Manyara: 8 mbaroni kwa kushangilia kifo cha Magufuli

Manyara: 8 mbaroni kwa kushangilia kifo cha Magufuli

Wakazi 8 wa Mererani Wilaya Simanjiro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kukejeli na kushangilia kifo cha Rais John Magufuli.

Rais John Magufuli amefariki Machi 17 kwa matatizo ya moyo na atazikwa Machi 26, Chato, Mkoani Geita. Taifa lipo katika maombolezo ya siku 21, huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
hata ww naona unashangilia kimoyo moyo
 
Mtaa upi huo nduguyangu hata huhisi aibu?
Dah kweli ushabiki ni kitu kibaya sana.

Labda mtusaidie uko mtaani kwenu mzee aliwakosea nini
Habari ndiyo hiyo ndugu.

Huku mtaani kwetu watu ni furaha tupu - sijui wanaofurahi wanafurahia nini kwa kweli - lakini wana furaha iliyopitiliza aisee!
 
Yani Hapa kuna jamboo litakujaa mnaweza semaa Hivi Mama Samia roho mbaya hii kaitoa wapi???? Lakini kitu ninachoweza kuwaambia watu Ufisadi kurudi na wizi wa mali za watanzania ni rahisi sana kuliko Kuondoa sheria kandamizi za Habari na Uhuru wa kutoa maoni... Watu wataumia sanaa tu maana Nchi ipo chini ya CCM na Kwa bongo Rais pekee alieweza kufanya mambo kinyume na matakwa na akili za CCM ni Magufulu tu waliobaki hawa Hawana la kusema against maamuzi ya CCM kabisa.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app

Kwahiyo unataka tumfufue au?
 
Nimeona kwenye mitandao Polisi wakikamata watu kwa tuhuma zakushangilia kifo. Naomba kujiuliza ni sheria gani inayotumika kufanya huu ukamataji? Nikifungu gani kinachotamka ili ni kosa?

Kama kifungu hicho kipo, je kinatumika kwa viongozi tu au hata raia wakawaida? Ningetamani kukijua ili jamii iweze kukitumia pale wanapopoteza wapendwa wao nakutokea watu wanaosherekea.
 
Nimeona kwenye mitandao polisi wakikamata watu kwa tuhuma zakushangilia kifo. Naomba kujiuliza ni sheria gani inayotumika kufanya huu ukamataji? Nikifungu gani kinachotamka ili ni kosa?

Kama kifungu hicho kipo, je kinatumika kwa viongozi tu au hata raia wakawaida? Ningetamani kukijua ili jamii iweze kukitumia pale wanapopoteza wapendwa wao nakutokea watu wanaosherekea.
Sijui kwa kweli... kama kuna sheria hiyo ila si uungwana kufanya sherehe kwa msiba au madhila ya wengine. TULIPATA KUANDIKA HUMU WATU WALIPOSHANGILIA MADHILA YA TL NA WENGINEO TUKASEMA MBEGU MBAYA INAYOPANDWA TUTAIVUNA... Au labda ni watani wa jadi au wajukuu maana ndio hushangilia na kucheza misibani.
 
Nimeona kwenye mitandao polisi wakikamata watu kwa tuhuma zakushangilia kifo. Naomba kujiuliza ni sheria gani inayotumika kufanya huu ukamataji? Nikifungu gani kinachotamka ili ni kosa?

Kama kifungu hicho kipo, je kinatumika kwa viongozi tu au hata raia wakawaida? Ningetamani kukijua ili jamii iweze kukitumia pale wanapopoteza wapendwa wao nakutokea watu wanaosherekea.
Sheria hiyo haipo.Hata kama ingekuwepo isingesaidia wanyonge. ingelenga kunufaisha watawala,kwani watunga sheria ni wao,kama haina masilahi kwao hawaileti ng'o!
 
Kwahiyo wote tulie kwa kupenda au kwa lazima.
or78yhntaij21.png
 
Back
Top Bottom