Tunawatakia kila la heri wote waendazao
Rafiki yangu, nikupongeze, sikupi pole hata kidogo kwa sababu sasa ndio chama chenu kinasafishika kabisa.
Hakuna sababu tena ya kusema mnahujumiwa.
Mtakaobaki nao huko chamani wakati huu, hao ndio wananchama wenu haswa, na mnatakiwa muwatambue na kuwathamini.
Kifupi ni kwamba, chama chenu kimeyapita na kuyashinda majaribio yote ya kutaka kukisambaratisha kutoka nje.
Kama CHADEMA itasambaratika sasa, ni nyinyi wenyewe ndio mtakaoisambaratisha.
Sasa nirudi kwako kukumbusha na kupitia kwako kuwakumbusha nyote. Chama chenu kiko huko mitaani. Huko ndiko kunakotakiwa kuimarishwa zaidi.
Haya yanayotokea sasa nchini, ni kama nyote, yaani vyama vyote, mnapewa mwanzo mpya, si CCM, ACT-Wazalendo, CUF, nyote mnapewa nafasi sawa ya kujiimarisha kwa wananchi. Na hilo litatokea tu iwapo SERA zenu zinaeleweka vizuri na wananchi.
Utakuwa ulishanielewa siku nyingi. Ngoja nikuachie hapo.
Ahaaa! Nimekumbuka jambo baada ya kuondoka.
Udanganyifu mkubwa ni kwamba wengi wanadhani sera za CCM zinaeleweka vizuri na kukubalika kwa wananchi?
Unaweza kunitajia hata moja wanayoifuata CCM?
Wananchi wataendelea kuwachagua CCM, sio kwa sera zao nzuri, bali hawaoni wala kuelewa sera zenu ni zipi.