Wiki kadhaa zilizopita niliwataja Mange Kimambi, Humphrey Polepole na Luhaga Mpina kama watu ambao sijaamini dhamira ya maneno na matendo yao ya kisiasa. Haya maneno niliyasema siku kadhaa kabla taarifa za kupotea kwa Polepole hazijatoka.
Niliwahi kusema master plan ya siasa za CCM ni kuwa pande zote mbili za shilingi ili ku control narrative. Kwa maana hiyo, watakuwa upande wa kujisifia lakini pia watakuwa upande wa kujisema vibaya. Kumbuka usemi wa "Shetani unayemjua".
Tuwaache hao wengine wawili kwa sasa, leo ngoja nigusie zaidi kwa nini nadhani Mange Kimambi anafanya kazi tofauti na mnayodhania.
Sina kawaida ya kutoa maoni yangu bila kwanza kujiridhisha jambo husika. Kwa jinsi siku zinavyokwenda, naona kama Mange anaweza kuwa anatumika kama "agent of confusion" ambaye nia na malengo ya kumtumia ni kuwachanganya watanzania, kuwaongezea hofu na kuwafanya wasiweze kuungana katika kuchukua hatua madhubuti za kisiasa.
Nitatolea mfano mmoja issue ya hiyo kampuni sijui ya ITEL anayoiongelea sana sasa hivi. Kwa muda sasa amekuwa anasema "Abdul" mara anachota pesa BOT, mara anachota pesa CRDB, mara tozo ya airport yote anachukua yeye. Sasa hivi anasema ana hiyo kampuni iliyopewa vibali na tenda kubwa kubwa za sukari, makaa ya mawe na mambo chungu nzima. Kama kampuni ina vibali na tenda hizo zote, kwa nini waende kuhangaika na kuchota pesa Hazina au kufanya mambo uliyokuwa unaibua hapo mwanzo? Kama mtu ana tenda na vibali hivyo vyote vya thamani ya mabilioni ya pesa, atashindwa kuwa na magari ya kifahari au nyumba nzuri? Real issue hapa ni ipi?
Jambo lililonihakikishia kuwa wasiwasi wangu kuhusu Mange unaweza kuwa na kweli ni issue ya "Kapteni Tesha". Dakika nilipoiangalia ile video ya Tesha sikuiamini hata 0%. Huyo Tesha kila alichokuwa anasema ni kama alikuwa anasoma post za Mange moja kwa moja kutoka katika IG account yake. Hakuna jipya alilosema halafu anaahidi atarudi tena! Baadae eti anatumiwa vitambulisho na wanajeshi, yaani tunafanywa kama watoto wadogo.
Mange anaibua mambo mazito ambayo kwa juu unaona ya maana lakini kisiasa hayana faida sana kwa siasa zetu. Siasa za kuibua mambo ya ufisadi zimekuwepo toka enzi za Mrema lakini hazijawahi kuitisha CCM na serikali zake.
Kwa kuibua mambo mengi mengi, wananchi wanakosa na kupoteza focus. Wanakosa lengo moja ambalo linawaunganisha. Zinabaki siasa za umbea. Real issues ambazo zingeweza kuwafanya wananchi wachukue hatua zinawekwa pembeni au kusahaulika maana wanakuwa busy kuongelea mambo mengi mengi ambayo yana ukweli nusu nusu au ambayo hayana nguvu za kisiasa katika mazingira yetu.