Serikali imetoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na mawe kutoka mlima Hanang Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara, ambapo imesema hadi kufikiasaa 6:00 mchana leo December 08,2023 idadi ya vifo imefikia 80 (Watu wazima ni 48 wakiwemo Wanaume 19 na Wanawake 29) na Watoto ni 32 (wakiwemo wa kiume 15 na wa kike 17).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali akiongea leo Katesh, Hanang, Manyara amesema “Mwili mmoja wa Mtoto wa kiume ambao ulikuwa haujatambuliwa hadi jana sasa umetambuliwa lakini kuna mwili wa Mwananke mmoja Mtu mzima uliopatikana leo ambao bado haujatambuliwa, hivyo jumla ya maiti zilizokwishatambuliwa hadi sasa ni 79.

”Kwa jumla hadi kufikia saa 6:00 mchana leo, idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali zetu Mkoani Manyara ilifikia 133 (Watu wazima 71 na Watoto 62, kwa mujibu wa agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waathirika wote wanatibiwa bure na pia serikali inagharamia mazishi ya waathirika wote”.
 
Kwenu ni sehemu gani hapo, na ni kwa nanu ili nikupe ramani yote, halafu uniambie nani amejenga sehemu hatarishi, watu wameishi hapo toka miaka ya 1950 hawakuwahi kuona jambo kama hilo.

Usifananishe ujenzi holela wa mwanza na huko hanang.
 

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A mud flow is a geologic phenomenon whereby a wet, viscous fluid mass of fine-to-coarse-grained material flows rapidly and turbulently downslope, usually in a drainageway. Typically a torrential rainfall or very rapid snowmelt runoff is the initiating factor.

Landslides are a type of "mass wasting," which denotes any down-slope movement of soil and rock under the direct influence of gravity. The term "landslide" encompasses five modes of slope movement: falls, topples, slides, spreads, and flows.
 
Wachache ingekufaa familia yako yote labda ndo ingekuwa watu wachache...!!
Aisee nimeshangaa pana watu wa ajabu sijapata kuona sema stress zinawafanya vijana kuandika chochote mtu alietimia hawezi kuandika vile...
 
Mwanza kaeni kwa tahadhari
Mwanza landslide haiwezi kutokea. Milima ina miamba mikubwa inayoshikilia ardhi. Landslide hutokea kwenye milima isiyokuwa na miamba. Ardhi inakunywa maji mpaka inakuwa tepe tepe hivyo inaanza kuslide.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…