KERO Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), hili la maegesho (parking) ni kero kubwa

KERO Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), hili la maegesho (parking) ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Leo nimeshangaa pale nilipoegesha gari Terminal 2 kwa saa 72 na kudaiwa 75,000 za maegesho na kuambiwa kuwa “Long term parking” inahesabiwa ukiegesha Terminal III.

Kwanza, kaka aliyekuwa pale nikamuomba anisaidie (najua kuna uwezekano huo kwani mfumo unaona wazi gari limekaa muda mrefu hivyo linakidhi vigezo vya kuwa kwenye discount ya Long term parking). Yule kaka akataka nimpe 50,000/- aniachie au nilipe hiyo 75,000/-. Mimi si muumini wa kutoa wala kupokea rushwa, nikaona nilipe na kupata risiti hii (nimeiambatanisha chini).

IMG_4354.jpeg


Nilisikitika mtu mzima mwenye kuonekana mwislam safi (alikuwa na sigda) kutaka rushwa huku kukiwa na maafisa wenzake 2 nyuma yake bila aibu. Ni aibu sana kama aina hii ya treatment watakuwa wanapewa wageni toka nje ya Tanzania. Watu hawa wanaaibisha Taifa kama hivi ndivyo wanavyofanya kazi.

Hivi, JNIA si ni ileile? Pia, kuna ugumu gani wa kuweka mifumo ya kidigitali ikatenda haki badala ya kuweka watu wanaoomba rushwa waziwazi?

Ushauri:
  • Mamlaka zinazohusika ziwachunguze wahusika hawa (hasa huyu kaka aliyekuwepo leo) kwa vitendo vya rushwa, watabaini mengi
  • Mfumo wa kidigitali ufungwe kuepusha usumbufu wakati wa ulipaji gharama za maegesho
  • Nina mashaka na kampuni yenye zabuni ya uendeshaji maegesho; kama ikiwezekana wale wanaoendesha maegesho Mlimani City aidha wapewe zabuni hii au waombwe ushauri ili kuifanya JNIA kuwa na maegesho yanayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
 
Pole kwa changamoto mkuu, ungeuliza hiyo huduma ipo?, Huduma ya long term parking inapatikana kwenye maegesho ya TB 3 pekee kwa sababu kuna maegesho makubwa, Terminal 2 maegesho madogo ukianza kutoa hiyo huduma patajaa haraka..
 
Pole kwa changamoto mkuu, ungeuliza hiyo huduma ipo?, Huduma ya long term parking inapatikana kwenye maegesho ya TB 3 pekee kwa sababu kuna maegesho makubwa, Terminal 2 maegesho madogo ukianza kutoa hiyo huduma patajaa haraka..
Yaani, kama na wewe unahusika huku maelezo yako yanaonyesha kwanini Tanzania inachelewa sana kwenda mbele kwenye mambo marahisi kama haya.

This is a lame excuse. Kaeni huko mkajitafakari.

Na la kuombwa rushwa unalionaje?
 
Mkuu ulisikitika kuombwa rushwa? Au kuombwa rushwa na sheikh? 🤣

Hoja iwe rushwa tu

Nb: inasikitisha sana
 
Yaani, kama na wewe unahusika huku maelezo yako yanaonyesha kwanini Tanzania inachelewa sana kwenda mbele kwenye mambo marahisi kama haya.

This is a lame excuse. Kaeni huko mkajitafakari.

Na la kuombwa rushwa unalionaje?
Mimi niliuliza kwanza, nikapewa hayo maelezo nikaenda Tb3.
 
Mkuu - hayo maegesho yapo. Ila ni lazima uulize, ili kuyajua. Yako kama ukiwa unatoka terminal 3 - kuelekea geti la kutoka la Terminal 3 - Mkono wa kushoto.

Mimi nilikuwa nasafiri kwenda nje ya nchi kwa siku kama 3 hivi - ndio nilipajua. Maana nilikuwa nataka kuacha gari - kuondoa hizi gharama za kufuatwa. Nikawauliza watu hao wa parking walioko kwenye hicho kibanda cha malipo - ndio wakanielekeza.

Ni vigumu sana kupaona; maana panaonekana kama parking nyingine - ingawa kuna kibao ukikaribia. Labda waweke vibao tangu huku mwanzo wa parking za T3 - ili mtu aweze kuziona. Na vibao vingine waweke huko T2 pia.
 
Acha kuchagua zambi.........

Kitimoto dhambi

Kusema uongoo dhamb

Kuzini dhambi

Kutaman dhambi

Kula ua dhambi

Kusengenya dhambi

.........rushwaa dhambi............
 
Mkuu - hayo maegesho yapo. Ila ni lazima uulize, ili kuyajua. Yako kama ukiwa unatoka terminal 3 - kuelekea geti la kutoka la Terminal 3 - Mkono wa kushoto. Mimi nilikuwa nasafiri kwenda nje ya nchi kwa siku kama 3 hivi - ndio nilipajua. Maana nilikuwa nataka kuacha gari - kuondoa hizi gharama za kufuatwa. Nikawauliza watu hao wa parking walioko kwenye hicho kibanda cha malipo - ndio wakanielekeza. Ni vigumu sana kupaona; maana panaonekana kama parking nyingine - ingawa kuna kibao ukikaribia. Labda waweke vibao tangu huku mwanzo wa parking za T3 - ili
mtu aweze kuziona. Na vibao vingine waweke huko T2 pia.

Kwamba uwazi wala taarifa za kutosha hakuna, usidhani kuwa hawajui bali huo ni mradi na mlolongo wa walaji utashangaa.
 
Sasa mkuu, wewe umeamua kuacha gari tu na kuondoka halafu unataka wakuchaji kama mtu ulioomba long term parking? Kwanini hukusema mwanzo? Hivi unawezaje kuacha gari muda mrefu bila kutoa taarifa kwa attendants?

Nilitaka kuacha gari SGR station kwa siku tatu. Nikauliza 24hrs kiasi gani? Wakaniambia ni 20,000/-. Nikaondoka na mkweche wangu nikarudi na bajaj.
 
Hao TAA ifike sehemu wabinafsishwe ili waweke vitu vya kisasa, mfano Barabara za kurusha ndege walishindwa kujenga mpaka wakapewa Tanroad, sasa hivi sijui hata viwanja nivya taasisi IPi kati ya Tanroad na hao TAA, maana wameshindwa kuviendeleza wapo wanasubiri muongozo viwanja ni vya taasisi ipi?
 
Hao TAA ifike sehemu wabinafsishwe ili waweke vitu vya kisasa, mfano Barabara za kurusha ndege walishindwa kujenga mpaka wakapewa Tanroad, sasa hivi sijui hata viwanja nivya taasisi IPi kati ya Tanroad na hao TAA, maana wameshindwa kuviendeleza wapo wanasubiri muongozo viwanja ni vya taasisi ipi?
Haa Wao Utawakuta Kwenye Maegesho Tanzania Ina Shida
 
Back
Top Bottom