Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa 'drones' kuzisajili ndani ya siku 4

leo toka saa nne Fb na whatsapp zinagoma.sijui ni Tcra
 
hapa jf watu hubishana kwa mkumbo na mihemko ya kisiasa kwani ni nchi gani kwa sasa iliyoondelea watu wanatumia drone ovyo pasipo Regulations ?
 
Yawezekana hujui kazi hatari zinazoweza kufanyika na hizi drones
Nafahamu vizuri sana, nimefanya kazi kampuni ya kutengeneza drones kama engineer najua fika kuhusu drones na airline industry nzima kwa ujumla.
Hii imetengenezwa ili kupiga hela tu hakuna kingine, nenda kufanya registration uone process ilivyo ndefu, utazungushwa kuchukua barua kwa sijui tako gani la mtaa. Ingeakua ni easy registration na maybe free au hadi 10,000 hata usingeona nalalamika. Nenda kafanye registration ulete mrejesho hapa usumbufu wake ulivyo. Tanzania kila kitu kinafanywa kiholela tu.
 
hapana mkuu. Serikali inafanya kazi yake. Vinatakiwa viwe monitored otherwise vinaweza vikaleta madhara vikirushwa ovyo ovyo. Anga ni mali ya serikali na lazima waangalie usalama pia. Drones zinafanya kazi nyingi sana siku hizi hata kubeba mabomu.

Kwa hiyo unadhani zikiwa registered basi unadhani mtu aliyepanga kutumia drone kubeba bomu naye atajipeleka kwenda kusajili? 😂 😂 atakua kilaza wa namna gani?
Registration ikiwa rahisi hata siwezi laumu, tatizo la registration za bongo unavyozungushwa na kupigwa hela.
 

Hahaha we jamaa una matatizo.
Drone iliyotumika kuua kamanda wa Iran unahisi ipo Tanzania? zile ni very advanced drones, kubwa balaa in size, mtu hawezi kua na drone ile Tanzania asijulikane, hawa wanachotaka ni kila mtu asajili drone hata wenye vi-toy vya kuchezea watoto vile unarusha dakika mbili kimeishiwa charge. Drone yenye uwezo wa kubeba kitu significant kama bomu ni size kubwa mno usidhani kitoy cha laki moja kinaweza fanya kazi hiyo.
Na we kwa akili yako unahisi mtu mwenye mpango wa kulipua bomu ataenda kuregister? atanunua drone atafanya anachotaka bomu litalipuka at the end of the day hadi mnakuja kufuatilia kujua haijawa registered the damage has already been done. Naona unachukulia poa sana technology. Wataalamu wetu ni wajinga ndiyo, wengi wao washamba haha it's obvious, nimekaa kwenye hii industry naijua vizuri, washamba bongo wamejaa tu wana PhD feki. Like it or not situation ndivyo ilivyo, kuishi kizamanizamani tu. Waste of time
 
Asante sana mkuu.Wanataka mpaka patunguliwe pale ubungo gas station.Ndio waje na uchambuzi wao humu usio na kichwa wala miguu.
Tujifunze kupinga kwa maarifa.
 
Hivi tunaelekea wapi jamani.
Hii ni process ya kawaida kabisa , drones zinachukua space angani na sometimes zinaweza kupaa umbalj wa juu
Kuzisajili kwa Sasa ni muhimu ili kujua idadi yake na wamiliki wake, zimekuwa nyingi kwa Sasa na huko mbele zinaweza kutumika kufanya uhalifu.
 
Taarifa za ndani zinasema lengo la kuamsha sheria hii n kudhibiti drone za ulinzi za kiongozi flani wa upinzni na pia kudhibiti drone zinazompiga picha kwa lengo la kudhibiti ulinzi na kudhibiti upigaji picha unaoonyesha nyomi.

Hivi hizi guts za kusema uwongo huwa mnazitoa wapi wenzetu??
 

Pathetic!!
 


Unatia kichefuchefu!!
 


Kite si ndio tiara?? Haki mnakera kuweka mikwamo katika mambo ya msingi sana na yasiyohitaji hata ubishi!! [emoji22]
 
Umekaa kwenye industry gani? Aviation, Security, ICT, au terrorism?
Kama umekaa kwenye security au Aviation ulipaswa kuwa na taarifa Mataifa yote duniani kuna sheria ya kuomba vibali vya kurusha drone zenye uzito flani, na hata hizo ndogo kama za kufanyia video shooting zinatakiwa maeneo flani zisipite, na kuna mwisho wa kimo cha kwenda juu (altitude) kuepuka kuingiliana na pilot operated civilian aircrafts kama helicopter na Aeroplane.

Kuna video hapo juu ya CBS TV nimeiweka inaelezea drone ndogo ya camera inaweza kugonga ndege na kutoboa body ya ndege, wanasema ni hatari kuliko bird strike ya ndege(mnyama) mwenye ukubwa sawa na hiyo drone.

Canada, EU, UK, Australia, USA, Japan, Israel, China, Rwanda, South Africa na kwingineko duniani lazima drone zisajiriwe au zisizo sajiriwa kuna maeneo huruhusiwi kuzirusha hadi upate kibali. Sasa nikuulize kama hujaenda kwenye mamlaka husika utayajuaje hayo mashariti?

Tatizo akili zenu zimakariri kukosoa na kupinga tu kiasi kwamba hujaelewa hilo tangazo halizuii watu kurusha drone au kzitumia au kuzimiliki bali unatakiwa uwe na kibali.

Si vibaya ukijifunza kuliko kutukana na kubishia vitu usivyo na uelewa navyo.
Sheria ya kuhitaji unmanned aircrafts au Remotely Piloted Aircrafts zisajiriwe ipo tangu mwaka 1944 kwa nchi wanachama wa ICAO iliyo chini ya UN. Mkataba ulisainiwa Chicago Marekani. wakati huo hata huko Marekani au China au Japan au Ulaya kulikuwa na watu binafsi wachache sana wenye kumiliki hizo drone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…