A
Anonymous
Guest
Leo nimeshangaa pale nilipoegesha gari Terminal 2 kwa saa 72 na kudaiwa 75,000 za maegesho na kuambiwa kuwa “Long term parking” inahesabiwa ukiegesha Terminal III.
Kwanza, kaka aliyekuwa pale nikamuomba anisaidie (najua kuna uwezekano huo kwani mfumo unaona wazi gari limekaa muda mrefu hivyo linakidhi vigezo vya kuwa kwenye discount ya Long term parking). Yule kaka akataka nimpe 50,000/- aniachie au nilipe hiyo 75,000/-. Mimi si muumini wa kutoa wala kupokea rushwa, nikaona nilipe na kupata risiti hii (nimeiambatanisha chini).
Nilisikitika mtu mzima mwenye kuonekana mwislam safi (alikuwa na sigda) kutaka rushwa huku kukiwa na maafisa wenzake 2 nyuma yake bila aibu. Ni aibu sana kama aina hii ya treatment watakuwa wanapewa wageni toka nje ya Tanzania. Watu hawa wanaaibisha Taifa kama hivi ndivyo wanavyofanya kazi.
Hivi, JNIA si ni ileile? Pia, kuna ugumu gani wa kuweka mifumo ya kidigitali ikatenda haki badala ya kuweka watu wanaoomba rushwa waziwazi?
Ushauri:

- Mamlaka zinazohusika ziwachunguze wahusika hawa (hasa huyu kaka aliyekuwepo leo) kwa vitendo vya rushwa, watabaini mengi
- Mfumo wa kidigitali ufungwe kuepusha usumbufu wakati wa ulipaji gharama za maegesho
- Nina mashaka na kampuni yenye zabuni ya uendeshaji maegesho; kama ikiwezekana wale wanaoendesha maegesho Mlimani City aidha wapewe zabuni hii au waombwe ushauri ili kuifanya JNIA kuwa na maegesho yanayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia