Sabato Njema!
1. Tulizoea kuona Wanamapinduzi wa kijeshi, yaani wenye mafunzo ya kijeshi. Vijeba na watu wa medani za kivita. Hasa physically
2. Lakini Dunia Kila Zama huja na mambo yake.
3. Mange Kimambi na genge lake ingawaje wanaonekana ni wanaharakati waliojikita na mambo ya siasa.
4. Lakini ukiangalia kimedani, mbinu wanazozitumia ni Mbinu za kijeshi za mapinduzi hatari ambayo hata wanaopindua nchi kwa mtutu wanasubiri, yaani wanaafadhali.
5. Mange na wenzake na hapa naona Wanawake wakiwa mstari wa mbele, Huku Mange Kimambi, kule Maria Sarungi, kushoto, Hilda Newton, juu Rachel Dangwa. Wote ni wanawake. Kila mmoja akiwa na style yake.
6. Hawa wanafanya mapinduzi ya fikra, wanazipindua fikra na akili za vijana huku wakichochea hasira, chuki, na nguvu ya vijana maskini kuona kwamba hawastahili kuwa masking
7. Katika Mapinduzi kuna Mauaji na umwagaji wa damu.
Mange kimambi wanafanya Character assassination kwa kiwango cha kutisha.
8. Kila jina litakaloingia katika mdomo wa Mange Kimambi linaenda kuchafuka na mhusika anajikuta akiwa ameuawa vibaya Character yake.
Kimedani kuna Msemo usemao,
If you loose money, you loose nothing.
If you loose health, you loose something
But if you loose character, you loose everything.
9. Ndicho Anachofanya Mange Kimambi kuua Adui zake character zao. Kuwapotezea Kila kitu.
10. Unajua mtu akishakuua character yako unakuwa haujabakiwa na kitu chochote. Unachanganyikiwa.
11. Kimedani mpaka sasa Mange Kimambi kama ingekuwa ni vita vile vya Kingdoms kama kwenye filamu basi yeye angekuwa jemadari heavy weight.
12. Miaka zaidi ya 10 sasa hakuna askari wa kiwango chake katika uwanja wa vita huko mtandaoni.
13. Na yeyote anayejiingiza kwenye mapambano anajikuta katika kuuawa Character. Jambo ambalo wengi wanaogopa kujiingiza katika mapambano naye.
14. Level aliyofikia Mange Kimambi, na kikosi chake imefikia hawezi shambulia mtu wa kawaida. Hii inawafanya wasipoteze nguvu nyingi bila sababu.
Wanarusha vyuma kwa viongozi wenye nafasi za juu tuu. Na sio Kila anayejitokeza.
15. Kama hii vita Wanaharakati watashinda. Mange Kimambi na kikosi chake atakuwa miongoni mwa wanawake watakaokumbukwa na historia na mchango wa wanawake hodari atakuwa mmojawao.
16. Ikiwa Hatashinda vita, basi historia itaandikwa kuwa alikuwa mwanamke mwenye sifa mbaya. Kama mjuavyo mshindi wa vita ndiye anayestahili kuandika historia. Au tuseme Mshindi ndiye huandika historia.
17. Fikiria Mange Kimambi angeongezewa power kidogo walau ya kusapoti hao vijana wake kifedha au silaha. Unafikiri ingekuwaje?
Kama sasa hana uwezo lakini ushawishi wake umemfanya awe juu Mahali ambapo hakuna yeyote kati ya adui zake anayeweza kufikia tawi lake.
18. Mange alichofanikiwa ni kumudu kutumia udhaifu wa adui zake na kuugeuza kama silaha.
Alafu Adui zake wanaudhaifu wa kuonyesha madhaifu yao.
Nawatakia Sabato Njema.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam