Mange Kimambi: Viongozi wa Chadema walio baki nje hawafikii hata nusu ya Lissu

Mange ni opportunist tu kama Sarungi, fatma karume, na kigogo, walimpinga sana JPM cha ajabu alipoingia Samia wakawageuka wapinzani na kuanza kuimba mapambio. Alipogusa tu maslahi yao ndio nao wakaanza tena kumpinga so hawa hawaaminiki kabisa. Kama anaona ni waoga aje bongo aongoze maandamano.
 
Mlete hapa aseme mwenyewe kwa mdomo wake, acha kumsemea.
 
Wewe unaifahamu namna viongozi wa Chadema wanavyowindwa? Watoke front wote huoni itakuwa mbaya na chama kinaweza kupotea. Ila Chadema tupo na Mungu. Hakuna kulala.
 
Sasa anataka wote waishie jela nani ataongoza chama,kazi wanayofanya kwenye hiyo mikutano siyo ndogo wanawaandaa watu kuja kufanya mambo makubwa, watawala wenyewe hawapati usingizi kwa jinsi watu wanavyoitikia mwito na kuelewa samo.
Kazi inayofanywa ya mikutano ni kubwa sana saana.
 

simunamwita dada wenu wa taifa
 
Mange hajawahi kuwa mwenyeji wa Samia Marekani. Alienda kumsalimia rais wake kama ambavyo Lissu alivyofanya Ubelgiji. Na hata kama ni CCM, watu wanabadilika. Mfano ni Polepole ambae hakuwahi kutoka CCM.

Amandla...

Polepole hakuwahi kabisa kubadilika
 
CCM kuporomoka ndio nguvu ya kina Mange na Maria.

Akipatikana mtawala mwenye akili timamu, wala hoja za kina Mange haziwezi kuwa na nguvu ya ushawishi.

Shida kubw aya CCM kwasasa ni rushwa, nepotism kubwa na uchawa.

Wanaokota okota watu useless kwasababu ya NEPOTISM, RUSHWA na Uchawa wanawapa uongozi halafu wanategemea mfumo wa dola ndio uwabebe.

Katika mazingira hayo, lazima watu waanze kumsikiliiza Recho Dangwa
 
Mange ajui tu chadema wanayo ya pitia huku mitaani,,,

Wanakufa wanatekwa na wanafungwa sana.

Cccm imewekaza nguvu zake zote kwa chadema kuhakikisha inafutika.
 
Mange ajui tu chadema wanayo ya pitia huku mitaani,,,

Wanakufa wanatekwa na wanafungwa sana.

Cccm imewekaza nguvu zake zote kwa chadema kuhakikisha inafutika.
Ni kama hajaridhika na shurubu wanazopitia CHADEMA; sasa anataka wajinyonge wenyewe moja kwa moja ili hao wanaomtuma kuchochea CHADEMA kujinyonga wamalize kazi.

Huyu siyo mpambanaji wa kuaminiwa.
 
CHADEMA wajitafakari, nyomi mikutanoni haziitishi CCM, imeshazizoea. Waitishe maandamano makubwa ya amani. Huu ndo wakati muafaka ambao CCM na serikali yake wako kikaangoni.
Maandamano si ni haki ya chama cha siasa?, kwa nini CHADEMA hawaitumii kama wako serious?
 
Hata Mimi ndiyo huwa namuona huyu Dada akili zake sio timamu. Yeye anaongea hayo yupo USA halafu anazungumzia viongozi wa CHADEMA kuwa ni wanawake?... Watanzania msiingie huu mkenge.. Hawa ni matapeli wa wanufaika na ujinga wenu period!
 
Watanzania ni gullible sana, yaani wanafanya vitu kwa mihemko tu, sasa Mange yeye ni nani mpaka awape viongozi go ahead?.. Hii Nchi ina upumbavu mwingi sana
 
Actually, kuna tofauti kubwa kati ya hao wawili, Mange na Maria. Pengine hujawapa muda wa kuchambua uzito wa kila mmoja wao upoje.
Maria yupo ngazi tofauti kabisa na huyo Mange katika hizo hoja unazozigusia wewe.

CCM kama ilivyo sasa, siyo chama cha siasa tena, imetekwa na kundi la watu wasioguswa kabisa na maslahi ya nchi hii na watu wake. Kwa hiyo wapo tayari kutumia nguvu zote, kama walivyofanya Oktoba kulinda maslahi hayo.
Bila ya kuliangamiza kundi hili, Tanzania haiwezi tena kuwa na mategemeo ya utulivu.

Ni lazima ipatikane njia ya kulitokomeza kundi hili; na kwa vile njia wanayotumia ni mabavu na kuua, huenda ikabidi njia hizo hizo zitumike kuliangamiza hili kundi. Vinginevyo, Tanzania haina matumaini.

Recho Dongwa?
 
Aaah wapi. Bado wataona tu kasoro, labda waongozwe na Malaika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…