GE2025 Mange Kimambi anaweza kuwa ni "Double agent" anayewasaidia anaowasema 'vibaya' kila siku

GE2025 Mange Kimambi anaweza kuwa ni "Double agent" anayewasaidia anaowasema 'vibaya' kila siku

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Vipi ile risiti ya bilioni 2.4 kwenye duka la vigae kwanini ilivyowekwa mitandaoni masaa machache tu TRA waliiondoa kwenye database ile QR code??

Pia double agent siku hizi TCRA wanaweza kutuma copyright claims na zuio kwa Meta ili habari fulani zisipatikane Tanganyika?

Double agent siku hizi anaweza kuitwa na FBI kwa mahojiano juu ya matishio wanayoyapata kuhusu uhai wake kutokea taifa alilopoishi zamani?

Make it make sense.
 
Wiki kadhaa zilizopita niliwataja Mange Kimambi, Humphrey Polepole na Luhaga Mpina kama watu ambao sijaamini dhamira ya maneno na matendo yao ya kisiasa. Haya maneno niliyasema siku kadhaa kabla taarifa za kupotea kwa Polepole hazijatoka.

Niliwahi kusema master plan ya siasa za CCM ni kuwa pande zote mbili za shilingi ili ku control narrative. Kwa maana hiyo, watakuwa upande wa kujisifia lakini pia watakuwa upande wa kujisema vibaya. Kumbuka usemi wa "Shetani unayemjua".

Tuwaache hao wengine wawili kwa sasa, leo ngoja nigusie zaidi kwa nini nadhani Mange Kimambi anafanya kazi tofauti na mnayodhania.

Sina kawaida ya kutoa maoni yangu bila kwanza kujiridhisha jambo husika. Kwa jinsi siku zinavyokwenda, naona kama Mange anaweza kuwa anatumika kama "agent of confusion" ambaye nia na malengo ya kumtumia ni kuwachanganya watanzania, kuwaongezea hofu na kuwafanya wasiweze kuungana katika kuchukua hatua madhubuti za kisiasa.

Nitatolea mfano mmoja issue ya hiyo kampuni sijui ya ITEL anayoiongelea sana sasa hivi. Kwa muda sasa amekuwa anasema "Abdul" mara anachota pesa BOT, mara anachota pesa CRDB, mara tozo ya airport yote anachukua yeye. Sasa hivi anasema ana hiyo kampuni iliyopewa vibali na tenda kubwa kubwa za sukari, makaa ya mawe na mambo chungu nzima. Kama kampuni ina vibali na tenda hizo zote, kwa nini waende kuhangaika na kuchota pesa Hazina au kufanya mambo uliyokuwa unaibua hapo mwanzo? Kama mtu ana tenda na vibali hivyo vyote vya thamani ya mabilioni ya pesa, atashindwa kuwa na magari ya kifahari au nyumba nzuri? Real issue hapa ni ipi?

Jambo lililonihakikishia kuwa wasiwasi wangu kuhusu Mange unaweza kuwa na kweli ni issue ya "Kapteni Tesha". Dakika nilipoiangalia ile video ya Tesha sikuiamini hata 0%. Huyo Tesha kila alichokuwa anasema ni kama alikuwa anasoma post za Mange moja kwa moja kutoka katika IG account yake. Hakuna jipya alilosema halafu anaahidi atarudi tena! Baadae eti anatumiwa vitambulisho na wanajeshi, yaani tunafanywa kama watoto wadogo.

Mange anaibua mambo mazito ambayo kwa juu unaona ya maana lakini kisiasa hayana faida sana kwa siasa zetu. Siasa za kuibua mambo ya ufisadi zimekuwepo toka enzi za Mrema lakini hazijawahi kuitisha CCM na serikali zake.

Kwa kuibua mambo mengi mengi, wananchi wanakosa na kupoteza focus. Wanakosa lengo moja ambalo linawaunganisha. Zinabaki siasa za umbea. Real issues ambazo zingeweza kuwafanya wananchi wachukue hatua zinawekwa pembeni au kusahaulika maana wanakuwa busy kuongelea mambo mengi mengi ambayo yana ukweli nusu nusu au ambayo hayana nguvu za kisiasa katika mazingira yetu.
Hizo kwa %98 ni porojo za wanufaika wa mfumo kama mlivyo sema kwa HPp na kwakuwa maji ya shingo mnaleta maigizo uchwara,mnachotakiwa kujua ni kuwa hata wale chawa wenu hamko mao tena,kwani kila washikapo kwa moto tena kweli kweli!.Wamefika mahali kuliko waungue wao wameonabora warudisheckijiti kwavwenye kijiti chao,isiwe tabu.
 
Vipi ile risiti ya bilioni 2.4 kwenye duka la vigae kwanini ilivyowekwaa mitandaoni masaa machache tu TRA waliiondoa kwenye database ile QR code??

Pia double agent siku hizi TCRA wanaweza kutuma copyright claims na zuio kwa Meta ili habari fulani zisipatikane Tanganyika?

Double agent siku hizi anaweza kuitwa na FBI kwa mahojiano juu ya matishio wanayoyapata kuhusu uhai wake kutokea taifa alilopoishi zamani?

Make it make sense.
Kwa hiyo wewe unaamini kabisa Mange alikuwa hajui kwa harakati zake yupo kwenye rada za hao FBI hadi eti kushangaa wamejuaje kwamba anakwenda kwenye maandamano? Mambo kama haya yananifanya nijiulize sana ukweli wake wa moyo.

Kuhusu TRA sijui TCRA, hivi kwani mtu akiwa pandikizi, ili kumuongezea uhalali wa kuaminika na upande wa pili huwa wanafanyaje? Si ni kwa mara kwa mara kumpa taarifa za "kweli" zisizo na madhara makubwa kwenu? Si ni kwa kuonyesha mnajaribu kupambana naye?

Hii mada nimeileta kama swali ili tufikiri kwa pamoja maana ni kwa miaka mingi sasa CCM imekuwa ina tabia ya kupandikiza watu wa kutuuzia malalamiko na misimamo ya kisiasa halafu mwisho wa siku wanaunga mkono juhudi.
 
Hizo kwa %98 ni porojo za wanufaika wa mfumo kama mlivyo sema kwa HPp na kwakuwa maji ya shingo mnaleta maigizo uchwara,mnachotakiwa kujua ni kuwa hata wale chawa wenu hamko mao tena,kwani kila washikapo kwa moto tena kweli kweli!.Wamefika mahali kuliko waungue wao wameonabora warudisheckijiti kwavwenye kijiti chao,isiwe tabu.
Bahati nzuri au mbaya, mimi siyo mnufaika wa mfumo hata kidogo. Nipo hapa kutoa maoni yangu kwa kile ninachoona. Naweza kuwa nakosea au napatia ila nia yangu ni njema kabisa.
 
Unaweza waza tofauti pia ila double agent unajuwa adhabu yake ni nini baada ya kazi kuisha? Mange si double agent kwa namna moja hajawahi badili msimamo wake na hata akibadili saiv it is too late maana kila mtu keshakuwa sumu
"Double agent" si kwa maana ya kuwa anatumika na NCHI mbili tofauti ila na PANDE mbili. Anajua maandamano yakishindikana, yeye anajisafisha kirahisi tu kwenu kwamba aliwapa kila taarifa na msisitizo ila mmeshindwa wenyewe. Upande wa pili pia utafurahi kwa maana amewavuruga wananchi na kufanikisha lengo la upande huo la kuvuka salama.
 
Ila mange mnafikiii! Anawahamasisha wenzie waandamane ila yeye hakuandamana🤣🤣🤣🤣

Kwa kujikosha sasa, akasafiri kabisa ila kufika huko akavaa mask na kujificha. Real drama queen.
 
Kwa hiyo wewe unaamini kabisa Mange alikuwa hajui kwa harakati zake yupo kwenye rada za hao FBI hadi eti kushangaa wamejuaje kwamba anakwenda kwenye maandamano? Mambo kama haya yananifanya nijiulize sana ukweli wake wa moyo.
Wewe una uhakika gani alikua anajua?
Kuhusu TRA sijui TCRA, hivi kwani mtu akiwa pandikizi, ili kumuongezea uhalali wa kuaminika na upande wa pili huwa wanafanyaje? Si ni kwa mara kwa mara kumpa taarifa za "kweli" zisizo na madhara makubwa kwenu? Si ni kwa kuonyesha mnajaribu kupambana naye?
Ok kwahiyo kuhusu TCRA wala TRA hujui ila mkataba wa hiyo kampuni ya ITEl unaujua?

Kuna kampuni yoyote kubwa inafanya ujenzi wa vile haina nambari ya mlipa kodi?

Hadi hapo kwa kushindwa kujua kwanini ile risiti ilifutwa katika kanzidata ya TRA inadhihirisha hata upeo wa kujua "wakala kivuli" wanafanya vipi kazi rudi kasome zaidi utajua.
Hii mada nimeileta kama swali ili tufikiri kwa pamoja maana ni kwa miaka mingi sasa CCM imekuwa ina tabia ya kupandikiza watu wa kutuuzia malalamiko na misimamo ya kisiasa halafu mwisho wa siku wanaunga mkono juhudi.
Hujaleta mada kama swali juu hapo umeanza kama swali mwisho umeweka hitimisho na kutuaminisha unachokijua wewe, sasa tunapokupa rejea zaidi unabaki huelewi ni kitu gani ulikuwa unaongelea.

Mange ni CCM na spana anazopiga zinawakaanga CCM ndio maana wamemuweka kwenye rada zao.

Kuhusu Polepole hata kesi zao na Mange hazifanani hata kidogo na hata Mange mwenyewe alikuwa hajui muda anapiga hizo spana alikua yuko maficho yapi , Polepole very likely ameuzwa na watu wa karibu aliowaamini kuwaeleza ukweli yuko wapi na nilishaandika nadharia tatu humu ambazo zilinipa hitimisho kufikia nilichoandika.
 
Samahani mkuu ila naona umetoa conclusion kupitia hisia binafsi kwa sababu hata vitu ulivyovitaja havihusiani.

Mfano Mange kumsema mpina kwa sababu ya kuhamia ACT ni tofauti na Mange kumsifia kwa kuibua scandal aliyoisema..

Kumuhusisha Lissu na Maandamano ni sawa na kuhusisha maandamano na CHADEMA, hiyo inaondoa focus yake ya kuyaonesha kama "maandamano ya wananchi" Pasipo kutazama mitazamo ya kisiasa. Yani ccm vs chadema

Kingine Mange kubadilika ni kawaida yake, alimpigia promo Magufuli ila alivyoingia ikulu, akamgeuka kwa kuona anakiuka misingi ya demokrasia. Kitu hicho hicho kilochotokea kwa utawala uliopo

Kwa hiyo Mange amejitanabaisha kama si mtu anaeangalia mtu ila issue na misingi ya demokrasia anayoiamini

Kingine kutoa controversies/breaking news kubwa kubwa kwa Mange ni sawa na samaki kumtoa katika maji. Hicho ndio kitu kinampa upperhand na influence "kutoa habari exceptional and exclusive"..

Nadhani unabidi utafakari zaidi maana point nyingi zina weak bases

Japo siwezi kusema Mange hatumiki kwa sababu kuna baadhi ya info anazitoa unajua hii ni channel kubwa ipo nyuma yake. Kwa hiyo yawezekana watu baadhi wanamtumia kama channel kupitisha habari kubwa ambazo wao hawawezi kuzifikisha kwa watu openly.

Lakini bado haihalalishi madai yako unless utolewe uthibitisho wa yeye kupokea fedha ili aifanye kazi.
Kuhusu Mpina, kama unajua mbinu za siku zote za CCM za kucheza pande mbili za shilingi, lazima ungejua tu lazima baada ya kifo cha Magufuli wangetafuta mtu wa kuwasemea mashabiki wa Magufuli na wa kanda ya ziwa. Sikushangaa kuona anaibuka Mpina kufanya kazi hiyo. Hii ni textbook style ya CCM. Na ndiyo maana mmeletewa Janet naye. Mimi siyo mfuatiliaji wa siasa za kila siku ila hilo nililiona zamani sana, inakuwaje nyie mlio na za ndaani mnashindwa kuyaona hayo?

Kushindwa kuikataa CCM waziwazi ni dalili na ishara za kuilinda.

Kama tunataka hadi Rais apunguziwe madaraka, inakuwaje mambo mazito kama haya ya uchaguzi tunamuachia na kumuamini mtu mmoja tena mwenye very questionable character afikirie kwa niaba yetu sote na hadi afanye maamuzi makubwa kwa niaba yetu? Hamuoni hatari katika hilo?

Kama anageuka na kubadili misimamo yake kila siku, haiwezekani kwamba msimamo wake uko sokoni na yoyote anaweza kuununua akifika bei?

By the way, hivi "Kigogo" aliishia wapi?
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu. Machawa na mali zao tunaishi nao mitaani kwetu.

Ndugu watanzania, mafuta ya taa, petroli na viberiti havijawahi kuwa adimu.

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
adriz Lucha Magonjwa Mtambuka
 
Ila Watanzania wengi wanapenda sana conspiracy theories jamani.
Tanzania tunawapenda whistleblowers maana tunaona wana ujasiri na connections ambazo sisi hatuna lakini ndiyo rahisi sana watawala kutumia njia hiyo kutupoteza maboya.

By the way, hivi "Kigogo" aliishia wapi?
 
Wiki kadhaa zilizopita niliwataja Mange Kimambi, Humphrey Polepole na Luhaga Mpina kama watu ambao sijaamini dhamira ya maneno na matendo yao ya kisiasa. Haya maneno niliyasema siku kadhaa kabla taarifa za kupotea kwa Polepole hazijatoka.

Niliwahi kusema master plan ya siasa za CCM ni kuwa pande zote mbili za shilingi ili ku control narrative. Kwa maana hiyo, watakuwa upande wa kujisifia lakini pia watakuwa upande wa kujisema vibaya. Kumbuka usemi wa "Shetani unayemjua".

Tuwaache hao wengine wawili kwa sasa, leo ngoja nigusie zaidi kwa nini nadhani Mange Kimambi anafanya kazi tofauti na mnayodhania.

Sina kawaida ya kutoa maoni yangu bila kwanza kujiridhisha jambo husika. Kwa jinsi siku zinavyokwenda, naona kama Mange anaweza kuwa anatumika kama "agent of confusion" ambaye nia na malengo ya kumtumia ni kuwachanganya watanzania, kuwaongezea hofu na kuwafanya wasiweze kuungana katika kuchukua hatua madhubuti za kisiasa.

Nitatolea mfano mmoja issue ya hiyo kampuni sijui ya ITEL anayoiongelea sana sasa hivi. Kwa muda sasa amekuwa anasema "Abdul" mara anachota pesa BOT, mara anachota pesa CRDB, mara tozo ya airport yote anachukua yeye. Sasa hivi anasema ana hiyo kampuni iliyopewa vibali na tenda kubwa kubwa za sukari, makaa ya mawe na mambo chungu nzima. Kama kampuni ina vibali na tenda hizo zote, kwa nini waende kuhangaika na kuchota pesa Hazina au kufanya mambo uliyokuwa unaibua hapo mwanzo? Kama mtu ana tenda na vibali hivyo vyote vya thamani ya mabilioni ya pesa, atashindwa kuwa na magari ya kifahari au nyumba nzuri? Real issue hapa ni ipi?

Jambo lililonihakikishia kuwa wasiwasi wangu kuhusu Mange unaweza kuwa na kweli ni issue ya "Kapteni Tesha". Dakika nilipoiangalia ile video ya Tesha sikuiamini hata 0%. Huyo Tesha kila alichokuwa anasema ni kama alikuwa anasoma post za Mange moja kwa moja kutoka katika IG account yake. Hakuna jipya alilosema halafu anaahidi atarudi tena! Baadae eti anatumiwa vitambulisho na wanajeshi, yaani tunafanywa kama watoto wadogo.

Mange anaibua mambo mazito ambayo kwa juu unaona ya maana lakini kisiasa hayana faida sana kwa siasa zetu. Siasa za kuibua mambo ya ufisadi zimekuwepo toka enzi za Mrema lakini hazijawahi kuitisha CCM na serikali zake.

Kwa kuibua mambo mengi mengi, wananchi wanakosa na kupoteza focus. Wanakosa lengo moja ambalo linawaunganisha. Zinabaki siasa za umbea. Real issues ambazo zingeweza kuwafanya wananchi wachukue hatua zinawekwa pembeni au kusahaulika maana wanakuwa busy kuongelea mambo mengi mengi ambayo yana ukweli nusu nusu au ambayo hayana nguvu za kisiasa katika mazingira yetu.
Wino mwingi unamaliza miti😂😂
Unajua faida za kufichua ufisadi nadhani uliona kilicho tokea napel ni mfano mzuri huo .

Hiyo ina sababusha hasira kwa watu wengi na kusababisha machafuko mno.mfano kumeongeza tozo, kodi n.k

Alafu tunaona zile kodi zetu zinatumika kwenye kununulia watoto wa viongozi magari, nyumba nzuri n.k

Sasa kama wew unasema kufichua mafisadi siyo mbinu bora na inatoa watu kwenye focus .embu naomba hiyo njia bora sasa
 
Jambo ambalo mleta mada ulipaswa kulitila mashaka ndugu mleta mada ni kwamba, kuna hatari ya wahuni kuunda kundi litakalojifanya ni hasimu wa wanamtandao na likawa linampa taarifa za uwongo Mange.
 
Tanzania tunawapenda whistleblowers maana tunaona wana ujasiri na connections ambazo sisi hatuna lakini ndiyo rahisi sana watawala kutumia njia hiyo kutupoteza maboya.

By the way, hivi "Kigogo" aliishia wapi?
Mimi niko measured na nina uwezo wa kuhakiki mambo mengi.

Wiki ya jana akaunti ya Tanzania Leaks imeripoti Jaji Warioba amezuiwa kuongea na waandishi wa habari, amewekewa kizuizi nyumbani kwake na rais Samia.

Nijaona hii habari mbona kama uzushi?

Nikamtafuta rafiki yangu mtu wa nyumbani kwa Mzee Warioba, akaniambia hizo ni fake news tu.

So mara nyingi nina resources za ku verify mambo sitegemei hao whistleblowers wa mitandaoni.

Uzuri nchi yangu hii, Mkapa kapelekwa chuo Columbia na Uncle wangu, nimeanza kutembea corridors za Ikulu Dar tangu nipo tumboni mwa mama yangu.
 
Ungeweka miamala ya milungula Mange anachukua kutoka kwa Abdul kidogo ungeweza kuwekea uzito hoja yako.

Huo ungekuwa ushahidi uliozidi habari za kuonesha contradictions tu katika maneno na matendo ya Mange.

Kwa sababu contradictions zinaweza kufanywa kwa sababu ya ujinga wa mtu tu.

Maybe Mange is not as bright as you would like her to be.

If that is the case, then, tp you at least, she is just not too bright. Labda anadanganywa kirahisi, stories zake hazina consistency. Labda yuko emotional zaidi. Then she is just not too bright.

But that does not mean she is a double agent.

Points zako zote 7 ulizoziweka hapo juu inawezekana kabisa zikatokana na Mange kutokuwa makini, kudanganywa, kuendeshwa na hisia badala ya kuwa fact based.

Watanzania wengi wako hivyo.

Frankly mimi ningemshangaa sana Mange angekuwa hayupo hivyo, kwa sababu hizo ndizo tabia za Watanzania wengi.

Sasa unamtuhumu vipi Mange kuwa ni double agent kwa kuwa na tabia ambazo kwa Watanzania ni kawaida kabisa?

Watanzania inconsistencies, contradictions, being emotional ndiyo tabia zao.

Kuanzia mfagia choo mpaka Rais Samia.

Sasa Mange naye akiwa na tabia hizi ambazo ni za kawaida kwa Watanzania wengi, utazitumiaje hizi tabia common kabisa kama ushahidi kwamba ni double agent?

Maybe she is just a Tanzanian being a Tanzanian.

And you are being a Tanzanian too, always conjuring up a conspiracy theory with no backing fact.

That is what your lot of Tanzanians do best.
Kwa hiyo inawezekanaje maelfu ya watu wanakubali kuweka imani yao kwa mtu mmoja ambaye hana elimu, uzoefu wala ufahamu wa mbinu za kisiasa ili awaongoze na kuwafanyia maamuzi magumu kama haya ya sasa?

Yaani mtu mmoja anayeendeshwa na hisia atuamulie mambo mazito ya mustakabali wa taifa?

Hivi si tumekuwa tunasema hadi Rais apunguziwe madaraka, na tena Rais ni taasisi kabisa yenye idadi kubwa ya watumishi, halafu tunageuka tunaenda kumuamini mtu mmoja ambaye ana simu na bando. Yeye ndiyo apokee taarifa za dunia nzima, yeye ndiyo azichakate, azitolee tafsiri na ufafanuzi, na hadi atuamulie cha kufanya.

Risiti haiwezi kuwa uthibitisho tosha maana hata huyo Mange mwenyewe anapost risiti kila siku ila bado nimetokea kuhoji dhamira yake. Ndiyo maana nasisitiza tumepewa akili, tuzitumie vizuri. Watu wenye busara walisema, usiamini kila unachoona.
 
Mange yupo sahihi analeta maovu ya Kizimkazi kadili anavoyapata
 
Back
Top Bottom