Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa 'drones' kuzisajili ndani ya siku 4

Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa 'drones' kuzisajili ndani ya siku 4

Ni kweli mkuu, usajili utasaidia na kupunguza hayo madhara. Lakini pamoja na usajili, bado kuna uwezo wa drone kutumika kufanya yote hayo. Kwa mfano bunduki zinasajiliwa lakini watu wana fyatuliwa kila leo!! Ila kusajili ni Sawa!
Upo sahihi.
Pia jiulize buunduki zingeruhusiwa kumiliki kama panga hali ya watu kujeruhiana au kuuwana ingekuwaje?
Kwenye ugomvi mdogo wa bar au majirani mtu angewasha chuma cha moto.
 
Kazi nyingine ambayo haisemwi ni kuwa Drone inaweza kutumiwa kulinda kura kipindi hiki cha uchaguzi
 
Sheria ilikuwa inataka uwe na kibali, hii ya Sasa ni usajili...kwa hiyo hata ukiwa nazo tano kila moja iwe na usajili wake.

Halafu popote utapozitumia uombe kibali Polisi na serikali ya mtaa husika.

Wanataka kujua zinazopiga kwenye mikutano ya Lissu ni za nani.?
Kama ni za Lisu mwenyewe itakuwaje
 
Hapo juu naona nyumbu wa upinzani wanaitukana serikali kwa kitu ambacho hawakijui vizuri. Hivi munakumbuka kuwa drone ilibeba vilipuzi na kutaka kumuua Madulo rais wa Venezuela?
Why now???? Wasubiri baada ya uchaguzi
 
Taarifa za ndani zinasema lengo la kuamsha sheria hii n kudhibiti drone za ulinzi za kiongozi flani wa upinzni na pia kudhibiti drone zinazompiga picha kwa lengo la kudhibiti ulinzi na kudhibiti upigaji picha unaoonyesha nyomi.
 
Mkuu punguza lugha kali.
Drone ni chombo hatari sana kama kikitumiwa bila utaratibu maalum au uangalizi.
Kumbuka yule Kamanda wa Iran aliuwawa na drone.

Kumbuka drone zilitumika kushambulia visima vya mafuta huko Saudi Arabia na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.
Drone zimetumika kushambulia na kufanya ujasusi katika matukio mbalimbali duniani, na kuna uwezekano mkubwa sana zikatumika kufanyia ughaidi.

Fikiria mtu akifunga kinyunyizi cha nerve gas au sumu yeyote akawadondoshea watu matone au punje chache kama kwenye kampeni au uwanja wa taifa, atauwa watu wangapi?

Fikiria mtu akifunga bomu (plastic bomb kama la C4) kwenye drone akaenda kugongesha jengo au kulitupa kwenye umati au sehemu nyeti atauwa watu wangapi?

Fikiria wakati huu wa kampeni za uchaguzi mtu akigongesha drone kwenye helicopter ya mgombea yeyote hakutatokea machafuko nchi hii kwamba ameuwawa na taasisi au watu flani?

Tuache matusi na kuona wataalam wetu ni wajinga au washenzi, washamba, siyo wasomi huku wewe ukijiona ndiyo unajua kuliko hao wataalam wengi waliosomea mambo ya usalama na anga.

Wewe usirudi TZ hakuna tunachopungukiwa kwa kutokuwepo kwako TZ. Unatupunguzia watu waliokosa hekima tu.
Bongo kuna watu wajuaji wengi wenye vielimu vya ajabu ajabu tu wanasumbuaa sana utahangaika kuelimisha mbuzi kama hii iliyokalili kila kitu ni kupinga tu pasipo kufatilia kiundani ni ajabu sana
 
Taarifa za ndani zinasema lengo la kuamsha sheria hii n kudhibiti drone za ulinzi za kiongozi flani wa upinzni na pia kudhibiti drone zinazompiga picha kwa lengo la kudhibiti ulinzi na kudhibiti upigaji picha unaoonyesha nyomi.
Check hili jinga
 
Upo sahihi.
Pia jiulize buunduki zingeruhusiwa kumiliki kama panga hali ya watu kujeruhiana au kuuwana ingekuwaje?
Kwenye ugomvi mdogo wa bar au majirani mtu angewasha chuma cha moto.
Kuna mjadala mkubwa sana katika umiliki na matumizi ya silaa huko, USA! Udhibiti ni jambo la msingi, lakini kujenga kizazi chenye maadili mema ni muhimu sana. Katika mapambano ya kiuchumi, hasa uchumi wa kati, tunajikita sana kwenye kazi na kusahau majukumu ya msingi ya kifamilia. Kuna kizazi kinaibuka kisicho na maadili mema, ambapo kutumia silaa vibaya kwao ni kawaida!! Kwa hiyo kujenga familia imara ni muhimu sana, na ni jukumu letu sote.
 
Sasa unatukana nini? Kosa lao liko wapi?
Kwa nini hujalalamika kusajili laini ya simu ambayo unanunua kwa Tsh 2000?
Sembuse Drone yenye uwezo wa kuambaa free on peoples private houses?
Security sensitive equipment?
Ikisajiliwa itakosa uwezo wa kudukua na kuchungulia faragha za watu?

Kuna kitu gani cha pekee kitakachosaidia ili droni isifanye kazi iliyokusudiwa?
 
Drones zinatumia anga,
kisheria vyombo vyote vinavyotumia anga ku operate, vinakua chini yao.
Basi na wamiliki wa baiskel wasajili vyombo vyao maana kuna mamlaka ya vyombo vya usafiri majini na nchi kavu....N.B WAZO TUU
 
Unanunua Drone ndogo tu tsh 60k ya kujipiga selfie inabidi ukaisajili[emoji1787][emoji1787][emoji1787] aise[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sio huto tu duroni twenu twa hepi besidei hatuwezi kuruka mita 20 toka ulipo na remote control. Ni zile duroni zinaingia nchini kwa kibali ambapo huko nyuma zilikuwa hazisajiriwi
 
Kuna mijitu kubisha iko fasta hata kabla ya kutafakari.
Hakijui hata hicho kinachotakiwa kulipiwa kisheria anakurupuka na kuanza kubwabwaja.
 
Watu wanapotoka sana na hii taarifa, wanafikiri hizi drone vitoy vinatakiwa vikasajiriwe.

Sio hizo jamani, zipo drone special ambazo huwezi kuingiza nchi bila kibali na zinatukika kwa kazi maalumu.

Kama ni hizo toy zenu si mngeambiwa na toy zenu za ndege na helikopta mkasajiri?
 
Back
Top Bottom