mambo ya usalama na anga.
Wewe usirudi TZ hakuna tunachopungukiwa kwa kutokuwepo kwako TZ. Unatupunguzia watu waliokosa hekima tu.
Asante sana mkuu.Wanataka mpaka patunguliwe pale ubungo gas station.Ndio waje na uchambuzi wao humu usio na kichwa wala miguu.Wengi mnaoshangazwa na hii taarifa mmeangalia upande mmoja tu wa shilingi.
Mnaichukulia drone kama toy au personal gadget, ila ukienda mbali drone inaweza kutumika kama silaha.
Mfano mdogo tu huu hapa.
Utajisikiaje jirani yako au mtu usiye mfahamu kuchungulia nyumbani kwako, au kuangalia chochote kilichopo ndani ya mipaka yako bila ruhusa yako?
Drone inaweza kufanya yafuatayo
1. Kubeba vilipuzi
2. Kupiga picha za siri
3. Kufanya uhalifu ( naweza kubeba chakula chenye sumu kwa drone na ku drop kwenye nyumba yenye mbwa wakali, kwa lengo la kudhoofisha ulinzi)
4. Drone inaweza kutumika kuharibu security cameras kwa lengo la kufanya uhalifu.
5.Drone inaweza kutumika kumfatilia mtu kwa lengo la kumdhuru au kumpora.
6.Drone inaweza kutumika kuharibu au kusababisha shoti kwenye power lines
Hayo ni machache ambayo drone ikitumiwa ndivyo sivyo inaweza kugharimu maisha ya watu, privacy na usalama kwa ujumla.
Hii ni process ya kawaida kabisa , drones zinachukua space angani na sometimes zinaweza kupaa umbalj wa juuHivi tunaelekea wapi jamani.
Taarifa za ndani zinasema lengo la kuamsha sheria hii n kudhibiti drone za ulinzi za kiongozi flani wa upinzni na pia kudhibiti drone zinazompiga picha kwa lengo la kudhibiti ulinzi na kudhibiti upigaji picha unaoonyesha nyomi.
Daah unazijua drones za kivita wewe?Hizo ni tofauti sana na hivi vitoy vya kupigia picha!Hebu kuweni serious na msitufanye wajinga!Nchi zilizoendelea kama marekani hizo drones vitoy zipo kama njugu na hazijawahi kuwa tstizo kama mnavyotaka kuaminisha watu!
Mmeona Lissu ana ulinzi na vifaa vya kuchukua matukio mmeanza kuja na upuuzi!
Yaani drone kitoy ikaangushe Boeing Kwa kugongesha?Uko timamu kweli?Umetoa mfano wa shambulio la Iran,hivi unajua size ya drones za marekani zilizoshambulia msafara ule?Au unajua ni drone kama hz za kufungia camera?Zile ni jet kabisa sema hazina rubani!Sasa wew unalinganisha na hivi vitoy vinavyotumia motor na betri[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]!!?
Mtu mpaka afikie hatua ya kushambulia kwa kutumia C4,basi hata drone yenyewe ni kiasi cha yeye kujifungia ndani na kutengeneza!ushamba tu unatusumbua!
Hahaha we jamaa una matatizo.
Drone iliyotumika kuua kamanda wa Iran unahisi ipo Tanzania? zile ni very advanced drones, kubwa balaa in size, mtu hawezi kua na drone ile Tanzania asijulikane, hawa wanachotaka ni kila mtu asajili drone hata wenye vi-toy vya kuchezea watoto vile unarusha dakika mbili kimeishiwa charge. Drone yenye uwezo wa kubeba kitu significant kama bomu ni size kubwa mno usidhani kitoy cha laki moja kinaweza fanya kazi hiyo.
Na we kwa akili yako unahisi mtu mwenye mpango wa kulipua bomu ataenda kuregister? atanunua drone atafanya anachotaka bomu litalipuka at the end of the day hadi mnakuja kufuatilia kujua haijawa registered the damage has already been done. Naona unachukulia poa sana technology. Wataalamu wetu ni wajinga ndiyo, wengi wao washamba haha it's obvious, nimekaa kwenye hii industry naijua vizuri, washamba bongo wamejaa tu wana PhD feki. Like it or not situation ndivyo ilivyo, kuishi kizamanizamani tu. Waste of time
Umekaa kwenye industry gani? Aviation, Security, ICT, au terrorism?Hahaha we jamaa una matatizo.
Drone iliyotumika kuua kamanda wa Iran unahisi ipo Tanzania? zile ni very advanced drones, kubwa balaa in size, mtu hawezi kua na drone ile Tanzania asijulikane, hawa wanachotaka ni kila mtu asajili drone hata wenye vi-toy vya kuchezea watoto vile unarusha dakika mbili kimeishiwa charge. Drone yenye uwezo wa kubeba kitu significant kama bomu ni size kubwa mno usidhani kitoy cha laki moja kinaweza fanya kazi hiyo.
Na we kwa akili yako unahisi mtu mwenye mpango wa kulipua bomu ataenda kuregister? atanunua drone atafanya anachotaka bomu litalipuka at the end of the day hadi mnakuja kufuatilia kujua haijawa registered the damage has already been done. Naona unachukulia poa sana technology. Wataalamu wetu ni wajinga ndiyo, wengi wao washamba haha it's obvious, nimekaa kwenye hii industry naijua vizuri, washamba bongo wamejaa tu wana PhD feki. Like it or not situation ndivyo ilivyo, kuishi kizamanizamani tu. Waste of time