Maneno ya Rais Samia Yanibubujisha Machozi Ya Furaha Mpaka Kuvimba Macho Utafikiri nimeng'atwa na Nyuki waliochokozwa katika Mzinga wao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Maneno yana nguvu,maneno yanaleta hamasa,maneno yana leta ushindi ,maneno yana ponya ,maneno yanaweza fanya Mtu akaingia uwanja wa vita bila silaha mkononi kupambana na mwenye silaha ya kivita na akashinda vita bila silaha, maneno yanaleta amani ya moyo ,maneno yanaleta matumaini,maneno yanatia nguvu ,maneno yanaleta na kuwajaza watu ujasiri ,maneno yana Uwezo wa Kuleta mabadiliko na mageuzi ya kifikira.

Kwa hakika maneno yaliyotoka kwenye kinywa cha Rais wetu na Mama yetu kipenzi na Mwenyekiti wa chama changu cha Mapinduzi,kwa hakika yamenibubujisha Machozi ya furaha mpaka kupelekea kuvimba macho Utafikiri nimeng'atwa au kuumwa na nyuki waliochokozwa katika mzinga wao.

Ni maneno ya kijasiri ,ni maneno ya kiuongozi ,ni maneno ambayo yametulipua kwa furaha wana CCM wote na wale wote wenye kuipenda Nchi hii na kuiamini CCM kama chama pekee chenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu na kuliletea maendeleo endelevu na yenye kugusa Maisha ya watu.

Ni maneno ambayo kila mwana CCM alitamani kuyasikia yakitoka katika kinywa cha Rais wetu na mwenyekiti wetu. ili kuleta na kujenga heshima na nidhamu ya chama chetu. Ni maneno ambayo yametukumbusha kuwa CCM ni kubwa kuliko mtu yeyote yule na hakuna aliye juu ya CCM wala mwenye uwezo wa kuipasua CCM.

Ni maneno ambayo yameonesha kuwa huwezi kuitikisa CCM wala kuiyumbisha wala kuigawa wala kuitunishia misuri na kuleta kiburi kwa CCM ukiwa ndani ya CCM.

Kwa hakika Rais Samia ni kiongozi na nusu na ni kiongozi sahihi kabisa kuiongoza CCM na Taifa letu kwa ujumla wake. Ni jasiri muongoza njia,ni nahodha Hodari,ni jemedari imara ,ni simba wa nyika ,ni nyota ya matumaini,ni Mwamba usiotikiswa.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Huchokagi kububujikwa na machozi kila mara?

 
Baada ya muda mrefu hatimae ocne again luca amebubujikwaaaaaaa 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hata SAMIA SULUHU HASSAN
Naye ana PhD
Basi kazi ipo Tanzania 🇹🇿
 

SISI TUNAMSUKUMIZIA MWENYEZI MUNGU KAMA ALIAMUA UGOMVI KIPINDI KILE BASI ATATUAMULIA UGOMVI KIPINDI HIKI.

PUMZIKA KWA AMANI MDUDE,SOKA NA WENGINE WOTE AMBAO MMEPOTEZWA / KUTEKWA NA MAMLAKA ZA DOLA.
 
Ile point ya kulifukuza li Gwajima.... Safi sana
Hoja haipigwi vilungu hujibiwa kwa hoja " Jk nyerere" hata ukimfukuza hoja ya wajima inaishi na haijajibiwa bado
Kwamba kuna watu 83 wametekwa. Gwajima ana ushahidi mkononi.
Kwamba wakuu wa vyombo wanabadilishwa kama " chupi za mwenyekiti"
Kwamba maslahi ya wafanyakazi ni hafifu!
Hoja hizi haziwezi kujibiwa kwa chawa kama wewe kubinua VIUNO na kushangilia wala mkubwa kumshughulikia mwanamke mwenzake mpaka KITOKE MAJI
 
GWAJIMA ni mnafiki tu yule na hana lolote lile zaidi ya kutapatapa tu.
 
WAZALENDO WOTEEEE TUMEPIGWA DOLE LA KATI.

SISI TUNAMSUKUMIZIA MWENYEZI MUNGU KAMA ALIAMUA UGOMVI KIPINDI KILE BASI ATATUAMULIA UGOMVI KIPINDI HIKI.

PUMZIKA KWA AMANI MDUDE,SOKA NA WENGINE WOTE AMBAO MMEPOTEZWA / KUTEKWA NA MAMLAKA ZA DOLA.
Tena hii mapema tu,damu za kina Mzee Kibao,Mdude, Soka na wenzake haziwezi kumuacha salama.
 
GWAJIMA ni mnafiki tu yule na hana lolote lile zaidi ya kutapatapa tu.
Narudia tena " hoja haipigwi virung" hujibiwa . Hoja ya GWAJIMA ni
1. Watu 83 wametekwa ( utekaji) ushahidi anao
2. Wakuu wa vyombo wanabadilishwa kama nguo za ndani
Kumuita GWAJIMA Mnafiki bila kujibu haya ni sawa na mwanamke kumsaga mwanamke mwenziwe akiambiwa anakasirika
Gwajima ajibiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…