Waarabu ndio wako hivyo, naweza fumba macho na kusema hamna haja ya kuwalaumu kwani ndivyo mfumo wao wa maisha unavyoenda. Waarabu wao wanaamini sana katika makabila, mwingereza alishangaa sana alivyoenda kuwaunganisha ili wampige mturuki kwenye vita ya pili ya dunia. Kuna kabila linaitwa beduli wanaonewa sana yaan haruhusiwi hata kunywa maji kwenye kisima alichochimba mwarabu mwingine akinywa hujumu ni kifo! Kuna jamaa yangu alienda kule anakwambia watu wazima wala hawatii hofu bali ni watoto wao, anasema unaweza lambwa bonge la kofi pasipo sababu yoyote ukikunja sura tuu ujue unaloo.