Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 80 na Majeruhii 133
Serikali imetoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na mawe kutoka mlima Hanang Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara, ambapo imesema hadi kufikiasaa 6:00 mchana leo December 08,2023 idadi ya vifo imefikia 80 (Watu wazima ni 48 wakiwemo Wanaume 19 na Wanawake 29) na Watoto ni 32 (wakiwemo wa kiume 15 na wa kike 17).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali akiongea leo Katesh, Hanang, Manyara amesema “Mwili mmoja wa Mtoto wa kiume ambao ulikuwa haujatambuliwa hadi jana sasa umetambuliwa lakini kuna mwili wa Mwananke mmoja Mtu mzima uliopatikana leo ambao bado haujatambuliwa, hivyo jumla ya maiti zilizokwishatambuliwa hadi sasa ni 79.

”Kwa jumla hadi kufikia saa 6:00 mchana leo, idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali zetu Mkoani Manyara ilifikia 133 (Watu wazima 71 na Watoto 62, kwa mujibu wa agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waathirika wote wanatibiwa bure na pia serikali inagharamia mazishi ya waathirika wote”.
 
Wewe umewahi kufika tu lakini mimi huko ndo nyumbani kwetu...

Kama ni sehemu salama imekuwaje watu wamelambwa,na maporomoko (landslide) hayo.?

By the way, hoja yangu kwa ndugu niliyemkwoti ilikuwa ni yeye pengine "kutojua kabisa jukumu la serikali"..

Ndiyo maana nikatoa maelezo marefu kidogo kumkumbusha. Na ishu siyo Hanang - Katesh tu. Ni maeneo mengi ya miji na vijiji Tanzania watu wanaishi kwenye maeneo hatarishi kupindukia na bado mamlaka za kiserikali zinazohusika zikiangalia tu pengine mpaka waje wafe watu kama huko Hanang...

Nikatoa mfano wa Jiji la Mwanza (maana ndo naishi huku Kwa sasa). Kwamba, Kuna watu wanajenga nyumba tena za udongo wa kawaida kabisa kwenye vilele vya miinuko ya milima...

Serikali ipo na inatoa mpaka vibali vya ujenzi na inapeleka huduma zingine za kijamii kama maji na umeme huko..

Swali la kujiuliza ni hili;

Kwamba ina maana Tanzania tuna uhaba wa ardhi salama, ya kawaida na tambarare kiasi cha watu wa kawaida kujenga makazi kwenye maeneo hatari kama milima, mabonde nk nk? Au ni serikali kukosa mipango thabiti tu?

Ni wazi kuwa iko shida serikalini..
Kwenu ni sehemu gani hapo, na ni kwa nanu ili nikupe ramani yote, halafu uniambie nani amejenga sehemu hatarishi, watu wameishi hapo toka miaka ya 1950 hawakuwahi kuona jambo kama hilo.

Usifananishe ujenzi holela wa mwanza na huko hanang.
 

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A mud flow is a geologic phenomenon whereby a wet, viscous fluid mass of fine-to-coarse-grained material flows rapidly and turbulently downslope, usually in a drainageway. Typically a torrential rainfall or very rapid snowmelt runoff is the initiating factor.

Landslides are a type of "mass wasting," which denotes any down-slope movement of soil and rock under the direct influence of gravity. The term "landslide" encompasses five modes of slope movement: falls, topples, slides, spreads, and flows.
 
Wachache ingekufaa familia yako yote labda ndo ingekuwa watu wachache...!!
Aisee nimeshangaa pana watu wa ajabu sijapata kuona sema stress zinawafanya vijana kuandika chochote mtu alietimia hawezi kuandika vile...
 
Mwanza kaeni kwa tahadhari
Mwanza landslide haiwezi kutokea. Milima ina miamba mikubwa inayoshikilia ardhi. Landslide hutokea kwenye milima isiyokuwa na miamba. Ardhi inakunywa maji mpaka inakuwa tepe tepe hivyo inaanza kuslide.
 
Back
Top Bottom