Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Maneno yana nguvu,maneno yanaleta hamasa,maneno yana leta ushindi ,maneno yana ponya ,maneno yanaweza fanya Mtu akaingia uwanja wa vita bila silaha mkononi kupambana na mwenye silaha ya kivita na akashinda vita bila silaha, maneno yanaleta amani ya moyo ,maneno yanaleta matumaini,maneno yanatia nguvu ,maneno yanaleta na kuwajaza watu ujasiri ,maneno yana Uwezo wa Kuleta mabadiliko na mageuzi ya kifikira.
Kwa hakika maneno yaliyotoka kwenye kinywa cha Rais wetu na Mama yetu kipenzi na Mwenyekiti wa chama changu cha Mapinduzi,kwa hakika yamenibubujisha Machozi ya furaha mpaka kupelekea kuvimba macho Utafikiri nimeng'atwa au kuumwa na nyuki waliochokozwa katika mzinga wao.
Ni maneno ya kijasiri ,ni maneno ya kiuongozi ,ni maneno ambayo yametulipua kwa furaha wana CCM wote na wale wote wenye kuipenda Nchi hii na kuiamini CCM kama chama pekee chenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu na kuliletea maendeleo endelevu na yenye kugusa Maisha ya watu.
Ni maneno ambayo kila mwana CCM alitamani kuyasikia yakitoka katika kinywa cha Rais wetu na mwenyekiti wetu. ili kuleta na kujenga heshima na nidhamu ya chama chetu. Ni maneno ambayo yametukumbusha kuwa CCM ni kubwa kuliko mtu yeyote yule na hakuna aliye juu ya CCM wala mwenye uwezo wa kuipasua CCM.
Ni maneno ambayo yameonesha kuwa huwezi kuitikisa CCM wala kuiyumbisha wala kuigawa wala kuitunishia misuri na kuleta kiburi kwa CCM ukiwa ndani ya CCM.
Kwa hakika Rais Samia ni kiongozi na nusu na ni kiongozi sahihi kabisa kuiongoza CCM na Taifa letu kwa ujumla wake. Ni jasiri muongoza njia,ni nahodha Hodari,ni jemedari imara ,ni simba wa nyika ,ni nyota ya matumaini,ni Mwamba usiotikiswa.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.