Manara aomba msamaha kwa dharau alizowafanyia Magereza

Manara aomba msamaha kwa dharau alizowafanyia Magereza

Nilisikia askari magereza huwa wanapitia mafunzo makali kudhibiti wafungwa sasaa kile kichambooo wakabaki wanakenua meno tu.
 
Msamehe tu, mtafute umuone kwanza kisha uje utupe mrejesho.

Hata utashangaa anawezaje kuongea hivyo.

Wanasema watu wenye infiriority complex wanaomgea sanaa, basi ndio yule, anajua kila kitu.
Ahhaha
 
Msemaji maarufu wa masuala ya michezo, Haji Manara, ameomba radhi rasmi kwa Jeshi la Magereza kufuatia matamshi makali aliyoyatoa dhidi ya askari wa Magereza.

Manara alitoa msamaha huo baada ya kuibuka kwa video inayomuonyesha akizungumza kwa hasira dhidi ya askari wa Magereza wakati wa mahojiano yake na waandishi wa habari.
Mwanachama huyo wa Yanga ameliomba radhi jeshi la Magereza huku akifafanua kwa undani tukio la kubishana na baadhi ya maafisa wa jeshi hilo wakati akitoka kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya Tanzania Prisons jana kwenye Uwanja wa KMC.
Uongozi wa Jeshi la Magereza limetoa onyo na kuwataka kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza au kudharau Mamlaka yake.

Kauli hiyo imetolewa na Msemani wa Jeshi la Magereza baada ya kipande cha video kilichosambaa mtandaoni kikimuonesha, Ndugu Haji Manara kukutaa kwa dharau na kuanza kutoa maneno yasiyo ya kiungwana baada ya kuombwa kutoa gari lake mbele lililozuia gari la Jeshi la Magereza.
IMG_1967.jpeg
 
Back
Top Bottom