GE2025 Mange Kimambi anaweza kuwa ni "Double agent" anayewasaidia anaowasema 'vibaya' kila siku

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hizi ni hisia, hujaweka ushahidi wa kuzipa uzito hisia hizi.

Again, extraordinary claims require extraordinary evidence.
Tumepewa akili na uwezo wa kufikiri, tutumie akili zetu.

Kuna mambo ambayo specifically yaliraise flag. Nimekupa mifano kadhaa, wewe niambie mtazamo wako.

1. Unaamini katika Tanzania, kapteni wa jeshi anaweza kutoa video ile halafu bado akabaki huru kambini kama Mange na huyo Kapteni walivyotuaminisha, eti akiambiwa kuna kambi nyingi na wanajeshi wengi wako nyuma yake? Unaamini hilo linawezekana Tanzania?

2. Kupeleka tarehe ya maandamano anayoyapromote kuwa siku ya uchaguzi, unadhani siyo njia ya kuilinda CCM?

3. Kupromote wazo la kutaka jeshi lichukue nchi, siyo njia ya kuilinda CCM na viongozi wake? (Ndiyo msingi wa uzi wangu ule mwingine kuhusu mada hii)

4. Kuna wakati aliibua ishu ya kontena la silaha. Je, haikuwa nia ya kuwaogopesha watanzania hawa ambao tayari wana asili ya woga? Ndiyo maana nimemuita "agent of confusion".

5. Kuna wakati "alimkataa" Mpina ila sasa hivi anamsifia na hadi kutumia video zake kama ushahidi wa tuhuma anazotoa. Je, nia haiwezi kuwa anatumika kumuuza tena kwa Watanzania na hivyo kutimiza lengo la kuzidi kuwachanganya watanzania wasijue mtetezi wao hasa ni nani?

6. Hataki sana kuyahusisha maandamano yake na ishu ya Lissu wakati huyo ndiyo nguzo pekee ya uhakika wa kupambana na CCM. Kwa nini?

7. Ameweka bifu lake kwa anayemuita "kimama" wakati tatizo la msingi ni mfumo wa kiutawala na kisiasa. Hata huyo anayemuita "kimama" asigekuwepo, hayo anayoyasema yangetokea maana tuliona yakitokea kabla yake.

Kwa haraka nimezifikiria hizi. Embu zijibu hoja hizi.
 
Bado sijakuelewa vizuri
 
Mbona unaharisha sana leo? Umekula chakula kilichochacha? Yaani huu ni uharo kabisa.
 
Matter to be supported by a beast of your kind, means it carries stupidity.
 
hata mimi hisia zangu zinanituma kabsa maandamano hayatafanikiwa na samia ataapishwa kuwa rais daaah japo inaniuma sana CCM na samia kuendelea kuwepo madarakani ila sina namna inasikitisha sana
 

Hayo uliyoandika hayamfanyi awe DOUBLE AGENT hata kidogo.

Inawezekana kabisa akawa hafocus vizuri lakini yeye objective yake ni kuhamasisha. Sasa huwezi hamasisha watu kwa story ileile kila siku ... lazima ubadili santuri!!
 
Point zako zote 7 zinaweza kuwa za uanaharakati wa kijinga tu, si lazima zitokane na Mange kuwa double agent.

Ili uweze kusema kwa ushahidi kuwa Mange ni double agent inabidi uoneshe ushahidi mkubwa kuliko hizi contradictions zinazoweza kutokana na ujinga tu.

Ujinga si ushahidi wa mtu kuwa double agent.

Ingekuwa hivyo kila mwanaharakati mjinga anayetaka kusimamisha uchaguzi bila strategy angekuwa double agent.
 
Kama kampuni ina vibali na tenda hizo zote, kwa nini waende kuhangaika na kuchota pesa Hazina

Swali zuri. Ni sawa na kuuliza “Tumekoppa matilioni ya pesa, mbona hakuna mradi tangible unao onekana ku cost pesa zote hizo?”
Haijulikani pesa zinatumika vipi. Time will tell.

Kuhusu double agent, Labda kuna tafsiri nyingine. Haujaweka ushaidi wowote.
 
Unataka ushahidi wa aina gani utakaokuridhisha?
 
Unataka ushahidi wa aina gani utakaokuridhisha?

Ungeweka miamala ya milungula Mange anachukua kutoka kwa Abdul kidogo ungeweza kuwekea uzito hoja yako.

Huo ungekuwa ushahidi uliozidi habari za kuonesha contradictions tu katika maneno na matendo ya Mange.

Kwa sababu contradictions zinaweza kufanywa kwa sababu ya ujinga wa mtu tu.

Maybe Mange is not as bright as you would like her to be.

If that is the case, then, tp you at least, she is just not too bright. Labda anadanganywa kirahisi, stories zake hazina consistency. Labda yuko emotional zaidi. Then she is just not too bright.

But that does not mean she is a double agent.

Points zako zote 7 ulizoziweka hapo juu inawezekana kabisa zikatokana na Mange kutokuwa makini, kudanganywa, kuendeshwa na hisia badala ya kuwa fact based.

Watanzania wengi wako hivyo.

Frankly mimi ningemshangaa sana Mange angekuwa hayupo hivyo, kwa sababu hizo ndizo tabia za Watanzania wengi.

Sasa unamtuhumu vipi Mange kuwa ni double agent kwa kuwa na tabia ambazo kwa Watanzania ni kawaida kabisa?

Watanzania inconsistencies, contradictions, being emotional ndiyo tabia zao.

Kuanzia mfagia choo mpaka Rais Samia.

Sasa Mange naye akiwa na tabia hizi ambazo ni za kawaida kwa Watanzania wengi, utazitumiaje hizi tabia common kabisa kama ushahidi kwamba ni double agent?

Maybe she is just a Tanzanian being a Tanzanian.

And you are being a Tanzanian too, always conjuring up a conspiracy theory with no backing fact.

That is what your lot of Tanzanians do best.
 
Pia yawezekena ni presha ya taarifa anazopokea na zote anataka kuziweka mitandaoni.

Ilibidi awe kama taasisi labda angweza kuwa kama mleta mada anavyotaka.

She is mere a person kama mleta mada tu.
 
Samahani mkuu ila naona umetoa conclusion kupitia hisia binafsi kwa sababu hata vitu ulivyovitaja havihusiani.

Mfano Mange kumsema mpina kwa sababu ya kuhamia ACT ni tofauti na Mange kumsifia kwa kuibua scandal aliyoisema..

Kumuhusisha Lissu na Maandamano ni sawa na kuhusisha maandamano na CHADEMA, hiyo inaondoa focus yake ya kuyaonesha kama "maandamano ya wananchi" Pasipo kutazama mitazamo ya kisiasa. Yani ccm vs chadema

Kingine Mange kubadilika ni kawaida yake, alimpigia promo Magufuli ila alivyoingia ikulu, akamgeuka kwa kuona anakiuka misingi ya demokrasia. Kitu hicho hicho kilochotokea kwa utawala uliopo

Kwa hiyo Mange amejitanabaisha kama si mtu anaeangalia mtu ila issue na misingi ya demokrasia anayoiamini

Kingine kutoa controversies/breaking news kubwa kubwa kwa Mange ni sawa na samaki kumtoa katika maji. Hicho ndio kitu kinampa upperhand na influence "kutoa habari exceptional and exclusive"..

Nadhani unabidi utafakari zaidi maana point nyingi zina weak bases

Japo siwezi kusema Mange hatumiki kwa sababu kuna baadhi ya info anazitoa unajua hii ni channel kubwa ipo nyuma yake. Kwa hiyo yawezekana watu baadhi wanamtumia kama channel kupitisha habari kubwa ambazo wao hawawezi kuzifikisha kwa watu openly.

Lakini bado haihalalishi madai yako unless utolewe uthibitisho wa yeye kupokea fedha ili aifanye kazi.
 
Zipi ni real issues, jambo moja ambalo litawafanya wananchi wachukue hatua kwa mtizamo wako na unataka lisemwe na nani?
 
Unaweza waza tofauti pia ila double agent unajuwa adhabu yake ni nini baada ya kazi kuisha? Mange si double agent kwa namna moja hajawahi badili msimamo wake na hata akibadili saiv it is too late maana kila mtu keshakuwa sumu
 
Mange kwa sasa ndo kiongozi mkuu wa CHADEMA akisaidiwa na Maria Sarungi. Heche na Lissu ni rubber stamps.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…