Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
- Thread starter
- #21
Tumepewa akili na uwezo wa kufikiri, tutumie akili zetu.Hizi ni hisia, hujaweka ushahidi wa kuzipa uzito hisia hizi.
Again, extraordinary claims require extraordinary evidence.
Kuna mambo ambayo specifically yaliraise flag. Nimekupa mifano kadhaa, wewe niambie mtazamo wako.
1. Unaamini katika Tanzania, kapteni wa jeshi anaweza kutoa video ile halafu bado akabaki huru kambini kama Mange na huyo Kapteni walivyotuaminisha, eti akiambiwa kuna kambi nyingi na wanajeshi wengi wako nyuma yake? Unaamini hilo linawezekana Tanzania?
2. Kupeleka tarehe ya maandamano anayoyapromote kuwa siku ya uchaguzi, unadhani siyo njia ya kuilinda CCM?
3. Kupromote wazo la kutaka jeshi lichukue nchi, siyo njia ya kuilinda CCM na viongozi wake? (Ndiyo msingi wa uzi wangu ule mwingine kuhusu mada hii)
4. Kuna wakati aliibua ishu ya kontena la silaha. Je, haikuwa nia ya kuwaogopesha watanzania hawa ambao tayari wana asili ya woga? Ndiyo maana nimemuita "agent of confusion".
5. Kuna wakati "alimkataa" Mpina ila sasa hivi anamsifia na hadi kutumia video zake kama ushahidi wa tuhuma anazotoa. Je, nia haiwezi kuwa anatumika kumuuza tena kwa Watanzania na hivyo kutimiza lengo la kuzidi kuwachanganya watanzania wasijue mtetezi wao hasa ni nani?
6. Hataki sana kuyahusisha maandamano yake na ishu ya Lissu wakati huyo ndiyo nguzo pekee ya uhakika wa kupambana na CCM. Kwa nini?
7. Ameweka bifu lake kwa anayemuita "kimama" wakati tatizo la msingi ni mfumo wa kiutawala na kisiasa. Hata huyo anayemuita "kimama" asigekuwepo, hayo anayoyasema yangetokea maana tuliona yakitokea kabla yake.
Kwa haraka nimezifikiria hizi. Embu zijibu hoja hizi.