Mange Kimambi: Viongozi wa Chadema walio baki nje hawafikii hata nusu ya Lissu

Mange Kimambi: Viongozi wa Chadema walio baki nje hawafikii hata nusu ya Lissu

Soma thread nzima hapa;-

Kwanini unaita umbeya wakati iko kwenye akaunti yake ya Twitter;-


View attachment 3611939View attachment 3611940
Anakosea anaposema Chadema ni kama kinaongozwa na wanawake. Bawacha siku zote ilikuwa mstari wa mbele kupigania haki za watanzania. Wakina Halima, Salome, Catherine, Husna walikuwa wanapambana bila uoga. Hii hali ya sasa ilisababishwa na Lissu mwenyewe kwa kuona wote waliotofautiana nae kuwa maadui. Wapambanaji wengi wamehama chama na wale waliobaki sijui kimewapata nini. Kwa kweli inabidi wajipange upya.

Amandla...
 
Kwamba hata akiwa upande fulani na huo upande ukikosea asikosoe?
Asifie hadi makosa kisa yupo huo upande?
Lakini akumbuke kila mtu ana pande mbili, kwa sasa ni mda wa kupigania haki ili kuwaondoa wadharimu walioko madarakani. Ni mda wa kuungana na kuwa kitu kimoja na sio kujigawa na kuwa makundi kisa mtu flani ana hofu ya kusema kisa ataitwa Polisi.
 
Lakini akumbuke kila mtu ana pande mbili, kwa sasa ni mda wa kupigania haki ili kuwaondoa wadharimu walioko madarakani. Ni mda wa kuungana na kuwa kitu kimoja na sio kujigawa na kuwa makundi kisa mtu flani ana hofu ya kusema kisa ataitwa Polisi.
Kwamba aungane kufanya makosa?
 
Mnyika ana akili sana mange yeye kama raia siakusanye watu waandamane

Chadema wao watapanga mana lazima kamati kuu ikae itoe maamuzi
 
Stuxnet, mshangiliaji wa vifo vya waTanzania, leo ndiye Mweneza habari wa Mange Kimambi leo?

Kama hapo hakuna jambo kuna nini?

Huyu Binti ni dish linaloyumba. Huenda kafikiwa na tapeli Thabiti Kombo; na pengine hata Nchimbi.

Hamza Johari alipokabidhiwa rudishwa kazini alitangaza kazi ya kwanza aliyopewa ni kumrudisha huyu Binti.
Sasa tuseme hii ndiyo aina ya kumrudisha?
Baada ya Mswada kupamba moto, wameona njia rahisi ni kumnunua.
 
Kaongea ukweli 100%

Chadema bado wana ufala sana.

Lissu angekuwa ccm, Tz ingebahatika kupata JPM wa pili ila ndo hvy yupo sehemu isiyosahihi mana amezungukwa na waoga.
Mada za namna hii zinachuja nafaka na pumba, bila ya wasiwasi wowote.
Hata sijui kama utaelewa nilichoandika hapa.
 
I’m sorry ila acha niseme tu ila ni hivi, kama viongozi wengine wa Chadema wangekuwa mwenyekiti wao haki tungekuwa tumepiga hatua flani kwenye movement.

Lissu ni zaidi ya mwaka sasa anapitia mateso yasioelezeka na kagoma kuwauza Watanzania ili apate freedom. Ila hawa viongozi wenzake walio uraiani wanaogopa hata kuitwa polisi.

Wanaogopa hata kuitisha maandamano ya kumpigania Mwenyekiti wao atoke. Dunia nzima inachukua action ili Lissu atoke, dunia inapitisha miswada, inafutwa misaada ya TZ juu ya Lissu na human rights ila Chadema hawachukui action zaidi ya maneno kwenye masteji tena maneno ya uoga uoga, wanahakikisha sio maneno ya kuitwa central.

Tatizo uongozi mzima kasoro Lissu wako soft. They are too soft kuleta ukombozi. Chama kizima kinafanya siasa za uoga kasoro mwenyekiti wao.

Atakaechukia kwa statement zangu, chukia ikisha pasuka, tena ukiweza ni block kabisa, Mimi sina chama na sipiganiii chama chochote, nachopigania ni Watanzania kupata HAKI na ACCOUNTABILITY then wao watachagua wenyewe chama chao na viongozi wao. So napoona the only people tunaowategemea kutupigania wanaonyesha uoga wa level hizi nakosa amani ya roho.

TunduALissu Mungu akupiganie utoke, uje urudishe uanaume kwenye hiki chama. Maana sasa hivi ni kama chama kinaongozwa na wanawake maana sio kwa u-soft huu.
Kuna neno lolote katika hayo ambalo amekosea kusema kwani?

Ninachokushangaa, proSamia leo iweje kanena haya kupitia mikononi mwako, au wamekuhack?

Kweli binadamu hubadilika na urafiki wa kisiasa si urafiki wa kudumu, unabadilika muda wowote!
 
Mange Kimambi is not a politician hajui chochote,akili ya Mnyika na Chadema ni kubwa wacha wananchi ndiyo waongoze maandamano na siyo CDM vinginevyo watajinasa. Polical Science is a science
Nakubaliana na yote uliyosema hapa, isipokuwa hayo maneno machache uliyomaliza nayo kwenye mstari wa mwisho.

Hakuna sayansi ya kipuuzi namna hiyo.

Whoever assigned the word science to that field of study must have been drunk..
 
Mange naye ni kama amepoteana.

Hajui ashike lipi, au afanye nini??

Analaumu kila mtu
Kuonyesha ni kiasi gani waTanzania wamekwama, ni kuangalia mtu kama huyu binti nay anawekewa matumaini katika kuchangia ukombozi wa taifa hili.

Kiwango chetu kimeporomoka sana.

Ukiangalia ndani ya CCM yenyewe, akina Makonda ndio tegemeo ndani ya CCM.

Sijui Tanzania itatoka vipi katika mkwamo huu..
 
Mange kuongea ukweli 100% watanzania ni watu ambao ni wajinga sana

Kupoteza muda na rasilimali zako kuwapambania ni kitu ambacho hakina maana.

TAL anapoteza muda wake bure hakuna ukombozi Atakuja kuuleta hapa TANZANIA zaidi ya EGO .
 
Shida yetu sisi waTanzania huwa tunapenda kusikia tunavyovipenda haijalishi ni ukweli au uongo.
Mimi binafsi huwa naona CCM haiwezi kutoka madarakani sababu hakuna chama ambacho kipo Tayari kuiongoza nchi hii(Kimejipanga kwa hilo).
 
Back
Top Bottom